KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
No alitolewa Kimara HC
Angetoka kwenye hospital ya mkoa rafiki yangu ungelipa gharama nafuu, kimara HC angeenda ngazi inayofuata hata kwa kuandikiwa tuuu tena huko ipo Hospital ya Kimkoa Ubungo, kuna ngazi za refferal rafk ndio maana wamekugonga hela ndefu. Ila mshukuru Mungu umepata watoto safi na Mungu aendelee kuwatunza na kuwapa afya njema na hekima ndani yake
 
Mjinga mmoja mwenye majivuno, unalinganisha uchumi wa TZ na state unamaana gani?
 
Wanaofanya maamuzi ya Rufaa sio mimi Mkuu. Mimi niliambiwa tu amehamishiwa Mloganzila mfuate huko
 
Muhimbili watu hujifungua kwa Tsh 200,000/

Ukute umeenda private afu unatupigia kelele hapa
Mkuu kwamba Mimi sina akili au sijui hata nilipoenda? ndio maana nimesema Docs zote ninazo za kuanzia Hospitali ya Chini, Rufaa hadi mloganzila. Receipt zote pia mimi sio mjinga mkuu.
 
Mh? Mbona wanawawe choka mbaya mitaani kutoka familia tiamajitiamaji naona wanajifungulia hospitali za serikali? Wanawezaje kumudu hizo gharama au kuna jinsi nyingine?

Kuna hospital za serikali, na kuna hospital zenye ubia wa aina Fulani na serikali, ukiingia hospital angalia facility ( Hasa malazi) Kama yana hadhi ya Guest ya 30,000 mfano, nothing will be cheap hata Kama ni ya serikali!
 
Niliambiwa Hiyo sera ya mama wajawazito wanajifungua Bure haipo ni Siasa na Propaganda Tu.
Lakini kwa Kifupi Gharama Za Hospitali ya Mloganzila Ni kufuru kule ndani nilikuta akina mama waliojifungua wana Daiwa Wengine Millioni tatu, tano na kuendelea wameshikiliwa wakae pale hadi fedha ipatikane.
Dah, hatari sana
Na hiyo ndiyo kazi wanayofanya ma CHAWA kudanganya wadau humu daily kuwa wanyonge wamefiikiwa, na blah blah nyingi...
Tlaatlaah Lucas Mwashambwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…