..Lema ameuliza maswali ya msingi sana.
..Watanzania tunaogopa kuvihoji vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
..Tumejitenga navyo. Tunaamini sio vyetu ni vya watawala.
Mkuu
JokaKuu
Maswali ya Lema ni Muhimu sana kuliko watu wanavyoyachukulia kirahisi na kimtaani taani tu
1. Kwanini CDF na TISS wanakutana na Rais kila mara au siku akini hawakumwambia habari hiyo kwa siri
2. Kwanini Jeshi lime 'appeal' kwa Wananchi hadharani
Hoja: Kwa mujiwbu wa CDF Mstaafu Mabeyo, Jeshi ni 'state' ndani ya state kwa maana ina kila kitengo
Mabeyo alikuwa mkuu wa Intelejensia Jeshini kwahiyo anajua anasema nini.
CDF ni Mkuu wa Jeshi lakini pia ana uongozi mzima 'top military brass' , washauri wake wakuu na wa karibu.
Hotuba yake ilipitia katika '' baraza'' na hoja ikaonekana isemwe na CDF.
Kuna uwezekano zipo taarifa hazijafanyiwa kazi na tatizo linazidi kukua! au kuna '' Politics'' zinazo ignore tatizo.
Kuna uwezekano pia Intelejensia ya Jeshi imebain kuna 'infiltration' katika vyombo vingine.
Njia nzuri ni kumweleza Rais hadharani hali halisi pengine na ukubwa wake na uzito wa tatizo
Pili, ku appeal katika public huenda ni kutokana na ukubwa wa tatizo, na kwa kuelewa mipaka ya Jeshi pengine wameona kulisema hadharani kutasaidia Wazalendo kufichua uozo kule wasikoweza kufika.
Swali lingine ni kwamba kwanini kumetumika neno '' Katika nafasi za Maamuzi''
Kuna uwezekano kabisa watoa maamuzi mazito ya nchi mmoja ni hao Wakimbizi.
Haiwezi kuwa Diwani, Mbunge, Naibu Waziri au hata Waziri wa Kawaida. Ni lazima awe kuanzi Waziri Mwandamizi
GENTAMYCINE anajua huko Visiwa vya Guam au Puerto Rico nafasi za maamuzi zipoje