Goba - Mbezi kuwa zaidi ya Sinza, Tabata

Goba - Mbezi kuwa zaidi ya Sinza, Tabata

Kwa mara ya kwanza nakanyaga ardhi ya Tabata, mandela road ni vumbi tupu.

Mwaka 2001 nakanyaga tena kwa mara ya pili, lami imeishia Kimanga darajani, bima kwenda segerea bado vumbi.

Mara ya mwisho nakanyaga Tabata mwaka 2021, Kiumbe ana hotel, 40 40 imekufa, Wallet sio maarufu tena, wakina Papa Mangi hawepo, yule mshikaji wa Kajala hasikiki tena, Swiss club ilishavunjwa, Babylon imezeeka, Toroka uje kwishnye, Mfojo hana jina tena, KB inajikongoja, Barakuda inajivuta vuta, The Great anakimbizwa na akina Kitambaa cheupe, Bucket alifeli hata kuanza, Corner pale jeshini anajivuta vuta, wakina Highbury na Annex wanafanana, Last call maji kupwa n.k

Jamaa mmoja akisimulia kijiweni, niliookumbuka hii stori, nikasema basi inawezekana pia sehemu nyingine ikabamba, muda ndio mwamuzi!
Umesahau kuna small planet 😂😂
 
Nyie ndio huwa mnakariri aisee na hamtaki kutembea. Uliza wenzako wanaotembea watakwambia na sababu kwanini Sinza itaachwa nyuma na hata saizi imeanza kupoa sana kibiashara. Mbezi - Goba inamaeneo mengi ya kando ya barabara watu walinunua wakayareserve na sasa yanajengwa kwa standard nzuri ya kibiashara. Kwa mwaka mmoja tu huu imekua kwa kasi sana sasa kama wewe unabisha bisha tu utajikana baadae

Labda kidogo kwa Tabata, lakini Sinza iko poa na baada ya Dual Carriagway, imeongeza sana thamani.
Ama kuhusu Tabata, ni muunganiko wa kuanzia Reli ya Mwananchi, Aroma, Mawenzi, Kimanga, Kisukuru, Chang’ombe, Segerea hadi Kinyerezi. Kuanzia tu Bima hadi ufike Segerea na Kinyerezi, zipo centre nyingi za biashara na nyingi zimechangamka, kumbi kubwa za harusi, Super market, recreation centres kama ile ya Kinyerez Park, Bar kwa wale wanywaji zipo nyingi na kali. Kwa hiyo Tabata kwa kuwa ni eneo kubwa, lina vigezo vyote na wakaz wake siyo matajiri sana lakini wako na maisha ya wastani, kwa hiyo nakubaliana na mtoa mada, Tabata iko juu kwa medium residents wa DSM
 
Kiukweli huwa nashangaaga sana wanapoifananisha Tabata na Sinza.

Pazuri ni wapi? Sinza? Ni facade ya mbele tu barabarani ndiyo iko vizuri. Ila ukweli ni kwamba kuna mitaa mdau Kinyerez ina nyumba kali hadi utashangaa. Bado kwa makazi bora na ya kisasa, Tabata ni bora kuliko Sinza. Ila kwa Biashara za boutique, Sinza inaizidi kidogo Tabata. Kwa Ukubwa, Tabata ni kubwa sana. Itakumbukwa, Kinyerez imeanza kujitegemea na kuondolewa kuwa Segerea baada ya eneo la kiutawala kuwa kubwa sana
 
Hahaha

Mkuu umeuaaa

Swali sasa boss!inakuwaje watu wanajenga nyumba wanatumia mpk mln70, 100 etc
Lkn kujenga kimpangilio huko wanashindwa

Ova
Gharama ya kuchimba kupata eneo la kuweka nyumba na kufukia makorongo
 
Watu ni kweli wanajenga kwa kasi, ila mipango miji ni mibovu kwa kweli. Ingekuwa na mipango miji ya kueleweka ingekuwa poa sana. Sasa sijui ni kwa sababu ya miinuko mingi au kupangilia mitaa ni janga sugu?!
Kuna miji huko duniani imejengwa kwenye miinuko na inapendeza sisi waafrika tuna laana,sioni faida ya chuo kikuu cha Ardhi kwa nchi yetu
 
Ni Tabata ipi hiyo unayoisifia wewe hii tunayo ijua au ipo nyingine NewYork?
Sijaidifia, ila nimesema asifananishe. Goba ni nzuri. Goba haiwezi kua sinza wala tabata. Kimpangilio wa biashara. Kama unaelewa lkini. Punguza hisia uelewe.
 
Back
Top Bottom