Godbless Lema asimulia jinsi alivyokamatwa Jumapili na kuandikiwa kosa la kuandamana kwenye ndege

Kuna aliyesema kuwa mama ni mjinga, mshmaba, hajiamini, etc, etc, kama walivyokuwa wanamsema JPM wakati huo?
 
Kila mtu amejua Sasa Ni kiasi gani CCM inaogopa DEMOKRASIA, Ni kiasi gani CCM imedhihirisha inaiogopa chadema.
CCM without police is nothing.
Kulikua na umuhimu gani wa kutumia gharama kiasi kile?
Silaha tukizonunua kwa ajili ya kulinda raia leo zimetumika kuwatisha wale wale walipa Kodi waliozinunua kwa maslahi ya CCM.
 
Najiuliza huyo RUBANI wa ndeg hiyo na mhudumu wanaishi Tanzania kweli hawajui ni majizi TU hapa mzee Ali kibao alishishwa kwenye basi na akatekwa na kuuwa?
Mkuu, hebu tulizana basi.

Hizi lawama zote bila kuwa na taarifa kamili zinamsaidia nani hasa, kama siyo hao hao wanao tenda maovu!

Unazo taarifa zote kuhusu polisi walivyo fanya kwenye hiyo ndege? Unao uhakika watu wote walio shuhudia tukio hilo, ikiwa pamoja na hao rubani na wahudumu walicho fanya katika muda wote wa tukio na hata baada ya tukio?

Wewe ulitaka wafanye nini, wazuie kwa nguvu hao waliokuja na silaha ndani ya ndege. Ulitaka hawa watu wapeleke wapi taarifa za Lema kutekwa/kukamatwa? Unao uhakika hawakutoa taarifa popote?
 
Shetani magu hawezi kutakata kwa uhayawani ule aliokuwa anafanya.
Inashangaza kwelikweli kwa baadhi ya watu kutaka kuonyesha kwamba magufuli ya aina hii tunayo shuhudia sasa yeye hayakumhusu.

Mimi nazidi kumshukuru tu Mungu kwa kuepusha janga lililokuwa litokee wakati wa UKUTA. Mungu alimwongoza vema Mbowe siku hiyo. Na pengine wakati huu tungekuwa na hali tofauti zaidi ya hii iliyopo sasa
 
Umesema ukweli mtupu.
Haya ndiyo wanayotakiwa kuyafahamu vizuri CHADEMA ili waweze kutimiza malengo yao vizuri bila kujali uwepo wa polisi wanaotumiwa na CCM. Mikakati inatakiwa ielekezwe huku.
 
Huu ni ule wakati ambapo ccm wanakuwa karibu sana na vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Mimi sioni kwa nini hili liwe swali la kuhangaisha watu kujibu.
Kiongozi yeyote mkuu anayekuwa katika nafasi hiyo ya uraisi hawezi kuepuka lawama mambo kama haya yanapo tokea.
Na mbaya zaidi inakuwa kiongozi huyo anapo onekana kuhusika na mambo hayo moja kwa moja; kama alivyo kuwa Magufuli, na sasa alivyo Samia.
Samia kajitoa moja kwa moja na kujionyesha kuhusika kwake kwa kushindwa hata kuyasemea tu watu wayaelewe.
Samia ameshiriki moja kwa moja, kwa kuteua watu maalum aliotaka wakatekeleze aliyokuwa akitaka yatekelezwe.
Samia ameweka hadi sheria kamili ya kupotezea watu, na kukiweka kitengo husika chini ya uongozi wake moja kwa moja.
Mtu atasemaje kwamba Samia haya yote yanayo tkea anasingiziwa; kwamba hayajui?
 
Si tulikubaliana ni siku ya maandamano, kwenye ndege alikuwa anatoroka au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…