Godbless Lema: Mtoto wa Simbachawene asikomolewe kwa sababu ya matakwa ya Baba yake

Godbless Lema: Mtoto wa Simbachawene asikomolewe kwa sababu ya matakwa ya Baba yake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mh Godbless Lema ambaye anatajwa pia kama miongoni mwa Manabii wa Mungu walioletwa Tanzania kwa makusudi Maalum , Amenukuliwa huko Twitter akipinga POLISI KUFANYA KAZI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE .

Mh Lema anadai mpaka sasa mtoto wa Simbachawene aliyedaiwa kudharau vyombo vya dola angali anashikiliwa Selo , jambo ambalo Lema analitafsiri kama ni uvunjifu wa KATIBA YA NCHI NA SHERIA ZILIZOPO , amesikitishwa sana kwa Jeshi la Polisi kuifanyia kazi kauli ya Simbachawene badala ya PGO , Pamoja na Sirro kung'olewa lakini bado shida ziko palepale .

Ni kweli kwamba mtoto wa Simbachawene amekosea lakini Haki zake zinapaswa kulindwa , Kosa alilotenda lina dhamana , lakini hadi sasa bado yuko rumande kwa vile tu Polisi wanamsikiliza Simbachawene , Mtoto akishazaliwa ni Mali ya Nchi , Ndio maana huwezi kuua mwanao tukakuacha , ni lazima tukukamate .

Binafsi nampongeza Lema kwa jambo hili na kiukweli MTOTO WA SIMBACHAWENE ASHUGHULIKIWE KWA MUJIBU WA SHERIA NA SI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE , tukiruhusu jambo hili tutakuwa Wajinga sana , Maana siku Simbachawene akisema mwachieni basi tutamuachia bila hata kufuata Taratibu .
 
Mh Lema anadai mpaka sasa mtoto wa Simbachawene aliyedaiwa kudharau vyombo vya dola angali anashikiliwa Selo , jambo ambalo Lema analitafsiri kama ni uvunjifu wa KATIBA YA NCHI NA SHERIA ZILIZOPO , amesikitishwa sana kwa Jeshi la Polisi kuifanyia kazi kauli ya Simbachawene badala ya PGO , Pamoja na Sirro kung'olewa lakini bado shida ziko palepale .
Pointi kubwa sana hii.

Ina maama Baba yake asingesema asingefanywa kitu.
 
Yaani mi naona hata Simbachawene alikosea kutoa kauli ya namna ile. Je angekuwa mtoto wa mtu masikini asiyekuwa kiongozi polisi wangesubiri amri ya baba yake aliyepo kijiji cha simba dume atoe press kuwa mwanae ashughulikiwe? Pia je kama dogo alikuwa na ugomvi binafsi na hao polisi then unasema eti mwanao ashughulikiwe? Yaani hapo mi naona huyo baba hakutumia hekima
 
Hivi karibuni Simbachawene alitumia madaraka yake kuwaamuru polisi wamshughulikie mwanae bila huruma! Nao polisi baada ya kupewa agizo wamesema watamfikisha mahakamani. Inawezekana alitenda kosa lakini kitendo cha baba yake kuingilia na kumkana tayari kumewapa nguvu ya ziada polisi jambo ambalo si sahihi. Huyo kijana hana wa kusikiliza hoja zake ziwe sahihi au si sahihi kwani amezingirwa na kundi kubwa la dola ambalo linaweza likajipa haki ya ushahidi wa uongo kutokana na maelekezo toka kwa baba yake, hii ni hatari kwa maisha ya furaha ya kijana.
Ombi langu kwa wanasheria wapenda haki wamtetee kijana ili sheria ifuatwe kwa njia zinazokubalika na si kwa maagizo ya baba.
Mkuu umehesabika tayari au unaandaaa nyuzi tu zinazotia kinyaa hapa jamiiforum
 
Back
Top Bottom