Sikulaumu unahaki ya kulalamika,ni kweli umechoka, kila unachokiandika kweli yaonyesha moyo hauwezi tena
Ni ngumu sana moyo unapofika eneo hilo,yawezekana hujui umuhimu au utamu wa uhai wa mshua angali yu hai sasa
Nimeondokewa na baba yangu mzazi last year,huyu baba yangu hakua mtu wa kisport sport ni mkali mno pilipili ikasome
huwezi kaa nae ukaona jino lake akikuchekea he is very serious wakati wote,watoto wote rafiki yetu alikua mama ila sio baba.
Baba yetu alitupenda sana watoto wake (namaanisha hili mkuu) upendo wake kwetu watoto wake sio wa level ya kawaida, tulipokua shule ukirudi kumuomba hela ya Trip, anakupa sura kakaza ila atakupa Hata trip muwe mnaenda kwenye SAYARI i cost millions baba alikua anatoa.
Ktk kipindi chote cha uhai wa mzee sikumbuki lini niliwahi kaa nae tukawa tunacheka tunapga story na kutaniana,sijawahi wala sikumbuki.
Mkuu,Mshua amefariki Mungu kamchukua My dear Brother naliona PENGO la mzee, na miss kitu, am incomplete MAN by now, sipo sawa tena I miss him, You can ask me nam miss kwa lipi sasa? Ki ukweli uwepo wake,Pumzi yake,sauti yake, kumsikia watu wakimuongelea YES najiona nina BABA.
Sasa hivi simsikii tena,hayupo,naona picha zake tu Nalia kila ninapomkumbuka,natamani angekua mgonjwa kama alivyo baba yako niwe naenda mtazama pale kitandani,nim kiss,nimkumbatie Nimwambie NAKUPENDA BABA hata kama haongei ila najua atasikia.
Mkuu kuna ulemavu wa aina nyingi lakini ulemavu wakukosa mzazi sio ulemavu wa kawaida, Mpende tu baba mkuu Nakuhakikishia akiondoka leo hii, Utashinda ndani wiki au mwezi mzima huongei na mtu ulimi utapoteza taste za vyakula vyote vitamu dunia hii,utakua unatembea kama robot,itakuchukua muda kuwa sawa mkuu.
Usione kawaida unavyosema baba baba baba unapgiwa simu unaambiwa story za baba baba baba,brother unakuja Ukimya ambao hutosikia tena neno baba, utasikia wenzako wakilitamka,ukiona matangazo ya voda,au makampuni familia ikiwa na baba na watoto (uta mmiss sana mshua)
Bado sikulaumu mkuu,Unajua kwanini sikulaumu,Maishani mwangu nimechagua kukataa umaskini Napambana sana,nahangaika sana na haya maisha mkuu,hadi na leo hii ninapambana kwa level ambazo hamna kijana ataekuwa na mafanikio yangu akapambana kama ninavyoendelea mimi.
Unajua kwann mkuu,UMASKINI ni sababu ya yote haya,ungekua na PESA usingelalamika,haya yote n sababu haupo sawa kiuchumi,Mkuu mimi nimesema niwapendao hata kama itabidi wawekewe mioyo ya kutumia BETRI nitalipia hizo BETRI hata kama gharama ya kuchaji betri ikiwa ni millions Nitatoa hizo pesa.
Umaskini Ni laana,siupendi nauchukia,nimeona uzi wako Sijakuchukia wewe ila nimeuchukia UMASKINI sio mzuri mkuu the reason of all these is POVERTY, Nakataa umaskini napambana na nitaendelea kupambana milele.
Nimebaki na MAMA tu ila kama Mungu hatomchukua kwa hiari yake asee hakuna kitu itamchukua mama yangu,What is Money siwezi itwa YATIMA mimi,asee nitamlinda huyu niliebaki nae kwa gharama zozote zile,Mkuu sina la kusema juu yako nakuombea Mungu aguse Moyo wako utambue kuwa baba ni baba ana umuhimu wake mkubwa sana maishani mwako, Unaitwa nani shule? Jina lako la pili ni la huyo uliemchoka hapo mkuu.
He is a master siku 1 utaelewa hii risala yangu Mungu atakapomchukua mshua.