Kuna watu wanapata umaarufu sana na mwisho wanapata kiburi cha uzima na kuanza kutukana watumishi na hata kumkufuru Mungu.
Katika ukurasa wake wa X(Twitter) Godbless Lema kaandika,
"Baba Askofu (picha ya Askofu Malasusa) Bwana Yesu asifiwe sana. Pole na kazi ya Mungu. Huku Arusha tunaendelea vizuri kiasi na watu wanaendelea kusubiri TAMKO la Kanisa unaloliongoza wewe juu ya ukatili mkali huko NGORONGORO na Utekaji na utesaji dhidi ya raia. Msalimie sana YESU."
Hiki ni kiburi.
Namshauri Lema kwa ukurasa huo huo aombe radhi kwa kuwaona watumishi wa Kanisa kuwa political sparring partners.
Mbaya zaidi kulifedhesha na kudhihaki Jina lipitalo majina yoye, YESU.
Asipofanya hivyo hizo salamu anazozitafuta atazipata, na si muda mrefu.