Uchaguzi 2020 Godbless Lema: Arusha leo kuna Mechi ya Simba bure na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu Mkutano wa Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Godbless Lema: Arusha leo kuna Mechi ya Simba bure na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu Mkutano wa Tundu Lissu

Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini Ndg. Godbless Lema amelalamika kuwa CCM inawahujumu kwa kuandaa mechi ya Simba bila kiingilio na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu mkutano wa mgombea urais wa CHADEMA Ndg. Tundu Lissu.

Hata hivyo Lema ameapa kuwa leo ndio CCM watajua kwamba CHADEMA ni baba lao Arusha.

Lema amesema haya katika ukurasa wake wa Twitter.

My take: Kwani sehemu anayoenda Lissu ni lazima shughuli zisimame?

Maendeleo hayana vyama!
Kwani watu wanashikiwa gobole lazima waende kwenye mechi?
 
Msianze kutapatapa na huyo Lissu wenu kwa kutafuta Huruma kwenye vilabu vyetu.

Kwani hata Kama wameweka kiingilio bure si nikwaajili ya Mashabiki wao wa Arusha, Wanahusiana na je na mikutano yenu?

Kwani kwenda kutazama hiyo mechi ilikuwa shurti au Sheria?

Kwani si Kila mtu anapenda na kwenda anakovutiwa?
Ukiona watu wamejaa kwenye mechi ya Simba Basi jua simba inavutia Sana kuliko chadema.

Mwisho; Nikosa kubwa Mtu kama lissu kumufananisha na Mungu kiasi kwamba watu walaaniwe kwasababu yake wakati mtu mwenyewe kajaa laana ya usaliti.

Ushauri: toa huu Uzi hapa upeleke kwenye jukwaa la siasa Maana hapa naona unajaribu kuchanganya maji na mafuta tu.
 
Jamani Arusha si ngome ya chadema huwa mnasema?

Sasa inawezekanaje waache rais wao waende kwenye michezo?

Hawa chadema waache visingizio! Ni kwamba wananchi wamewapuuza
Waulize kawe palikua na mechi gani?
 
Hali ya CCM ni mbaya kweli kweli,muda huu wapo kikaoni wanamlaumu DC kaboringa sana.Mwenyekiti wa CCM Mkoa RPC Mstaafu Zelot anataka wajumbe wa kamati ya Wilaya ya kutafuta mbinu mbadala mapema ndani ya week 2 kabla jahazi halijazama kabisa.
Hapo lazima wachemshe tu hawana plan b ya kuisimamisha cdm mkoani Arusha.

Tulisha kula kiapo kuwa ccm ni adui yetu
 
Kama kuna taarifa za ndani kuhusu hujuma hapo sawa.Ila kama ni kujisemea sababu kumekuwa na mechi huo ni ujinga. Shughuli lazima ziendelee na Simba wapo kazini AFC wapo kazini wanatafuta posho za wachezaji. Jana ACT imezindua kampeni na ilikuwa Yanga Day.
Sasa hapa mnaburudisha viti?
Screenshot_20200831-175942.jpg
 
Wakuu Salamu toka Arusha na vitongoji vyake.

Uwanja wa Shekh Amri Abeid na tamasha uwanja wa Kilombero hakuna watu ni aibu tupu kama si fedhehea.

Wana Arusha wapo uwanja wa Relini wamejaa tele hakuna nafasi ya kutema mate.Hakuna nafasi ya kujigeuza wala kujinasi ni nyomi ya kutosha na kusikitisha kwa wenye hila na hiyana.

Mkuu wa Wilaya njoo na style nyingine hii imebuma vibaya mno,tamasha tuwekee kesho leo tunasikiliza sera na miongozo ya Mh Lissu mmekata umeme lakini haisaidii asilani.
View attachment 1554438
Kwani una tatizo gani?mbona unamalizia stress kwa mabingwa wa nchi?
Mechi ya Simba ilikua Jana Leo Ni mazoezi
Simba hawana haha ya watu wanapima wachezaji wao kwa ajili ya ligi,ndio Mana wanacheza mechi mbili kwa siku bunju na uhuru bila ya mashabiki
 
Back
Top Bottom