Godbless Lema ukimbizi: Kaingia jela ya kufikirika

So, ina maana unataka kusema Lissu kupewa ukimbizi? Wakati mwenye alishasema ana kibali cha kuishi Ubeligiji?
Kupata kibali cha ukimbizi is a long process. Lissu yuko kwenye process ya kuomba kibali cha ukimbizi. Wakati wa kungoja maamuzi ya mwisho, muombaji hupewa residence permit. Hiyo ndiyo aliyokuwa nayo Lissu.
 
Sidhani kama unaelewa utofauti kati ya hivyo vitu viwili ulivyoviandika (Residence permit and ukimbizi - refugee). Huwezi kuwa na residence permit ambayo ina hadhi ya juu na inakuruhusu kufanya mambo mengi, ukaenda kuomba ukimbizi ambao una hadhi ya chini na uhanyimwa uhuru kufanya mambo yako ikiwa pamoja na kusafiri huku na kule.

Lissu mwenye kwa matamshi yake amesema yeye hajaomba ukimbizi nchi yoyote

Lema si mkimbizi, wewe msajili wao?
mmezidi ubazazi, mwawakimbiza makwao,
kwani ya nini makazi, si bora ya roho zao?
Yu eni hechi si ara, wajua ni mkimbizi!

(UNHCR = "Yu eni hechi si ara" wanayo orodha ya wakimbizi. Jiridhishe Lema hayumo.)
Ni mipango mkakati,kufitini Tanzania
Na kamwe hafurukuti,atakuja kujutia
Yakamkuta mauti,kamwe kwetu kuingia
Lema kweli ni jahula,dawa ya deni kulipa.
 
Hizi tuhuma Senzige, zakushusha hadhi yako,
Hizi waambie ndege, siyo wasomi wenzako,
Au umepata mbege, kuzipanga beti zako?
Linganisha usemayo, na ukweli hapa chini!

Je Lema si mkimbizi, wewe msajili wao?
Au hata mwangalizi, wa wale wakimbiao?
Kwa wote wakimbizi, si ipo orodha yao?
UNHCR, Orodhani yumo Lema!

Orodha yako ni ipi, au wapata Lumumba?
Sababu za Lema zipi, au macho mmefumba?
Adaiwacho ni kipi, mbona mnayumba yumba!
Msicheze na UN, karibu mtaumbuka!
 
Namhurumia sana Godbless Lema.
Kaingia jela ya kufikirika, jela ambayo ni yeye mwenyewe atajua ni kifungo cha miaka mingapi na atatokaje kwa msamaha wake mwenyewe.

Mbaya zaidi familia nzima imemsindikiza jela hiyo ya kufikirika.

Lema ata enjoy miezi michache ya kwanza huko Canada, pamoja na familia.
Baada ya hapo ndipo ataelewa uzuri na utamu wa Tanzania, maji ya kunywa bure, hewa bure, shule karo za watoto karibu na bure, chakula unarudi kutoka Moshi na mikungu miwili ya ndizi bure!
Mbge ndo usiseme!

Tuliokaa nje muda kidogo tunaelewa jinsi matatizo tuliyo nayo, yalivyotukomaza na kuishi nayo kama ndugu.

Nampa pole Lema maana alisema wanataka kumuua.
Bado angeweza kubaki na kutatua hilo fumbo na shinikizo.

Tanzania ni nzuri!
Itabidu afungue baa huko au duka la reja reja
 
Ughaibuni vibali vya biashara yoyote ni very very strictly controlled.
Vibali huko vina vipengele vingi sana toka Afya, ajira,leseni, enviromental na vingine vingi.
Na hapo hapo lazima atapata ushindani kwa waliomtangulia kuuza ulabu mtaani, na watapiga vita.
Hata hivyo ni vizuri akajaribu.
 
Kila nchi unao matajiri na maskini, kama unafikiria kila mtu huko Ulaya au Canada ni tajiri wewe bado sana tu. Pole sana.
Hivi katika maandishi uliyosoma kuna sehemu yoyote nilipoandika kuwa "...kila mtu huko au Canada ni tajiri"? Haya maneno umeyatoa wapi kama sio kutoelewa kilichoandikwa na wewe kujibandikia unayofikiri wewe?

Hata hivyo ngoja nikufahamishe: utajiri sio hoja kuu hapa. Unaweza kuwa tajiri wa mali katika nchi ambayo inawakandamiza wananchi wake, na utajiri huo wa mali ukawa haumpi mtu huyo furaha ya kuwa nao. Hana tofauti kubwa na maskini waliomo nchini humo, kwa sababu wote hawako HURU; ni mateka wa mtu mmoja anayefahamika kuwa kiongozi au mtawala wa nchi hiyo.

Maskini na tajiri waliomo katika nchi inayoheshimu HAKI za raia zake na kuwa HURU, ni tofauti na hao wanaoishi chini ya ukandamizi.

Fungua akili yako uelewe nilichoandika, usibakie tu kuwa shabiki asiyetumia akili yake kufikiri.
 
Hizi tuhuma Senzige, zakushusha hadhi yako,
Hizi waambie ndege, siyo wasomi wenzako,
Au umepata mbege, kuzipanga beti zako?
Linganisha usemayo, na ukweli hapa chini!

Je Lema si mkimbizi, wewe msajili wao?
Au hata mwangalizi, wa wale wakimbiao?
Kwa wote wakimbizi, si ipo orodha yao?
UNHCR, Orodhani yumo Lema!

Orodha yako ni ipi, au wapata Lumumba?
Sababu za Lema zipi, au macho mmefumba?
Adaiwacho ni kipi, mbona mnayumba yumba!
Msicheze na UN, karibu mtaumbuka!
Mwashabikia ujinga,eti nchi kakimbia
Niambie lipi janga,yeye limemfikia ?
Mambo hayo ya kupanga,mzidi kulialia
Unang'ang'ana orodha,ni watu wameandika !
 
Namhurumia sana Godbless Lema.
Kaingia jela ya kufikirika, jela ambayo ni yeye mwenyewe atajua ni kifungo cha miaka mingapi na atatokaje kwa msamaha wake mwenyewe.

Mbaya zaidi familia nzima imemsindikiza jela hiyo ya kufikirika.

Lema ata enjoy miezi michache ya kwanza huko Canada, pamoja na familia.
Baada ya hapo ndipo ataelewa uzuri na utamu wa Tanzania, maji ya kunywa bure, hewa bure, shule karo za watoto karibu na bure, chakula unarudi kutoka Moshi na mikungu miwili ya ndizi bure!
Mbge ndo usiseme!

Tuliokaa nje muda kidogo tunaelewa jinsi matatizo tuliyo nayo, yalivyotukomaza na kuishi nayo kama ndugu.

Nampa pole Lema maana alisema wanataka kumuua.
Bado angeweza kubaki na kutatua hilo fumbo na shinikizo.

Tanzania ni nzuri!
Bora kwenye hiyo u call it jela ya kufikirika kuliko KABURI... CCM ya leo inaua watu, kuwapa vilema vya maisha wananchi wafanya, kiwafunga vifungo virefu kwa makosa ya kubambikiza nk...shame on you!! HOJA hamna iliyobaki ni kuwatisha wananchi.
 
Mwashabikia ujinga,eti nchi kakimbia
Niambie lipi janga,yeye limemfikia ?
Mambo hayo ya kupanga,mzidi kulialia
Unang'ang'ana orodha,ni watu wameandika !

Milumumba mna nini, vichwani hamna kitu!
Hii haijulikani, si yenu hii mijitu?
Kawakimbia kwa nini, hilo uliza vifutu!
Orodha zao UN, huwezi zibeza wewe!

Nyie mwaona utani, wanapopotea watu,
Azory na kina Beni, leo hii si wenzetu,
kwamba hawajulikani, vile kwenu siyo kitu?
Orodha zao UN, huwezi zibeza wewe!
 
Orodha zao YUENI ,si injili si kurani
Vile umeiamini,imekuwa ya mbiguni ?
Vifutu viseme nini,kwani vina shida gani ?
Dawa ya deni kulipa,siyo kukimbia nchi.
 
Kama kwenda kuishi Canada ni jela, hebu Canada wakosee waje waseme watu waliochoka kukaa Tanzania waende jela Canada.

Ndani ya mwezi watanzania watakaokuwa wamebaki ni wale wanaotembelea maVX ya umma, na wafanyabishara wachache wenye vipato vikubwa.

Kisha baada ya mwaka wawaulize watanzania walioko jela huko Canada, wangapi wanataka kutoka kifungoni Canada kurudi Tanzania, uone kama kuna mtu atakubali kurudi.
Achana na mtoa mada.. amevurugwa.. eti Canada ni kifungo..!!
 
Sidhani kama unaelewa utofauti kati ya hivyo vitu viwili ulivyoviandika (Residence permit and ukimbizi - refugee). Huwezi kuwa na residence permit ambayo ina hadhi ya juu na inakuruhusu kufanya mambo mengi, ukaenda kuomba ukimbizi ambao una hadhi ya chini na uhanyimwa uhuru kufanya mambo yako ikiwa pamoja na kusafiri huku na kule.

Lissu mwenye kwa matamshi yake amesema yeye hajaomba ukimbizi nchi yoyote

Basi wewe ndio huelewi. Ukimbizi unatoa haki zaidi kuliko residence permit. Mkimbizi ana haki almost like raia.
 
Nasubiri kusikia hizo haki mkimbizi anapewa kuliko residence permit holder. Haki za matibabu? Haki za kujiendeleza na masomo, haki ya kufanyakazi? ukiwa permit holder hizo haki unapewa pia.

Kitu cha kuzingatia, ukimbizi sio permanent? Unapewa ukimbizi mpaka pale inapoonekana usalama wako umetengemaa. Sasa unawezaje kuweka investment kwenye nchi iliyokupa ukimbizi wakati hujuwi lini utaambiwa urudi kwenu au uhamie nchi nyingine?
 
Namhurumia sana Godbless Lema.
Kaingia jela ya kufikirika, jela ambayo ni yeye mwenyewe atajua ni kifungo cha miaka mingapi na atatokaje kwa msamaha wake mwenyewe.

Mbaya zaidi familia nzima imemsindikiza jela hiyo ya kufikirika.

Lema ata enjoy miezi michache ya kwanza huko Canada, pamoja na familia.
Baada ya hapo ndipo ataelewa uzuri na utamu wa Tanzania, maji ya kunywa bure, hewa bure, shule karo za watoto karibu na bure, chakula unarudi kutoka Moshi na mikungu miwili ya ndizi bure!
Mbge ndo usiseme!

Tuliokaa nje muda kidogo tunaelewa jinsi matatizo tuliyo nayo, yalivyotukomaza na kuishi nayo kama ndugu.

Nampa pole Lema maana alisema wanataka kumuua.
Bado angeweza kubaki na kutatua hilo fumbo na shinikizo.

Tanzania ni nzuri!
Kifo cha kuuawa wewe na familia yako , na utamu wa Tanzania kipi ni kizuri zaidi?
 
Nasubiri kusikia hizo haki mkimbizi anapewa kuliko residence permit holder. Haki za matibabu? Haki za kujiendeleza na masomo, haki ya kufanyakazi? ukiwa permit holder hizo haki unapewa pia.

Kitu cha kuzingatia, ukimbizi sio permanent? Unapewa ukimbizi mpaka pale inapoonekana usalama wako umetengemaa. Sasa unawezaje kuweka investment kwenye nchi iliyokupa ukimbizi wakati hujuwi lini utaambiwa urudi kwenu au uhamie nchi nyingine?
Ukimbizi sio permanent kwenye nchi gani?
Hizi nchi ukija kama mkimbizi ukipokelewa it is just a step towards uraia.

Usichanganye residence permit na permanent residence. Residence permit can be a long stay visa. By long stay, it means the visa is longer than 90 days.

Mkimbizi ana haki ya kupewa makazi, jobless allowance kama hana kazi, matibabu. Residence permit huwezi kupewa kama huna kazi au proof ya kipato.
 
Kama kwenda kuishi Canada ni jela, hebu Canada wakosee waje waseme watu waliochoka kukaa Tanzania waende jela Canada.

Ndani ya mwezi watanzania watakaokuwa wamebaki ni wale wanaotembelea maVX ya umma, na wafanyabishara wachache wenye vipato vikubwa.

Kisha baada ya mwaka wawaulize watanzania walioko jela huko Canada, wangapi wanataka kutoka kifungoni Canada kurudi Tanzania, uone kama kuna mtu atakubali kurudi.
Kwa utawala huu wa muhutu ni heri kuwa mkimbizi. Zaidi ya visasi na mauaji lakini pia maisha ni magumu mno. Kifupi, hafai kuwa Rais na hakushinda uchaguzi. Asilimia 84 ni za uchafuzi.
 
Hana muda huyo ataunga juhudi Slaa alikua huko kapiga sana box supermarket mok wakampa mchongo hapo Stockholm
 
Back
Top Bottom