Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kumbe alisharudi bongo!
Hata hivyo kuna kitu nyuma ya maombi haya ! Ngojea tuone.
 
Haya yote mnayajua baada ya Lisu kutaka Uenyekiti?

Mlimpa Umakamu akiwa wapi?

Ni hasara sana kwa wazazi waliowazaa na kuwasomesheni.
Kwaajili ya propaganda za wakina lisu na mbowe ndio iwe hasara kwa mzazi wake!
Tupo serious kweli?
 
Mimi hicho ndio sielewi. Kwa vile wameona hastahili kuendelea kuwa Mwenyekiti wafanye kampeni ili wapiga kura wasimchague. Haya ya kumtaka apumzike, oh ni ndugu yangu, oh kabila yangu n.k. halina nafasi hapa. Lema hakuwa na haja ya kuweka press conference kutoa taarifa ya kitu ambacho wote tunakijua. Au anaogopa kuwa Mbowe nae atasema " et tu Lema?"

Mimi ningewashauri kuwa pamoja na kumshauri apumzike wangemwambia pia kuwa apumzike katika kuchangia chama kifedha kupita kiasi. Wanachama watakibeba chama chao.

Amandla...
Wanaweweseka na wanajua huenda yule kibaraka wao asishinde uchaguzi
 
Wakuu,

Siku ya jana aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini kupitia akaunti yake ya X aliahidi kwamba siku ya leo Tarehe 14 January 2024 atakuwa anazungumza na wanahabari.

Wengi wameshuku kuwa huenda Lema atazungumzia kuhusu Uchaguzi wa CHADEMA na kuainisha ni mgombea gani ya Freeman Mbowe au Tundu Lissu anamuunga mkono.

Kaa karibu na Jamii Forums kupata updates zote

======================================================

  • Godbless Lema amesema kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na amemuomba Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe apumzike
"Mimi Mbowe ni kaka yangu, tunajuana. Yeye ni Mchaga na mmachame kama mimi, na familia zetu zinafahamiana, ila kwa uchaguzi ujao wa Mwenyekiti namuomba amuachie Tundu Lissu.

Lissu amekuwa Makamu Mwenyekiti, mnadhimu wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, wanaosema hawezi kuwa Mwenyekiti wanataka nani awe?

Kuna watu wanasema Lissu asiwe Mwenyekiti kwasababu hana pesa, sasa niwaambie katika wakati ambao chama kinapaswa kupata kiongozi asiye na hela ni sasa ili wajumbe wajue kuwa chama hakipaswi kuendeshwa kwa pesa za mtu mmoja bali mobilization kutoka kwa watu. CHADEMA inabidi kitafute namba ya ku-rise fund. Kuna watu waliingia kwenye uongozi bila kuwa na pesa"


  • Aidha Godbless Lema amesema kuwa hatogombea Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi wa mwaka 2025



View: https://www.youtube.com/live/n4jGmCXtOsc?si=QELvyU3Ewhqvx9gA




nabii mnyang'anyi mashuhuri wa malori hana ushawishi wala credibility ya kuskizwa na wanachadema kuelekea uchaguzi wao muhimu wa kitaifa,

nadhani inafaa zaidi aendelee kupuuzwa kama alivyo puuzwa na wana Arusha wa chadema 🐒
 
Machame oyee, Machame safii, Embu mwangalie jirani yako mwambie mimi ni mmachame.
Wamachame wabinafsi sana,hawawapendi hata wachaga wa jamii zingine,pale njia panda machame,barabara ya arusha,kuna maduka ya vibanda ni wamachame tupu,hadi boda,ukienda mchaga wa jamii nyingine unaibiwa vitu vyako vyote,unaweza usiuze hata 100.
ukipeleka daladala yako machame to moshi mjini,hupati hata abiria mmoja kama sio mmachame..
 
Wamachame wabinafsi sana,hawawapendi hata wachaga wa jamii zingine,pale njia panda machame,barabara ya arusha,kuna maduka ya vibanda ni wamachame tupu,hadi boda,ukienda mchaga wa jamii nyingine unaibiwa vitu vyako vyote,unaweza usiuze hata 100.
ukipeleka daladala yako machame to moshi mjini,hupati hata abiria mmoja kama sio mmachame..
Duuu. Aisee. Hatari mno.
 
Kadiri Mbowe anakavyokuwa mgumu kuachia kabla ya sanduku la kura...

Matamko yanazidi kuwa mengi....kumsihi aachie ngazi kabla ya uchaguzi, fedheha ya kuachia kabla ni ya muda mfupi kuliko la sanduku la kura, atashindwa hata kumshauri Lissu kwenye mambo ya Msingi
hata akishinda,heshima kwa watu na wanachama haitakuwepo kama zamani,mengi yamesemwa juu yake,kama anabusara,angejitoa tu.
 
mh!
hahahahahahahahahahaahaha
Uchaguzi ukiisha yeye na Lisu wanahama Chadema na makelele hayo

Mbowe bigwa walitaka kumpindua akiwa gerezani sasa kawaibukia sanduku.la kura kuwa njooni tupambane sanduku la kura

Wanapiga miyowe kibao wanajua Mbowe anaenda kuwabwaga sanduku la kura
 
Back
Top Bottom