Godbless Lema: Mtoto wa Simbachawene asikomolewe kwa sababu ya matakwa ya Baba yake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mh Godbless Lema ambaye anatajwa pia kama miongoni mwa Manabii wa Mungu walioletwa Tanzania kwa makusudi Maalum , Amenukuliwa huko Twitter akipinga POLISI KUFANYA KAZI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE .

Mh Lema anadai mpaka sasa mtoto wa Simbachawene aliyedaiwa kudharau vyombo vya dola angali anashikiliwa Selo , jambo ambalo Lema analitafsiri kama ni uvunjifu wa KATIBA YA NCHI NA SHERIA ZILIZOPO , amesikitishwa sana kwa Jeshi la Polisi kuifanyia kazi kauli ya Simbachawene badala ya PGO , Pamoja na Sirro kung'olewa lakini bado shida ziko palepale .

Ni kweli kwamba mtoto wa Simbachawene amekosea lakini Haki zake zinapaswa kulindwa , Kosa alilotenda lina dhamana , lakini hadi sasa bado yuko rumande kwa vile tu Polisi wanamsikiliza Simbachawene , Mtoto akishazaliwa ni Mali ya Nchi , Ndio maana huwezi kuua mwanao tukakuacha , ni lazima tukukamate .

Binafsi nampongeza Lema kwa jambo hili na kiukweli MTOTO WA SIMBACHAWENE ASHUGHULIKIWE KWA MUJIBU WA SHERIA NA SI KWA MATAKWA YA SIMBACHAWENE , tukiruhusu jambo hili tutakuwa Wajinga sana , Maana siku Simbachawene akisema mwachieni basi tutamuachia bila hata kufuata Taratibu .
 
Pointi kubwa sana hii.

Ina maama Baba yake asingesema asingefanywa kitu.
 
Yaani mi naona hata Simbachawene alikosea kutoa kauli ya namna ile. Je angekuwa mtoto wa mtu masikini asiyekuwa kiongozi polisi wangesubiri amri ya baba yake aliyepo kijiji cha simba dume atoe press kuwa mwanae ashughulikiwe? Pia je kama dogo alikuwa na ugomvi binafsi na hao polisi then unasema eti mwanao ashughulikiwe? Yaani hapo mi naona huyo baba hakutumia hekima
 
Mkuu umehesabika tayari au unaandaaa nyuzi tu zinazotia kinyaa hapa jamiiforum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…