KERO Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Umenichekesha sana mbee...
 
Kama hii ni kweli hii taarifa kweli hii nchi imekuwa ya walafi na wakosa vipaumbele... Maswali ni haya
  • Je Gharama halisi (cost ni kiasi gani) ?
  • Je Kodi zetu zinakwenda wapi ?
  • Hata kama gharama ni kubwa na Kodi hazitoshi Je hizo pesa wanazofuja kwa kununua magoli na kufanya wanachofanya na safari zenye delegations za kumwaga zingesaidia wangapi ?
  • Kama wakunga majumbani wanaweza kufanya hii kazi cheaply basi na Muhimbili wajifunze kupunguza costs
 
maswali ni Mengi ila nikutoe wasiwasi hiyo ni kweli kabisa
 

Ulienda bila kufanya utafiti. Unapokuwa na mjamzito fanya utafiti wa gharama za kujifungua uende hospitali unayoimudu. Zipo hospitali bei chee kifupi wanatoa msaada. Nenda mfano hospitali ya mbweni misheni hao watu kweli wanafanya huduma sio biashara ya kujifungua.
 
Mkuu hili ni Tatizo pia la Kusoma kichwa cha habari na Kuhitimisha. Mimi nilimpeleka hospitali ya Chini ambayo ninajua gharama zake ninazimudu.

lakini baadae nikaambiwa nilipie Ambulance anapelekwa Mloganzila na Hapo mim nilikuwa nje napewa taarifa na mlinzi tu, baadae ikaja ambulance wakaondoka Mimi ningewazuia?

Mimi sina utaalam wa masuala ya afya Jukumu langu nililipia Ambulance nikapanda usafiri mwingine nikaenda Mloganzila
 
Harusi mnafanya za milioni ishirini. Kumleta kiumbe salama duniani mnataka msaidiwe na serikali.
samahan kwa kukukera tajiri, vipi hao wanaofanya hizo sherehe ndio wamelalamika? Kila mtu anaeleza kero yake Mkuu. ila kama unamjua aliyefanya harusi ya 20m amelalamika gharama hizo ni kubwa Please mtag hapa
 
Kweli mkuu, nilisoma ila nikaghafirika. Basi huo ushauri wangu uende kwa wale ambao wanatarajia kujifungua katika mazingira ya kawaida, pasipo dharura kama yako uliyoelezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…