Hivi rais gani atakuja kukubalika na Watanzania akiwa madarakani na baada ya kuondoka madarakani tangu turudi kwenye mfumo wa vyama vingi?
Magufuli alipoingia madarakani, watu wakaanza kumkumbuka Kikwete, leo Samia ameingia madarakani, Magufuli anaanza kukumbukwa!!
Itakuwa Tanzania tunahitaji katiba mpya kwakweli, ili kiongozi aliyepo madarakani aifuate hiyo katiba, ili asichukiwe na raia kwa sababu anakuwa anaongoza kwa kufuata katiba iliyotengenezwa na wananchi.
Kwa sasa kila rais anaongoza kwa utashi wake akiingia madarakani, hali inayopelekea huyu anakumbukwa, yule anachukiwa!
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app