KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Angetoka kwenye hospital ya mkoa rafiki yangu ungelipa gharama nafuu, kimara HC angeenda ngazi inayofuata hata kwa kuandikiwa tuuu tena huko ipo Hospital ya Kimkoa Ubungo, kuna ngazi za refferal rafk ndio maana wamekugonga hela ndefu. Ila mshukuru Mungu umepata watoto safi na Mungu aendelee kuwatunza na kuwapa afya njema na hekima ndani yake
Hospitali zingine sio za kwenda kabisa😂
 
Wakuu Kwema? Bila shaka muko salama.

Mwezi uliopita Nilikuwa Hospitali ya Taifa ya Mloganzila, Baada ya mke wangu Kuhamishiwa hapo baaada ya Kupewa Rufaa kutoka Kituo cha Afya ambapo alienda Kujifungua. Alienda Hospitali ya kawaida baade madaktari wakashauri awahimishwe Hospitali ya Taifa Mloganzila.

Kitu ambacho Nimeona Gharama za pale ni kubwa sana ni kama Hospitali za Watu Binafsi au Taasisi za Dini n.k

Wakati anapokelewa Pale Emergence nilitakiwa Kulipia Laki moja Fedha Taslimu ambayo wanaita ni ya Accomadation na haina maelezo mengine tena unapewa Control number ulipie ndio aanze Kuhudumiwa.

Baada ya Hapo alijifungua salama watoto wawili Mapacha alikaa siku ya Ijumaa hadi Jumatatu yaani Siku tatu Tu nikapewa Bill ya 1.35 yaani (Milioni moja laki tatu na elfu thelathini na tano) Nikasita kulipa nikaenda kwa wahasibu Kugombana nao Kidogo nikitaka Ufafanuzi japo Ilishindikana.

Baadae niliuliza Nikaambiwa Ghrama ya Kulala kwa Siku ni 50,000 lakini gharama ya Kujifungua ni 750,000. Niliambiwa Hiyo ssera ya mama wajawazito wanajifungua Bure haipo ni Siasa na Propaganda Tu.

Nilipambana nikalipia kiasi nikatoka.

Lakini kwa Kifupi Gharama Za Hospitali ya Mloganzila Ni kufuru kule ndani nilikuta akina mama waliojifungua wana Daiwa Wengine Millioni tatu, tano na kuendelea wameshikiliwa wake pale hadi fedha ipatikane.

Kwa kweli jambo hili linaumiza sana watanzania wa hali ya Chini ambao Kimsingi wanaamini Hospitali za Umma zinazoendeshwa naKupata Ruzuku kutoka serikalini ambayo ni kodi za wananchi gharama zake ziwe rafiki ili kila mwananchi aweze Kumudu ila imekuwa ni Tofauti.

Soma Pia:Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza

WIZARA YA Afya Aid Inatakiwa ilitazame hili na wawaweke wananchi wazi kwamba ile ni Hospitali ya Kulipia .

Ushahidi wa Nyaraka zote nianzo Mods musifute mukitaka ushahidi wa Receipt na Bill nitawapa
Mkuu, ulikuwa unajipinda tu kwa shemeji huku mnashangilia, ulitakiwa kujiandaa mapema, yaani unaona mavifaa ya kisasa yamejaaa humo yanang'weka mataa, unaware unachekelea tu
 
Sera ya Afya ya 2007 inaelekeza kuwa Matibabu ya Mama Mjamzito na Watoto chini ya Miaka 5 ni bure.

Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa anatambua kuwa zipo baadhi ya Hospitali za Umma zinazotoza wananchi fedha na kuzitaka kuacha mara moja huku Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakitakiwa kusimamia jambo hilo.

Dkt. Mollel hakusema kuwa hakuna Hospitali isiyotoza watu kwa ajili ya kupata huduma hiyo kama ilivyoandikwa hapo juu.
Hio sera ni kwa vituo vya afya😂 ila hospitali za kitaifa hazihusiki na sera hizo. Unapigwa kwenzi kama kawaida.
 
Mchawi pesa bima hupati uduma nzuri na rafiki lakin pia bima ni usumbufu baada ya kudeal na mgojwa unawaza kuzaja makaratasi na baadhi ya dawa watakwambia hazitolewi kwa bima

So pesa Muhimu
Huo ujinga ndio ulinifanya ni drop swala la Bima. Kimsingi Bima inatakiwa ku cover kila kitu tena upate huduma first class sababu wewe ni mteja wa Prepaid.

Ila bongo mtu wa bima unaonekana kama fala ambaye unatibiwa bure. Yani treatment ya watu wa Bima ni kama ya mbuzi na sio binadamu. Mtapangishwa foleni mistari hata mitatu na kauli za kejeli kadri wahudumu watakavyojiskia. Ila watu wa cash wao ni fasta na wanapapatikiwa 😂 kama raia wa kigeni. Bima its a No No kwangu mimi bora kutumia cash tu kwa tulipofikia.
 
Halafu Kile kibabu cha Muhimbili Janabi badala ya kufanya tafiti namna gani huduma zao ziwe za bei rafiki kwa wananchi yeye kila siku nikutaka kutrend na vitu vya hovyo hovyo...watu wa hivi enzi za u communist ilikua nikunyongaa tu.
Kibabu kinawaambia mnywe juisi ya tango na kipande cha samaki ili kuepusha ugonjwa wa moyo.
 
Mtoto wangu wa kwanza wa kike alijifungua nilitumia million 5, ilikuwa kama movie.

Hospital nilikupa 2 million private, mtoto alikuwa amekaa vibaya mno na pia kajifunga na umblical cord.

Madaktari waliangaika 4 hours kuweka sawa afya ya mama kabla hawajamfungulisha. Anesthesia alidai sijui presha imecanyaje akifanyi2a operation lazima mama aende

Nilitoka fasta baada ya kupewa akili, kumtafuta dokta bingwa gyno, naye alitaka 2.5 million ili atoke kwenye kazi yake. Analipwa kwa saa

Niliona bora nimpe tu hapo sijui kama mtoto ama mama atapona. Gyno na wenzake walifanya juhudi, operation ilikuja fanyika ndani kuna madaktari saba, gyno wawili, manesi na anesthesiologist, acha tu

Naambiwa mkeo kajifungua mtoto wa kike kwa kisu, nililia kama fala. Huwa silii na sijawahi lia hata msibani, siku anayokufa bibi kwanz usiku wake nilikul mzigo, yan kifup hata misib ikitokea nakula mzig. Inawezekana nina shida sehemu kwan hata majonzi haya yanaendelea nchin bado siku zote hizi nimekul mzigo, niombeen nina shida sehemu, thanks

Nisitoke nje ya mada, mtoto alizaliw, nilitumia gharama nyingine hapo kati. Sasa nina binti mtundu sana, mke wangu yuko salama mishono tu huwa inamuuma


Hii kulalamika ni kwa sababu hatuna hela. Gharama za kuzalisha tanzania ni nafuu compared to states. Serikaii ibireshe na indelee kupunguza jwa kulipia asilimia kubwa zaidi

Tutafute hela ndugu zangu, umaskini mbaya sana
Kwa kuwaa umesema ullienda private hospital ghalama kuwa kubwa sio jambo la ajabu hasa kama operation zinahusika. Lakini kufika 5M ni wewe ulitengeneza mazingira hayo ingewezekana kuishia 2.5M. Kwanza kwa nini uende hospital ikutoze 2M halafu bado Daktari utafute wewe umlipe 2.5M? Ilitakiwa huyo Daktari kama anahusika na hiyo hospital ulipompa hiyo 2.5M mengine yote amalize kwenye bajeti hiyo.

Tunaposema ghalama za kujifungua tunahusisha ghalama za kuzalisha, malazi na dawa. Ghalama huongezeka kulingana na complication za mimba . Operations nyingi zina ghalama hivyo haiwezi kuwa tofauti kwenye kujifungua. Mwanamke akijifungua kawaida ghalama huwa ndogo.

Changamoto inakuja umeandaa 400,000 kama akiba ya kujifungua kawaida unafika hospital unaambiwa hawezi kujifungua kawaida anatakiwa operation. Hapo tayari tunakuwa tunazungumzia 1M+.

Lakini pia kwa upande wa hospital za serikali mambo mengi yanahusika. Unamtoa mgonjwa kutoka hospital ya mkoa kama temeke na kwenda hospital ya Rufaa ya taifa. Hapa lazima ghalama zibadirike. Mpaka kufika Mhimbili unakuwa umeruka vituo vingi vya afya. Sasa hapa itategemea Rufaa ya kuhamisha imeandikwaje. Ukienda Mhimbili bila rufaa ya hospital za chini yake unapigwa ghalama kama za private hospital na hakuna wa kumlilia. Pia kuna chumba alicholala kinaongeza ghalama za kujifungua. Huwezi kuwa private room ghalama zikawa chini..

Jambo la msingi ni kuhesabu ghalama kabla ya maamuzi yoyote. Lakini pia ni vizuri kuandaa Daktari mapema ambaye atakuwa anamfanyia chekup mpaka wakati wa kujifungua kama uwezo unaruhusu ili kuepusha taarifa za kushtukiza
 
Huo ujinga ndio ulinifanya ni drop swala la Bima. Kimsingi Bima inatakiwa ku cover kila kitu tena upate huduma first class sababu wewe ni mteja wa Prepaid.

Ila bongo mtu wa bima unaonekana kama fala ambaye unatibiwa bure. Yani treatment ya watu wa Bima ni kama ya mbuzi na sio binadamu. Mtapangishwa foleni mistari hata mitatu na kauli za kejeli kadri wahudumu watakavyojiskia. Ila watu wa cash wao ni fasta na wanapapatikiwa 😂 kama raia wa kigeni. Bima its a No No kwangu mimi bora kutumia cash tu kwa tulipofikia.
Tumia Jubilee Insurance. Downside ni kuna mikoa haipo zaidi ya mjini so ni changamoto ila switch huko nenda hospital za hadhi na hiyo bima halafu lete mrejesho.

NHIF inasemekana ni wazito kulipa kwa wakati ndiyo sababu kuna kipindi baadhi ya hospital waliachana na NHIF kabisa.
 
Tumia Jubilee Insurance. Downside ni kuna mikoa haipo zaidi ya mjini so ni changamoto ila switch huko nenda hospital za hadhi na hiyo bima halafu lete mrejesho.

NHIF inasemekana ni wazito kulipa kwa wakati ndiyo sababu kuna kipindi baadhi ya hospital waliachana na NHIF kabisa.
Nitaifatilia hiyo Jubilee
 
Naona Kuna watu wanaendekeza upumbavu unaoitwa BIMA.
BIMA sio dawa ya gharama kubwa z hospital.zipunguzwe serikali iweke bajeti kubwa huko na si VINGINEVYO
 
Na mamaenu anachezea pesa kwenye mipira badala kuwwkeza kwenye afya tunashindwa makaburu walikuwa na roho mbaya ila kwa afya waliijali saana
 
Back
Top Bottom