Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vyama vya kisiasa vinategemea sana good will za watu. Sio tu kwa kura bali na rasilimali watu ( ushauri n.k.) na fedha. Mbowe amejijenga sana. Bila shaka kuna watu wanamchangia pesa kwa sababu wana imani nae. Kuna watu wanampa ushauri wa nini cha kufanya. Hawa wote wanafanya hivyo kwa sababu wana imani nae. Unadhani wataendelea kuwa na moyo wa kushirikiana na CDM baada ya kuona walivyomtendea Mbowe? Thubutu.

Amandla...
waende naye tu, chadema mpya inahitajika
 
Nyerere alikuwa na rasimali watu ambao ni kama baba yake Mbowe alihakikisha anapata suti nzuri kwenda kwenye mambo ya kudai uhuru.Hapa tuelewane kama huna hela lazima utakuwa na marafiki wenye hela hata kama ni kidogo.Ila kama huna na marafiki zako hawana.Utaona kila aliye nacho ni fisadi.

..utamaduni wa kuona kila aliyenacho ni mwizi, mhujumu, fisadi, ni matokeo ya sera za kijamaa za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

..Ni kitu gani kilimtokea Baba wa Taifa mpaka akafikia kuwa na sera za kijamaa zinazojenga chuki na kutweza wale wenye nacho?
 
Nje ya siasa.
Huu uchaguzi wa chadema umenipa funzo kubwa sana kuhusu binadamu.

Binadamu ni kiumbe Cha ajabu sana! Nimefunza pa kubwa!

Najaribu kuwaza, FAM akishinda Hali itakuwaje katika chama?
percentage ya kushinda mbowe inazidi kupungua kadri siku zinavyoenda kuelekea uchaguzi huo, labda ashinde ki namna
 
Uchaguzi ukiisha yeye na Lisu wanahama Chadema na makelele hay
yao

Mbowe bigwa walitaka kumpindua akiwa gerezani sasa kawaibukia sanduku.la kura kuwa njooni tupambane sanduku la kura

Wanapiga miyowe kibao wanajua Mbowe anaenda kuwabwaga sanduku la kura
kwa vibe hili mbowe atashinda? Hebu acha utani!
 
Yeye ndio anajivunjia Heshima kwa kutokusoma alama Za Nyakati, Mjadala wa JPM tu kutaka Kuongeza terms kwenye ofisi mlipiga kelele kweli kweli leo mbowe amekuwa chairman for 21 Yrs bado mnataka tu aendelee, Kwa nafasi yake pia anaona akiwa challenged na Mgombes yoyote anaona ni Kuvunjiwa heshima mana miaka yote amekuwa kama Mgombea pekee tu na kufanyia Figisu wenzie refer issue za Kina Chacha Wangwe na Zito,

Sasa leo amepata Opponent ndio analeta story za Kuvunjiwa heshima apambane na Platform hio na alichosema leo Lema hakijavunja Katiba ya chama ni maoni yake na kama Mwanachama ni haki yake kutangaza mgombea anayetaka
Mnachanganya nafasi ya Mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa chama cha siasa. Ingawa nchi yetu ina ukomo wa mtu kuwarais lakini vyama vingi vya siasa havina ukomo wa kuwa kiongozi. Hata CCM haina ukomo. Hata nchi kama Marekani hazina ukomo wa Mwenyekiti wa chama cha siasa. Kuna sababu ya kutaka nafasi ya Amiri Jeshi Mkuu kuwa na ukomo. Amiri Jeshi Mkuu anaweza kutumia dola kubaki madarakani asipowekewa ukomo. Hizo nguvu, Mwenyekiti wa Chama cha siasa hana.

Mbowe ana haki ya kugombea kwa vile Katiba ya Chadema haina huo ukomo. Mnapotaka asigombee mnakuwa mnataka kumnyima haki yake ya kikatiba.

Ya Chacha Wangwe siijui ila najua aliyesimamia suala la Zitto na wenzake kuvuliwa uanachama ni Lissu. Hata kesi alisimamia yeye.

Kwani nani kasema Lema kavunja Katiba? Kama vile alivyo na haki ya kutoa msimamo wake hadharani ndio vile na sisi tuna haki ya kumkosoa.

Amandla...
 
Shukran sana Mh Lema kutoka hadharani. Hii ni move nzuri kwa wapenda mabadiliko. Sasa Mbowe ajione kabisaa jinsi alivyochemsha. Mh Mbowe sijui alishikwa wapi, ila yeye kuside na watawala —amechemsha sana. Wananchi wanaona kila kitu.. Sijui alidhani watu ni wajinga!!
 
Lema na team Lisu acheni kelele wacheni sanduku la kura wapiga jura waamue

Mbona mna makelele sana mnataka Lisu apate ushindi wa mezani sio sanduku la kura mnaogopa nini?

Wqpiga kura walio wengi acheni waamue
It's very simple. Ukiona ambaye anaungwa mkono na ccm basi ujue huyo hafai hata bure na moja kwa moja ujue ni kibaraka wao.
 
Iwapo team TAL,itashinda uchaguzi, Baada ya uchaguzi huu wa chadema kumalizika,kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Ninashauri serikali ya CCM kujenga magereza na vituo vya polisi vingi kwani idadi ya wafungwa na wakamatwaji itaongezeka kwa asilimia 1000
Mithali 26:27
Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

Mungu hadhihakiwi, na mwishowe yatakayo wakuta nyie wenyewe mtajua hamjui
 
Kumbe kulikukwa na mkakati maalum ulio sukwa na viongozi waandamizi wa Chadema ili kumg'oa Kamanda Mbowe.
Ukimsikiliza Lema utabaini njama hizo.
Mbowe usikubali kuondolewa kwa njama na hila.
 
Back
Top Bottom