Godbles Lema: Wafanyakazi wengi wa Serikali ni jobless, baadhi wanafanya uovu ili walishe familia

Godbles Lema: Wafanyakazi wengi wa Serikali ni jobless, baadhi wanafanya uovu ili walishe familia

Leo kwenye maria space iliyokuwa na mada ya mfumuko wa Bei man of the space was Lema. Ameongea mambo mazito na muhimu Kwa Taifa Leo.

Moja ya jambo kubwa ninalotaka kushare nawewe ni hili:

1. Tanzania haitaendelea kama hakuna miundombinu ya kisera yakutufanya tuendelee.

2. Wafanyakazi wa serikali ni jobless, wengi kipato Chao Kwa mwaka ni chini ya milioni 8, wanafanya kazi Lakini ni Jobless. Kipate cha mfanyakazi kwa mwaka ni mtaji wa machinga wengi waliopo masoko makubwa nchini.

Endeleeni kuwahita wenzenu jobless mkasau ninyi pia ni jobles
Ni kweli tupu vipato ni vidogo sn
 
Kisa yeye analishwa na mabeberu ndo anajiona siyo jobless, atuambie anafanya kazi gani huko ughaibuni huyu baba wa nyumbani.

Huko aliko ana maisha mazuri kuliko aliyokuwa nayo akiwa mbunge hapa. Watoto wake wote wanasoma shule nzuri kuliko zinazoitwa za international hapa nchini.

Na uwezekano wa watoto wake kupata ajira nzuri hapa nchini wakirejea kutokana na elimu nzuri ya huko ni mkubwa sana. Ww utabaki kushinda kwa waganga na kusifia viongozi wenye uwezo duni, huku watoto wako wakipata elimu ya bora liende.
 
Anaosha masufuria kwenye restaurant. Kumbuka kisomo hana, ufundi hana, kingereza hana, kifaransa hana. Sasa unategemea atafanya kazi gani zaidi ya kuosha masufuria. Huko aliko anajutia, kwa nini alijidanganya kwenda huko huku akijua alichopoteza ni kiti cha ubunge tu. Angekuwa huku anapiga pesa ya biashara zake. Alidanganyika na Lissu ambaye hata umachinga hauwezi, sasa analia kilio cha mbwa koko.

Hata kuosha masufuria ni kazi, au unadhani huko masufuria yanaoshwa kwenye mabeseni ya kuogea kama hapa Mwananyamala. Watoto wake wakirudi hapa watakuwa waalimu wa kiingereza wa profesa Ndalichako.
 
Huko aliko ana maisha mazuri kuliko aliyokuwa nayo akiwa mbunge hapa. Watoto wake wote wanasoma shule nzuri kuliko zinazoitwa za international hapa nchini. Na uwezekano wa watoto wake kupata ajira nzuri hapa nchini wakirejea kutokana na elimu nzuri ya huko ni mkubwa sana. Ww utabaki kushinda kwa waganga na kusifia viongozi wenye uwezo duni, huku watoto wako wakipata elimu ya bora liende.
Mfuate huko
 
wafanyakazi wa serikali halafu ni jobless hebu nielewesheni jamni
 
Leo kwenye Maria Space iliyokuwa na mada ya mfumuko wa Bei man of the space was Lema. Ameongea mambo mazito na muhimu Kwa Taifa Leo.

Moja ya jambo kubwa ninalotaka kushare na wewe ni hili:

1. Tanzania haitaendelea kama hakuna miundombinu ya kisera yakutufanya tuendelee.

2. Wafanyakazi wa serikali ni jobless, wengi kipato chao kwa mwaka ni chini ya milioni 8, wanafanya kazi Lakini ni Jobless. Kipate cha mfanyakazi kwa mwaka ni mtaji wa machinga wengi waliopo masoko makubwa nchini.

Endeleeni kuwahita wenzenu jobless mkasau ninyi pia ni jobles

"Wafanyakazi wa serikali Ni Jobless" ingawa English Ni ngumu Jaman hata hii Mie sielewi naomba mnisaidie Ndugu zangu
 
Leo kwenye Maria Space iliyokuwa na mada ya mfumuko wa Bei man of the space was Lema. Ameongea mambo mazito na muhimu Kwa Taifa Leo.

Moja ya jambo kubwa ninalotaka kushare na wewe ni hili:

1. Tanzania haitaendelea kama hakuna miundombinu ya kisera yakutufanya tuendelee.

2. Wafanyakazi wa serikali ni jobless, wengi kipato chao kwa mwaka ni chini ya milioni 8, wanafanya kazi Lakini ni Jobless. Kipate cha mfanyakazi kwa mwaka ni mtaji wa machinga wengi waliopo masoko makubwa nchini.

Endeleeni kuwahita wenzenu jobless mkasau ninyi pia ni jobles
Hii inaweza kuwa sawa kabisa, kwani MTU mwenye take home ya million kwa mwezi inamaanisha kwa mwaka ni 12million, Ambayo ndio Majority
 
Serikali inapaswa kumfanya kila mtanzania kuwa productive, aliye na ajira na asiye na ajira...

Walioajiriwa na Serikali wanapaswa kuwa busy masaa yote ya kazi na kuzarisha kadili target inavyotaka na malipo yawe kulingana na kiwangi cha uwezo wa kila mtu....

Serikali ifute vyeo vingi vya kisiasa na baadala yake watu wengi wawe kwenye uzarishaji mali, polisi wa usalama barabarani wapunguzwe maana wako wengi mno na baadala yake teknolonia itumike sana na polisi wa usalama wawe wachache..

JWTZ iajiri vijana wengi wapate mafunzo ya uaskari na wabaki makambini wakifanya shughuli za ujasiriamali..huku wakiwa askari pia..

Walimu walipwe mishahara mikubwa na posho nzuri na tuanze kuajiri walimu waliotoka vyuo vikuu kuanzia msingi mpaka sekondari...ualimu wa waliomaliza form four ukome....wote wawe ni wahitimu wa degree na mishahara iwe minono plus posho..

Jeshi la Polisi lianze kuajiri wahitimu wa vyuo vikuu na form six au college leavers na mitaala pale CCP ibadirishwe kuaendana na nyakati...

JKT iwe kitengo chini ya JWTZ na lasaba waajiriwe huko wakipata mafunzo ya kijeshi under JWTZ commanding na hawa watumike kama polisi in speacial operation na wawe under JWTZ controlling...
 
Kaongea ukweli mchungu sasa mwalimu wa sekondari au shule ya msingi hawezi kusave hata laki tatu kila mwezi na yuko kazini, matumaini yote anahamishia kujifariji kwenye job security na pension ambayo kwa miaka yote ya kazi kama 30 hatolipwa zaidi ya dola 50000 , akistaafu anakufa mapema maana elimu ya mtaani hana, nawapongeza wafanyakazi wenye mafanikio hasa waliojiongeza kwenye kilimo na biashara na uwekezaji mwingine zaidi.
Hakika! Unafanya kazi ukipata kitu cha kufanya hata cha million moja tu! Lazima uende kukopa! Bila kuwaza nje ya box hakika lazima ubaki mtu duni kwenye njaa kali!
 
Hii inaweza kuwa sawa kabisa, kwani MTU mwenye take home ya million kwa mwezi inamaanisha kwa mwaka ni 12million, Ambayo ndio Majority
Kaka hao wenye take home ya 1 million kwa bongo wala sio wengi! Hata akiwa na hiyo anakuwa amechukua mikopo uchwara ya miaka saba anachukua laki nne tu kwa mwezi hela yote kwenye mkopo! Halafu hapo hapo hana hata biashara yeyote! Huyu mtu lazima awe jambazi pale kazini kwake anakwapua kila hela inayopita kwenye mikono yake! Na hapo ndo mwanzo wa miradi mibovu ya serkali!
 
Leo kwenye Maria Space iliyokuwa na mada ya mfumuko wa Bei man of the space was Lema. Ameongea mambo mazito na muhimu Kwa Taifa Leo.

Moja ya jambo kubwa ninalotaka kushare na wewe ni hili:

1. Tanzania haitaendelea kama hakuna miundombinu ya kisera yakutufanya tuendelee.

2. Wafanyakazi wa serikali ni jobless, wengi kipato chao kwa mwaka ni chini ya milioni 8, wanafanya kazi Lakini ni Jobless. Kipate cha mfanyakazi kwa mwaka ni mtaji wa machinga wengi waliopo masoko makubwa nchini.

Endeleeni kuwahita wenzenu jobless mkasau ninyi pia ni jobles
Hivi hata kama humpendi Lema huoni point yake? Mtumishi anapokea 320000 Kwa mwezi, analipa deni la mahtaji ya ndani 140000, anabakiza 180000 ambayo haimtoshi na familia yake. Mwezi unaofuata mwendo ni uleule kopa lipa kopa lipa, lipa kopa. Jobless wanaishije kama siyo Kwa style hii hii?
 
Back
Top Bottom