Goba - Mbezi kuwa zaidi ya Sinza, Tabata

Goba - Mbezi kuwa zaidi ya Sinza, Tabata

What are you talking about? Vile vingi sio viwanja...ni mashamba. Mbweni na Bunju kumepimwa properly lakini sio Goba. Salasala pia kuna eneo limepimwa na kweli kuko njema kweli kweli

Kama pesa ipo wahi Goba.Mbona Kigamboni kumepimwa ila bei sii kama ya Goba?Kwa Tz sehemu kupimwa au kutokupimwa sii issue sana
 
Sinza haina tofauti na Magomeni, ishapitwa na wakati, Goba ni habari nyingine, inapendeza sana kutokana na vilima kuna sehemu karibu na Mbezi Juu kuna mandhari nzuri sana unaliona jiji na lote na city centre na bahari kwa pamoja,pia barabara kuu za kuingia na kutoka Goba zinapendeza sana
Hakuna mpangilio wa majengo wala mitaa, eneo likishakuwa na mpangilio hovyo hata liwe na nyumba kali kiasi gani, linabaki hovyo tu.
 
Mleta mada anazungumzia masuala ya biashara.
Ila kwa makazi mbweni na bunju beach ndo masaki mpya
 
Goba itafunika vibaya sana kutokana na madhari yake ya vilima....na hili limeshadhiri kutokana na kasi yake ya ujenzi wa nyumba nyingi za hadhi ya juu...
 
Goba itafunika vibaya sana kutokana na madhari yake ya vilima....na hili limeshadhiri kutokana na kasi yake ya ujenzi wa nyumba nyingi za hadhi ya juu...

Kitu ambacho wengi hatukubali ni kuwa wa Tz wanaangalia vitu vingi zaidi ya eneo "kupangwa".
 
Kuna eneo nasikia wametengewa na ruti mpya za magari ya abiria zitaanzishwa za kuanzia na kuishia hapo.

Nimesikia eneo linaitwa Saisai. Kwa habari nyepesi pia kuna ujenzi wa barabara kiwango cha lami kuunganisha Goba-Matosa-Kimara na Goba-Matosa-Temboni (Mbezi).
Kwenda Mbezi Luis, Mbezi Beach, na Kwenda Madale na Tegeta tayari kiwango cha lami.
Mkuu pande za mbezi itakua habari nyingine imagine hapo hujazungumzia barabara za makabe,msumi nazo zikiunganishwa.
 
Moja ya suluhu ya watu kuacha kujenga kiholela ni kuacha kukata viwanja vya high density baadala yake viwanja vyote katika nchi viwe Low density...Kuanzishwe vyeo vya mabwana ardhi wa kata ambao wanaripoti ardhi wilayani na kazi yao kuhakikisha ujenzi unafuata taratibu na ramani za mipango miji zinafuatwa..

Ushauri mzuri sana huu ili huko mbeleni kuepuka
Kuchafua miji. Leo sinza, magomeni, tabata, tandika, mwananyamala, mbagala, ni sawa na kipilipili cha nywele za mtu asie pitisha chanuo kichwani.

Inatia aibu sana pale upo kwenye ndege unatua DSM. hiyo DSM yenyewe sasa,[emoji23][emoji23][emoji23] ukianza kuangalia maeneo ya jirani ya Yombo, Kiwalani, Temeke, huko kote kote ni takataka.

Nyumba hazina mpangilio, ukanaribishwa Dar na nyumba zina mabati yenye kutu, yameshikiliwa na vipande vya mawe kwenye mapaa... zimekaa kulia kushoto juu chini , hakuna mpangilio and no green zone kabisaa. Ni aibu kwa city center kuwa ya ovyo
 
Eneo kama goba ingekua kwa wenzetu huko dunia ya kwanza pangekua pa kuvutia sana kwa jinsi ambavyo kungepangiliwa na ile mandhari yake ya vilima
Ila ss ni hapa bongo ukipita pale kuna mchanganyiko wa kila kitu 😃😃😃😃
 
Ushauri mzuri sana huu ili huko mbeleni kuepuka
Kuchafua miji. Leo sinza, magomeni, tabata, tandika, mwananyamala, mbagala, ni sawa na kipilipili cha nywele za mtu asie pitisha chanuo kichwani.

Inatia aibu sana pale upo kwenye ndege unatua DSM. hiyo DSM yenyewe sasa,[emoji23][emoji23][emoji23] ukianza kuangalia maeneo ya jirani ya Yombo, Kiwalani, Temeke, huko kote kote ni takataka.

Nyumba hazina mpangilio, ukanaribishwa Dar na nyumba zina mabati yenye kutu, yameshikiliwa na vipande vya mawe kwenye mapaa... zimekaa kulia kushoto juu chini , hakuna mpangilio and no green zone kabisaa. Ni aibu kwa city center kuwa ya ovyo
Mkuu mbona kama unafoka hivi[emoji3]
 
Eneo kama goba ingekua kwa wenzetu huko dunia ya kwanza pangekua pa kuvutia sana kwa jinsi ambavyo kungepangiliwa na ile mandhari yake ya vilima
Ila ss ni hapa bongo ukipita pale kuna mchanganyiko wa kila kitu [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Nenda Mwanza uone kule milimani vijumba vilivyo utadhani uko milima ya Galilaya

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Si kweli ,Sehemu yeyote ambayo haijapimwa at the end inakuja kuwa slum tu....Goba ni skwata hakutakuja kuwa kama sinza...sinza imepimwa.
 
Tabata itabaki juu
Kwa mara ya kwanza nakanyaga ardhi ya Tabata, mandela road ni vumbi tupu.

Mwaka 2001 nakanyaga tena kwa mara ya pili, lami imeishia Kimanga darajani, bima kwenda segerea bado vumbi.

Mara ya mwisho nakanyaga Tabata mwaka 2021, Kiumbe ana hotel, 40 40 imekufa, Wallet sio maarufu tena, wakina Papa Mangi hawepo, yule mshikaji wa Kajala hasikiki tena, Swiss club ilishavunjwa, Babylon imezeeka, Toroka uje kwishnye, Mfojo hana jina tena, KB inajikongoja, Barakuda inajivuta vuta, The Great anakimbizwa na akina Kitambaa cheupe, Bucket alifeli hata kuanza, Corner pale jeshini anajivuta vuta, wakina Highbury na Annex wanafanana, Last call maji kupwa n.k

Jamaa mmoja akisimulia kijiweni, niliookumbuka hii stori, nikasema basi inawezekana pia sehemu nyingine ikabamba, muda ndio mwamuzi!
 
Back
Top Bottom