Godbless Lema akamatwa Kajiado akitorokea Kenya yeye na familia yake. Kurudishwa nchini kesho Novemba 9, 2020

Nchi imefika mahali ambapo wengine hawana haki na nchi yao, wamegeuzwa wakimbizi ndani ya nchi yao. kwa mara ya kwanza ndani ya Tanzania raia wanapigwa risasi kama nguruwe wezi wa mihogo wakati vitendo Kama hivi tulikuwa tunavisikia kwa majirani zetu.
 
Ina maana anapaswa kukubaliana na mawazo yao? Wasipingwe kwa chochote?
Hapana. Anachotakiwa tu kufanya ni kutumia ulimi wake vizuri, maana kuna maisha baada ya kampeni na uchaguzi. Ninyi huwa mnamjaza upepo weee kisha mnachoropoka mnamwacha kwenye mataa.
 
Mtoto alie ila mbwa mwitu

Ndio madhara ya kupenda kutengeneza matukio inakuwa ngumu sana kuaminika.
 
Pumbavu sana.Lissu apewe ulinzi Kamara nani ? Aliopewa wakati wa kampeni akatukana wee mpkaa akachoka mwenyewe. Sasa akitaka ulinzi aende mwenyewe Ultimate security kuna walinzi kibao atapewa.
 
😭😭😭 jamaa kawa mkimbizi kwenye nchi yake
 
Lazima tumwogope kwa sababu ajenda yake kuu ni kuzua fujo na machafuko; hataki kuona Tanzania ikifanikiwa na kusonga mbele.
 
Hapana. Anachotakiwa tu kufanya ni kutumia ulimi wake vizuri, maana kuna maisha baada ya kampeni na uchaguzi. Ninyi huwa mnamjaza upepo weee kisha mnachoropoka mnamwacha kwenye mataa.
Hawezi kutumia ulimi wake vizuri kama wengine hawatumii ya kwao vizuri, Kuna watu wana jazba hata ukiwajibu vizuri wao wanakubwatukia tu.
Yaani mtu ana gubu utafikiri nini sijui...analazimisha ukubaliane na mawazo yake,kila lisemwalo uamini bila kuhoji.
 
Stunt

Lema hakuuawa alipokuwa mbunge leo sio mbunge kabakiwa na suruali nani anataka kumuua?

Lema ni threat kwa nani??

Kama personal issue alikabili tu
Ben Saanane alipotezwa mpaka leo kwa kuhoji tu degree ya mfalme. Hivi alikuwa kweli alikuwa threat? Kwa dikteta hata usipompigia tu makofi wakati wengine wote wanampigia, unaweza kupotezwa.

Nondo mla watu, siyo lazima utishie kwa lolote, unaweza kupotezwa hata kwa kufikiriwa tu kuwa siku moja utakuwa tishio.
 
Hakuna ajuae sababu hata dereva aliyekua nae ambaye alikua shahidi mzuri amefichwa Ubelgiji. Inafikirisha sana hii
Kwa hiyo dereva ndiyo kazuia kukamatwa kwa waliomshambulia?
 
Lema hana tishio lolote,na kama kuuwawa sio kipindi hiki, hata hao wauwaji wana akili.
 
Kwa hiyo dereva ndiyo kazuia kukamatwa kwa waliomshambulia?
Unamkamaje aliyemshambulia bila kupata maelezo ya shuhuda muhimu namna hiyo? Mbona vitu vingine vipo wazi vinaeleweka?
 
Binafsi nisichangie chochote kumhusu.

Ila tu. kama nchi yangu Tanzania ip katika hii hali wanasiasa wanayotaka kutuaminisha, tusingeshindwa kuingia mtaani na kuwaunga mkono.

Mbona hapa kitaa barida tu.
Toa maoni yako publicly halafu yule jamaa akusikie
 
Sijaona kaka, sijui mtaani kwenu.

Mtaani kwetu mtu haonewi aseeh, tungeshaliamsha.
Acha tuu mkuu, tuipende nchi yetu, maana ni muhimu kuliko chochote.

Ila kilichofanyika siyo poa, dunia inajua nawewe unajua
 
Acha tuu mkuu, tuipende nchi yetu, maana ni muhimu kuliko chochote.

Ila kilichofanyika siyo poa, dunia inajua nawewe unajua
Inawezekana kuna yaliyofanyika sio poa, ila kuleta drama kama hizi kusababisha taharuki sio poa zaidi.
 
Yep. Uko sahihi kabisa. Meaning: NATAKA!!! NATAKA!!! Nchi ambayo haina machafuko yasababishwayo na vipanga wenye tamaa ya madaraka, posho & ruzuku plus makuwadi wa mabepari.
 
Tulikuonya tangu mapema kwamba Shetani hana rafiki , bado wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…