Gigy Money Waziri Katambi alitupa elfu 50 za kula. Aendelee kutuita tu kila wiki

Pesa yake matumizi yake ...hio 50 alaf Kuna ubaya gan kumpa mtu pesa ya mlo mmoja 😁
 
Huyo low IQ anapewaje platform? 50k ndio kitu cha kuweka public? Wtf
 
Ni sawa kabisa hiyo inasimamia usafiri na chakula uwezi kumuita mtu bila kumkalimu
 
Gigy Money, ameibua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka wazi kilichojiri katika mkutano uliofanyika hivi karibuni kati ya wasanii na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Katika video hiyo iliyosambaa kwa kasi, Gigy Money anaonekana akizungumza kwa uwazi bila kuficha kitu, akieleza na kufichua namna kikao hicho kilivyokuwa nyuma ya pazia.

Msanii huyo amedai kuwa kila mshiriki aliyehudhuria kikao hicho alipewa kiasi cha shilingi elfu 50,000 za Kitanzania mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Mheshimiwa Waziri.

Kauli hiyo imezua maoni tofauti miongoni mwa wafuatiliaji wa mambo kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wapo wanaompongeza kwa ujasiri wa kusema ukweli bila uoga, huku wengine wakikosora kitendo cha kuweka wazi mambo ya ndani ya kikao cha serikali. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani kujibu au kufafanua madai hayo.
Your browser is not able to display this video.
 
kwamba huyo waziri wa damu za watu mnataka aje akanushe kuwa hakuwapa hiyo 50,000 na kwamba akikanusha watanzania wenye akili wataamini? Ni mjinga pekee anayefikiri kuwa kile kilikuwa kikao cha maana, kama hamfahamu ile ilikuwa kiki kutest kama wanaweza kuhamisha mawazo ya watu ambao kwa sasa Kesi ya Lissu ndio inafatiliwa kuliko kitu chochote kwenye hii nchi. By the way kiki imebuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…