Gharama ya usafiri kupitia ATCL kuanzia KIA mpaka Dar ni laki 8+ haya ni maajabu

Gharama ya usafiri kupitia ATCL kuanzia KIA mpaka Dar ni laki 8+ haya ni maajabu

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
5,559
Reaction score
8,747
Ila kuna mambo huwaga yanashangaza sana imagine dunia kote watu wanaumiza kichwa kupunguza gharama za usafiri ila habari ni tofauti sana ukija Tanzania

IMG-20260929-WA0000.jpg

Kutoka Kia mpaka dsm bei ni laki 8 kupitia ATCL haya ni maajabu makubwa sana kwenye dunia ambayo inapambana kupunguza gharama

Nchi yeyote ile dunian lazima ipunguze safari za usafiri mdani ya nchi ili kurahusisha biashara ndani ya nchi ndo maana nchi kama china gharama za usafiri ndani ya nchi ni ndogo sana na hii imewasaidia ila hali ni tofauti na Tanzania

Kuna mambo kama nchi tuyaangalie kwa upana ila tokea wakati wa utawala wa magufuli alipoamua kuanzisha shirikia la ndege nilipinga approach na economic model alizokuwa anatumia sio sustainable

Mfano tungeendela na business model ya kina fastjet bali leo hii gharama ya usafiri wa ndege ingekuwa chini zaidi ila tokea ATCL wawe na monopoly bei zimepanda maradufu
 
Nini kifanyike ila ATCL waingize faida
Ili sector ya ndege iwe na faida angalau kuwe na watanzania million 10 wanaoweza kupanda ndege kwa hii idadi wakiwa wanaweza tumia ndege basi shirikia litakuwa linapata faida maradufu ila hii business model bei inatakiwa ndogo mfano arusha to dsm elfu 80, yaani kusiwe na nauli ya kuzidi laki moja na nusu 150,000 kwa sehemu yeyote ndani ya nchi
 
Johannesburg kwenda Durban unafika saa saba na nusu Oliver Tambo unakata ticket ya ndege nusu saa mbele uondoke unalipia rand 700 mpaka 900 haifiki hata 160,000 Tsh na ndege zinajaa zile balaa..
Tanzania kodi tu ya Ticket moja inafika Tsh 100,000 bado gharama zingine niliwahi kutaka kwenda Songea haraka kutoka Daslm walitaka nauli ya Ticket moja laki sita sawa na nauli ya Harare Lusaka au JHB kwa Malawi Air.
 
Tulitakiwa tuwe na treni za kisasa za umeme zinazounganisha majiji, tuwe na ndege halafu mafuta bei nzuri ili kila mtu awe mfanyabiashara. Unapanda treni chap umeingia mbeya unakodisha shamba ukivuna kuna treni ya mizigo unapakia mzigo unashushwa Arusha, Mwanza na Dar ndani ya siku moja.
 
Johannesburg kwenda Durban unafika saa saba na nusu unakata ticket ya ndege nusu saa mbele uondoke unalipia rand 700 mpaka 900 haifiki hata 160,000 Tsh na ndege zinajaa zile balaa..
Tanzania kodi tu ya Ticket moja inafika Tsh 100,000 bado gharama zingine niliwahi kutaka kwenda Songea haraka kutoka Daslm walitaka nauli ya Ticket moja laki sita sawa na nauli ya Harare Lusaka au JHB kwa Malawi Air.
Ni flight ya masaa mangapi? Kia to dar 800k is a joke. 800k ni trip ya Dubai one way
 
Kuna route ya DSM - Mwanza nililipa atcl shilingi 525,000 one way

Kwa ufupi, gharama za kusafiri na ndege Tanzania ni kubwa hadi watu wanahisi ni anasa kupanda ndege 🙌
Kubwa mno. Imagine dar Dubai return ticket mpaka 1.2m unapata, Sasa flight ya lisaa kimoja eti laki nane. Round ticket ya dar kia ikizidi ni 400k. One way ni 200k
 
Kubwa mno. Imagine dar Dubai return ticket mpaka 1.2m unapata, Sasa flight ya lisaa kimoja eti laki nane. Round ticket ya dar kia ikizidi ni 400k. One way ni 200k
Ndiyo maana nimesema hapo juu, ni kukosekana kwa ushindani wa kibiashara

Yule Fast Jet aliijulia hii biashara, bei nafuu ya nauli kwa Kila route
 
Ni flight ya masaa mangapi? Kia to dar 800k is a joke. 800k ni trip ya Dubai one way
Pale kama sio mbali ila Kia to Dar ni karibu mimi kuna vitu home huwa hata sijisumbui kuuliza labda Mbeya to Dar naona nauli zao ni reasonable hiyo nauli ya SA wao ndio wapo juu kuliko Flight zote..
Watanzania wanajificha na Rwanda air,Malawi au AirLink.
 
Sio wamekosa ushindani wao wana mawazo ya kizamani ndege lazima iwe juu gharama zake wakati sio kweli.
Ni kweli Mkuu, ingekuwa mashirika ya ndege ya nje yanaruhusiwa kupiga route za humu ndani, mbona atcl ingekosa abiria labda kwa safari za wakubwa tu
 
Back
Top Bottom