Orodha zao YUENI ,si injili si kurani
Vile umeiamini,imekuwa ya mbiguni ?
Vifutu viseme nini,kwani vina shida gani ?
Dawa ya deni kulipa,siyo kukimbia nchi.
Asemaye ni yueni, kuwananga Amerika?
Au dhidi ya Sudani, China au Dominika?
UN dhidi ya nani, na nyie vinyangarika?
Mbingu zenu Magwajima, ziaminike na nani?
Mavifutu yana shida, hayo ndiyo mauaji!
Hayo ndiyo yatuwinda, pande zote za majiji,
Hayo ndiyo huviunda, viroba vya kwenye maji!
Tumeshaumwa vifutu, heri Lema kastuka!