Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana Mbezi Beach

Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana Mbezi Beach

Status
Not open for further replies.
Tulipoa na haya mambo yenu ya kutekana tekana ama kutishana kutekana wakati DJ wenu yupo segedance sasa hivi yupo uraiani mnaanza kuja na hizi story aaagh

kapotea msaidizi wa dj, tumeona DJ kachuna sasa hivi michezo inaibuka upyaaaa aaagh mrudisheni dj stoo tukae kwa aman
 
JARIBIO LA KUTEKWA MALISA GJ NA WATU WASIOJULIKANA LINATUKUMBUSHA HALI YA USALAMA WETU.

Malisa GJ was almost to be kidnapped na maafisa wa usalama (watu wasiojulikana). Tukio hili, kama lingefanikiwa, sijui ningelikuwa kwenye huzuni kiasi gani, sijui ningekuwa kwenye uchungu kiasi gani? haswa ninapomkumbuka Ben rabiu saanane.

Mungu ni mwema kwamba, mipango hii ya uovu imeshindikana na kufeli dakika za mwisho kabisa na ambapo watekaji na wauwaji hao kwa jina la usalama wa Taifa wakashindwa kutekeleza mipango yao na habari zao zimetufikia mapema. Mipango ambayo muda kama huu tungelikuwa kwenye hali ya kumpoteza kijana mahiri anaetumia weledi, uzalendo na haki zake za kikatiba kuijenga nchi hii.

Tukio hili lisipite kwa bahati mbaya, lisipite kimyakimya. Tujue kwamba kuna taarifa kwamba kuna watu wamechuliwa kwenye nyumba hiyo, kama mbadala baada ya jaribio la Malisa Gj kushindikana, je ni wakina nani hao waliochukuliwa? Na kwanini wao wachukuliwe usiku, nani amewapa mamlaka hao mashushu kuchukua watu tena usiku kinyume kabisa na sheria za usalama wa Taifa?

Tukio hili litukumbushe kwamba, watu wasiojulikana walijificha ndani ya mfumo wetu wa usalama wa Taifa, kwamba bado wapo na kazi yao ipo palepale. Wale ambao ni sehemu ya juu za mamlaka za nchi ambao ndio wanaowatuma kuteka na kuua watu ambao ni wakosoaji wa serikali nao bado dhamira zao ziko palepale na mipango yao iko palepale, sema tu Mungu amewaumbua mapema.

Tusijisahau kwamba sisi ambao mara kadhaa tumenusurika kutekwa na watu hawa, kwamba bado tunatafutwa kwa udi na uvumba. Bado watu hawa ambao wanashiriki kwenye misiba ya watu ambao wamehusika kuwaua tena wakilia kwa machozi ya unafki Wanaendelea kupanga na kuchukua hatua za kutokomeza kabisa kizazi cha ukosoaji dhidi ya serikali.

Watu hawa (kamati ya roho mbaya) ndio waliomteka Ben saanane, ndio waliojaribu kumuua Tundu Lisu na ndio hawahawa ambao leo walijaribu kumteka Malisa Gj bila mafanikio, Asnte Mungu.

Usalama wetu uko mikononi mwa Mungu mwenyewe. Watu hawa wanaoratibu utekaji huu wa wakosoaji wa serikali, wamefanikiwa kuwateka viongozi wa dini kadhaa, wamefanikiwa kuwateka wanasiasa kadhaa na wamefanikiwa kuwateka wajinga kadhaa, ambao wameendelea kutumika kama kinga yao dhidi ya unyama wao wanaoutenda kwenye nchi hii, unyama wa kuwateka, kuwapiga risasi, na kuwafungia kwenye viroba watu ambao wamekataa kusifiasifia upumbavu.

Ujenzi wa miundombinu umegeuka kuwa kinga ya watu wasiojulikana, watu ambao wameendelea kukikingiwa kifua na serikali ya Magufuli, kwa kukataa uchunguzi huru na kimataifa dhidi ya kundi hili la kigaidi, jambo ambalo linatufanya kuwahusisha watu hawa na mamlaka za serikali ya Tanzania.

Leo tena, Mungu ametukumbusha kwa upendo kabisa, kupitia kijana wake mahiri, Malisa Gj kwamba bado hatupo salama. Bado maadui wa haki, demokrasia na utawala wa sheria wanaendelea kuwatafuta na kuwatokomeza wale wote wanao ukosoa utawala huu wa kiimla (udikteta). Bado wale watekaji hawajamaliza mission yao, bado dhamira za mamlaka za serikali za siri ni kuhakikisha watanzania wote wanamsifia tu mkuu, si umnakumbuka maneno ya Kabudi!!

Ndugu zangu, tuendelee kuwa makini sana, maana wauwaji na watekaji wetu, sisi ambao tumechagua upande wa haki, upande wa kuikosoa serikali, ndio kwanza tuko nao kwenye misiba na tunalia nao, ndio kila kukicha wanakesha na viongozi wa dini, sasa wanafikili tumesahau....

Pole sana kamanda Malisa Gj
Wakati Mbowe yupo mahabusu haya mambo yalitulia sasa yamerudi tena...kwani dogo amehoji matumizi ya ruzuku au ni mfuasi wa Tundu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni genge la watu basi serikali itafute namna ya kudhibiti maana linachafua taswira yake.

Kama ni miongoni mwa taasisi za serikali na iache mara moja.

Lakini kama ni wasiojulikana kweli,inabidi kwa ujumla wetu tutafute njia ya kukabiliana na hilo bila kuingiliwa na yeyote aliyeshindwa kutulinda.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe (wasiojulikana) ndiyo maafisa usalama!!!! Hatimaye wamejulikana sasa!
 
Mimi mwenyewe naona Kuna (MKAKATI) wa Kutusakama>kutulege>Kutuvuluga>

Kutusambalatisha, Watu au Vijana Wenye>
Erementi >za Tundu Lissu na huu mpango umekaziwa Sana baada ya Lissu kuonyesha( nia) ya urais na ziara za nje.

Ukionyesha >kumwelewa lisu imeshakua shida kubwa Awamu hii ya Jiwe... Sasa kunachangamoto kua mpinzani.

Zaidi na zaidi ukiwa unamwelewa Sana lissu > mimi mwenyewe nimepata msukosuko baada ya kuonyesha dalili za lissu >kwenye mji wetu!

Aluta continuea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitahidi kuandika lugha fasaha.

Anyway huyu mungu mtu tutshindwa kukabiliana nae sababu ya unafiki wa watu wachache wanakula matunda yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitachangia kikwaresmakwaresma....'Ninyi mnaowatesa maskini jueni kwamba malaika wao wapo mbele yangu siku zote wakinililia ipo siku nitawasikia na kuwajibu' mwisho wa kunukuu.
 
Tuombe tu MUNGU amuepushe na 'wanaojulikana', yaani waliovamia makazi yake na 'wasiojulikana' yaani kama atapotezwa kama ben saanane! Tuombe MUNGU amlinde na dhidi ya mabaya yote yaliyopangwa na 'watesi' wake!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom