Godbless Mushi adaiwa kujaribu kumbaka mtoto wake wa miaka mitano

Godbless Mushi adaiwa kujaribu kumbaka mtoto wake wa miaka mitano

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limemkamata na linaendelea kumhoji Godless Mushi (39) mfanyabiashara wa kuza vifaa vya magari kwa tuhuma za kujaribu kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano

Taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya Habari inasema mnamo Aprili 2/2023 saa nne usiku katika mtaa wa Shibula wilayani llemela mwanaume huyo alitaka kumfanyia mtoto wake kitendo cha udhalilishaji wa kingono wakati akiwa amelala chumbani kwenye kitanda cha wazazi wake wakati mama yake mazazi akiwa anaendelea na shughuli zake za nyumbani


Aidha jeshi hilo kupitia dawati la jinsia na Watoto limesema uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea kwa kuwahoi mashahidi na kumfanyia binti huyo chunguzi wa kitaalamu, na kwamba wanashirikiana na ofisi ya Ustawi wa jamii Mkoa wa Mwanza na upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

Chanzo: East Africa TV
Harafu mnasema adhabu za kifo zifutwe
 
Back
Top Bottom