Siwaelewi watanzania wenzangu
- Wakati wa wakoloni walisema bora utawala wa Machifu
- Wakati wa Mwl. J. K. Nyerere wakasema bora ukoloni
- Wakati wa Mzee Mwinyi walisema bora Mwl. J. K. Nyerere
- Wakati wa Mzee Mkapa walimsifu sana Mzee Mwinyi
- Wakati wa Kikwete walimsifu sana Mzee Mkapa
- Wakati wa Magufuli walimponda na kumkumbuka Kikwete
- Kaja Samia sasa wanamkumbuka Magufuli
KUna siku niliona baiskeli ya mkodishaji mmoja imeandikwa "...kila asubuhi mpya heri ya jana, siku kdhaa baadaye nikaona nyingine ya mkodishaji huyohuyo imeandikwa "...every new morning is better than yesterday" nilihisi alilenga kutafsiri ile statement ya kiswahili iliyopo kwenye baiskeli nyingine