Godbless Lema: Makamu wa Rais ni Rais mtarajiwa, CCM amueni kwa busara

Godbless Lema: Makamu wa Rais ni Rais mtarajiwa, CCM amueni kwa busara

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Nimetafakari sana baada ya tukio la Rais kufia madarakani. Nafasi ya Makamu wa Rais ni lazima ijazwe kwa HEKIMA/BUSARA/ UWEZO na sio UDINI, UKANDA, UKABILA. Katiba yetu imeweka mtego mbaya sana kwamba Rais akifa anayekuwa Rais ni Makamu wa Rais mara moja.

Kama UKANDA/UKABILA/UDINI utaamua VP na sio uwezo basi kuna siku tunaweza kujikuta tuna Rais kama RC Mbeya. Ni muhimu pia kuheshimu UWEZO, hapa simaanishi elimu tu. Prof Kabudi ni zao la utafiti mzuri kuwa elimu bila akili ni sawa na choo bila mlango. CCM amueni kwa ajili ya Nchi.

Godbless Lema.
 
Wachawi mmeanza sasa
Ccm Ina taratibu zake, haiwezi kupokea maelekezo toka kwa makada wa chadema
Miezi michache nyuma, Kabudi alikuwa anatukanwa na kukejeliwa
Mwenyekiti Magufuli Mungu amrehemu, alishatoa muelekeo wa chama namna ya kutoa viongozi baada ya uchaguzi wa 2020, mtu Kama kabudi, Lukuvi wanatupwa nje dimba sababu tu ya umri wao
 
Nimetafakari sana baada ya tukio la Rais kufia madarakani. Nafasi ya Makamu wa Rais ni lazima ijazwe kwa HEKIMA/BUSARA/ UWEZO na sio UDINI,UKANDA,UKABILA. Katiba yetu imeweka mtego mbaya sana kwamba Rais akifa anayekuwa Rais ni Makamu wa Rais mara moja.

Kama UKANDA/UKABILA/UDINI utaamua VP na sio uwezo basi kuna siku tunaweza kujikuta tuna Rais kama RC Mbeya. Ni muhimu kuheshimu UWEZO, hapa simaanishi elimu tu. Prof Kabudi ni zao la utafiti mzuri kuwa elimu bila akili ni sawa na choo bila mlango. CCM amueni kwa ajili ya Nchi.

Godbless Lema.
Elimu bila akili ni sawa na choo bila mlango by Godbless Lema

Nimecheka sana!
 
Back
Top Bottom