Godbless Lema: Mtoto wa Simbachawene asikomolewe kwa sababu ya matakwa ya Baba yake

Godbless Lema: Mtoto wa Simbachawene asikomolewe kwa sababu ya matakwa ya Baba yake

Hivi karibuni Simbachawene alitumia madaraka yake kuwaamuru polisi wamshughulikie mwanae bila huruma! Nao polisi baada ya kupewa agizo wamesema watamfikisha mahakamani. Inawezekana alitenda kosa lakini kitendo cha baba yake kuingilia na kumkana tayari kumewapa nguvu ya ziada polisi jambo ambalo si sahihi. Huyo kijana hana wa kusikiliza hoja zake ziwe sahihi au si sahihi kwani amezingirwa na kundi kubwa la dola ambalo linaweza likajipa haki ya ushahidi wa uongo kutokana na maelekezo toka kwa baba yake, hii ni hatari kwa maisha ya furaha ya kijana.
Ombi langu kwa wanasheria wapenda haki wamtetee kijana ili sheria ifuatwe kwa njia zinazokubalika na si kwa maagizo ya baba.
Hao wamevimbiwa tozo achana nao, mwanasiasa akikwambia twende kushoto wewe nenda kulia wote utawakuta huko.

Uchungu wa Mwana aujuwaye mzazi usidanganyike, yule mtoto ana mama yake na mama ana nguvu yake Kwa mume wake ulielewe hili, na ukute ndio mtoto kipenzi cha mama nyumbani hakukaliki huyo George Simbachawene atatukanwa kama mtoto Mdogo mpaka mtoto wa mama awe huru.
 
Hivi karibuni Simbachawene alitumia madaraka yake kuwaamuru polisi wamshughulikie mwanae bila huruma! Nao polisi baada ya kupewa agizo wamesema watamfikisha mahakamani.

Inawezekana alitenda kosa lakini kitendo cha baba yake kuingilia na kumkana tayari kumewapa nguvu ya ziada polisi jambo ambalo si sahihi.

Huyo kijana hana wa kusikiliza hoja zake ziwe sahihi au si sahihi kwani amezingirwa na kundi kubwa la dola ambalo linaweza likajipa haki ya ushahidi wa uongo kutokana na maelekezo toka kwa baba yake, hii ni hatari kwa maisha ya furaha ya kijana.

Ombi langu kwa wanasheria wapenda haki wamtetee kijana ili sheria ifuatwe kwa njia zinazokubalika na si kwa maagizo ya baba.

Kwani wakili wao msomi Robert Kidando ni dhidi ya haki tu?
 
akili ndogo kweli kweli wewe....hii movie ndio kwanza imeanza.
 
Hahaha eti mtoto akishazaliwa ni mali ya nchi, wakati yeye (Lema) kakimbizia kuanzia Watoto, Mke mpaka yeye mwenyewe Kanada, au yeye na watoto wake siyo mali ya nchi?
We ni kilaza namba moja afrika sema amen
 
asiyefunza na baba/mama yake hufunzwa na ulimwenguuu ...... huenda nyumbani ameshindikana
 
Mh Godbless Lema ambaye anatajwa pia kama miongoni mwa Manabii wa Mungu walioletwa Tanzania kwa makusudi Maalum , Amenukuliwa huko Twitter akipinga POLISI KUFANYA KAZI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE .

Mh Lema anadai mpaka sasa mtoto wa Simbachawene aliyedaiwa kudharau vyombo vya dola angali anashikiliwa Selo , jambo ambalo Lema analitafsiri kama ni uvunjifu wa KATIBA YA NCHI NA SHERIA ZILIZOPO , amesikitishwa sana kwa Jeshi la Polisi kuifanyia kazi kauli ya Simbachawene badala ya PGO , Pamoja na Sirro kung'olewa lakini bado shida ziko palepale .

Ni kweli kwamba mtoto wa Simbachawene amekosea lakini Haki zake zinapaswa kulindwa , Kosa alilotenda lina dhamana , lakini hadi sasa bado yuko rumande kwa vile tu Polisi wanamsikiliza Simbachawene , Mtoto akishazaliwa ni Mali ya Nchi , Ndio maana huwezi kuua mwanao tukakuacha , ni lazima tukukamate .

Binafsi nampongeza Lema kwa jambo hili na kiukweli MTOTO WA SIMBACHAWENE ASHUGHULIKIWE KWA MUJIBU WA SHERIA NA SI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE , tukiruhusu jambo hili tutakuwa Wajinga sana , Maana siku Simbachawene akisema mwachieni basi tutamuachia bila hata kufuata Taratibu .
Lema ni Nabii wa nani?
 
Mbona mzazi pia kasema sheria ichukue mkondo wake! Au mi sikuelewa
 
Ilikua lazima mheshimiwa aoneshe msimamo Kama ule mbele ya umma.
Vipi Kama angenyamaza?watu wangekuja namaneno kwamba mzee kabariki ndoman yupo kimya.
Vipi angeonekana kumtetea mwanae hadharani? Watu wangeibuka nahasira kwamba viongozi ndivyo walivyo kutetea watoto wao.
Nini kitafanyika Sasa? Simbachawene Kama kiongozi katoka hadharani kuwataka polisi wafate sheria... yupo sahihi.
Baada yahapo?, Simbachawene anabaki kuwa mzazi wa kijana.Taratibu zakumsaidia kijana Kama mwanae lazima zifanyike nahizi sio za hadharani tena
 
Back
Top Bottom