KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wakuu Kwema? Bila shaka muko salama.

Mwezi uliopita Nilikuwa Hospitali ya Taifa ya Mloganzila, Baada ya mke wangu Kuhamishiwa hapo baaada ya Kupewa Rufaa kutoka Kituo cha Afya ambapo alienda Kujifungua. Alienda Hospitali ya kawaida baade madaktari wakashauri awahimishwe Hospitali ya Taifa Mloganzila.

Kitu ambacho Nimeona Gharama za pale ni kubwa sana ni kama Hospitali za Watu Binafsi au Taasisi za Dini n.k

Wakati anapokelewa Pale Emergence nilitakiwa Kulipia Laki moja Fedha Taslimu ambayo wanaita ni ya Accomadation na haina maelezo mengine tena unapewa Control number ulipie ndio aanze Kuhudumiwa.

Baada ya Hapo alijifungua salama watoto wawili Mapacha alikaa siku ya Ijumaa hadi Jumatatu yaani Siku tatu Tu nikapewa Bill ya 1.35 yaani (Milioni moja laki tatu na elfu thelathini na tano) Nikasita kulipa nikaenda kwa wahasibu Kugombana nao Kidogo nikitaka Ufafanuzi japo Ilishindikana.

Baadae niliuliza Nikaambiwa Ghrama ya Kulala kwa Siku ni 50,000 lakini gharama ya Kujifungua ni 750,000. Niliambiwa Hiyo ssera ya mama wajawazito wanajifungua Bure haipo ni Siasa na Propaganda Tu.

Nilipambana nikalipia kiasi nikatoka.

Lakini kwa Kifupi Gharama Za Hospitali ya Mloganzila Ni kufuru kule ndani nilikuta akina mama waliojifungua wana Daiwa Wengine Millioni tatu, tano na kuendelea wameshikiliwa wake pale hadi fedha ipatikane.

Kwa kweli jambo hili linaumiza sana watanzania wa hali ya Chini ambao Kimsingi wanaamini Hospitali za Umma zinazoendeshwa naKupata Ruzuku kutoka serikalini ambayo ni kodi za wananchi gharama zake ziwe rafiki ili kila mwananchi aweze Kumudu ila imekuwa ni Tofauti.

Soma Pia:Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza

WIZARA YA Afya Aid Inatakiwa ilitazame hili na wawaweke wananchi wazi kwamba ile ni Hospitali ya Kulipia .

Ushahidi wa Nyaraka zote nianzo Mods musifute mukitaka ushahidi wa Receipt na Bill nitawapa
Duh
 
Watu wajifunze kulipia gharama za afya, hasa kwa vitu vya kawaida kama kujifungua. Mkuu ulitaka mkeo alazwe mlagonzira na ajifungue bure?
 
Nitaifatilia hiyo Jubilee
Hiyo bima ukilazwa kila asubuhi unaletewa maua na mratibu wa hiyo bima kwa hospital husika.

Nililazwa ward ya peke yangu, kuna sofa TV imeungwa na DSTV package ya juu zaidi, friji wanakuletea fresh juice na maziwa, breakfast kila asubuhi na button ya kengele ya kumuita nesi muda wowote.

Washroom classic hata hiyo breakfast unaweza kula humo. Upande wenu wa hizo ward mtu haingii kama hana id kuonyesha anaenda kwa nani.

Changamoto ni kwamba hospital wanataka wakae na wewe muda mrefu ila mratibu wa bima hataki ukae sana 😅 kwa siku nne za kua pale kwa kuumwa malaria ikaonekana nimetumia zaidi ya 3M.

Kuna bima ukizionyesha tu hospital cha kwanza ni kulazwa hata kama 😅 umejikata
 
Hiyo bima ukilazwa kila asubuhi unaletewa maua na mratibu wa hiyo bima kwa hospital husika.

Nililazwa ward ya peke yangu, kuna sofa TV imeungwa na DSTV package ya juu zaidi, friji wanakuletea fresh juice na maziwa, breakfast kila asubuhi na button ya kengele ya kumuita nesi muda wowote.

Washroom classic hata hiyo breakfast unaweza kula humo. Upande wenu wa hizo ward mtu haingii kama hana id kuonyesha anaenda kwa nani.

Changamoto ni kwamba hospital wanataka wakae na wewe muda mrefu ila mratibu wa bima hataki ukae sana 😅 kwa siku nne za kua pale kwa kuumwa malaria ikaonekana nimetumia zaidi ya 3M.

Kuna bima ukizionyesha tu hospital cha kwanza ni kulazwa hata kama 😅
Hahaha yani Malaria wanataka wakulaze🤣
 
Mkuu, ulikuwa unajipinda tu kwa shemeji huku mnashangilia, ulitakiwa kujiandaa mapema, yaani unaona mavifaa ya kisasa yamejaaa humo yanang'weka mataa, unaware unachekelea tu
Chiembe Hkauna aliyetaka Bure shida ni gharama Kubwa. Wewe ni Mtanznaia unaelewa uhalisia wa amisha yetu Mtu unaandaa 500k Kwaa ajili ya Kujifungulia unaletewa Bil ya 1m+ Plus na munawaaminisha watu hizo Huduma ni Bure kabisa.

Hoja Kubwa gharama zipunguzwe kuzaa sio anasa.

Matozo na Kodi kibao lakini Huduma za afya bado zipo juu.
 
Umeandika ujinga, uliposema wizara ya afya itazame, watazame nini unadhani hawajui hawa kenge, adui wa mtanzania wa kwanza ni viongozi wetu..
Wanaishi kwenye ule usemi mwenye shibe hamjui mwenye njaa.. Wao wanapata huduma zote bure, maji bure, umeme bure, makazi bure, afya bure tena daraja la juu kabisa, usafiri na mafuta bure Na bado wanapiga dili za kuiumiza nchi.
Sasa mtu kama huyo ataumia akisikia mafuta lita 2900 ama hata ikiwa 4000, atalalamika gharama za umeme, ama ukosefu wa maji. Atahisi huduma za afya ni mbovu na ghali?
 
Kam alisomea ualimu alipaswa kujal zaid kwakuw aliwah kuishi maish magumu
Sio ishu ya kujali tu. Ungekua kwenye sekta ya afya ungenielewa.

Ukiingia mikoani ndanindani maisha ya watu n magumu na hali ya chini ambao hata hawawezi ku afford bima ya afya.
Akija hospitali hanakuwa hana pesa cash bali snasema ana mazao ambayo akiuza ndo ataleta pesa na hspo huwezi kumtibu mtu ukampa dawa pamoja na vipimo bure
Sasa yeye kasomea ualimu ana experience na sekta ya afya na yanayotendeka on the ground. Kwanini wasiwe wanamchagua Daktari ambae kasha kaa hospitalin na anaexperience ya bima inavyofanya kazi, malalamiko ya wagonjwa na ugonjwa kwa ujumla.

Kuna watu wanakuja hospitalin wanaumwa figo au figo zimefeli ukimuhoji anasema kameza panadol miezi miwili alizo kuw ananunua duka l dawa kwa sababu lalosa hela ya kutibiwa hospital. Ayo kama ujasomea afya na kukaa hospotal huwez kuya jua na kukutan nayo

Kuna watu wana hali ngumu kiuchumi. Unakuta bodaboda kapata ajali akavunjika mguu. Kakaa hopital mwezi bila pesa na ata ndugu wa kumsaidia mpaka mguu unaoza. Ayo ukisomea ualimu utayajua au kukutan n scenario za hivyo. .

Kupitisha Bima ya afya ni furaha kwa asiyeijua . Ila kwa sisi wazoefu wa hio sekta
Kuna dawa zinakuwa hazitolewi kupitia bima kisa bei yake ni ghali, kwa bima tu uwezi kuafanyiwa upasuaji mpaka utoe na cash,
Kwa bima tu huwezi kupata vofaa kama miwani na magongo kwa wanaohotaji.
Kama umesoma afya na una experience na hivyo vitu huwezi kaka kimya bungeni mswaada wa afya ukipitishwa kwani unajua effect yake kwenye jamii na hospitali lwani experince na scenario za huko unazifahamu.
 
Sio ishu ya kujali tu. Ungekua kwenye sekata ya afya ungenielewa.

Mkuu umeandika Point sana, wachache watakuelewa
 
Kwa kuwaa umesema ullienda private hospital ghalama kuwa kubwa sio jambo la ajabu hasa kama operation zinahusika. Lakini kufika 5M ni wewe ulitengeneza mazingira hayo ingewezekana kuishia 2.5M. Kwanza kwa nini uende hospital ikutoze 2M halafu bado Daktari utafute wewe umlipe 2.5M? Ilitakiwa huyo Daktari kama anahusika na hiyo hospital ulipompa hiyo 2.5M mengine yote amalize kwenye bajeti hiyo.

Tunaposema ghalama za kujifungua tunahusisha ghalama za kuzalisha, malazi na dawa. Ghalama huongezeka kulingana na complication za mimba . Operations nyingi zina ghalama hivyo haiwezi kuwa tofauti kwenye kujifungua. Mwanamke akijifungua kawaida ghalama huwa ndogo.

Changamoto inakuja umeandaa 400,000 kama akiba ya kujifungua kawaida unafika hospital unaambiwa hawezi kujifungua kawaida anatakiwa operation. Hapo tayari tunakuwa tunazungumzia 1M+.

Lakini pia kwa upande wa hospital za serikali mambo mengi yanahusika. Unamtoa mgonjwa kutoka hospital ya mkoa kama temeke na kwenda hospital ya Rufaa ya taifa. Hapa lazima ghalama zibadirike. Mpaka kufika Mhimbili unakuwa umeruka vituo vingi vya afya. Sasa hapa itategemea Rufaa ya kuhamisha imeandikwaje. Ukienda Mhimbili bila rufaa ya hospital za chini yake unapigwa ghalama kama za private hospital na hakuna wa kumlilia. Pia kuna chumba alicholala kinaongeza ghalama za kujifungua. Huwezi kuwa private room ghalama zikawa chini..

Jambo la msingi ni kuhesabu ghalama kabla ya maamuzi yoyote. Lakini pia ni vizuri kuandaa Daktari mapema ambaye atakuwa anamfanyia chekup mpaka wakati wa kujifungua kama uwezo unaruhusu ili kuepusha taarifa za kushtukiza
Yeah nakuelewa
Gyno huwa anafanya kazi hospital kubwa na analipwa kwa saa. She spent five hours kumfanyia operation mama mtoto.

Na kama nilivyosema presha yake mama haikuwa sawa ilikuwa ni kazi kubwa sana

I was hanging out on this chance bro. Ungekuwa hapo ungeelewa. Kikubwa mtoto yuko salama mama yuko salama...
 
Nakuelewa bro I have been through hali hii ambayo huwezi kwepa ghalama ili kuokoa uhai
Yeah nakuelewa
Gyno huwa anafanya kazi hospital kubwa na analipwa kwa saa. She spent five hours kumfanyia operation mama mtoto.

Na kama nilivyosema presha yake mama haikuwa sawa ilikuwa ni kazi kubwa sana

I was hanging out on this chance bro. Ungekuwa hapo ungeelewa. Kikubwa mtoto yuko salama mama yuko salama...
 
ni muhimu ila watu walio na bima wanateseka sana. Utaambiwa karibu dawa zote kanunue nje unaanza kuhangaika afadhali hataambao hawana bima wanakujazia tu huko unakuja kulipia kwenye Bill
Mimi Nina bima na sijawahi kuteseka kabisa! Hao wanaoteseka sijui wanateseka vipi!
 
Hayajakukuta.
Miwani, magongo, kuna dawa ambazo hazilipiw kwa bima.. ambulance nayo hailipiwi kwa bima inabidi ns ww uchangie ya mafuta.

Ni vizuri tukae kimya. Maana yasemwayo yapo
Au tembelea uo uzi uone shida iko wapi
 
Back
Top Bottom