Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana Mbezi Beach

Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana Mbezi Beach

Status
Not open for further replies.
#TAARIFA: Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa watu wanaodai kuwa maafisa usalama wamemvamia kamanda Malisa GJ maeneo ya Mbezi Beach. Chochote kitakachotokea juu yake wao ndio watakuwa na majibu!
Mmm Malisa alishawahi kushukuru jeshi la polisi kuwahi kumtetea yeye alipovamiwa Kilimanjaro nyumbani kwake . Swali Malisa pesa za kujenga nyumba za uhakika Kilimanjaro na Mbezi beach na Arusha katoa wapi ? Takukuru na TRA ,ingieni kazizi yawezekana ni money laundering ingieni kazini haraka.Malisa hana uwezo wa kumiliki nyumba arusha,kilimanjaro na mbezi Dar es salaam.kipato chake kidogo mno tena mno
 
Kamuulize dikteta na dhalimu kama kaulizia uchunguzi kuhusu kutekwa kwa MO Kwanini hakuulizia kuhusu kutekwa kwa Roma, shambulizi la kutaka kumuua lissu, kupotea kwa Azory na Ben Saanane pamoja na miili iliyookotwa ufukweni? Muulize huyo dhalimu kama hahusiki anahofia nini kuwakaribisha FBI au UK investigation unit?
Hiyo miili iliyookotwa ufukweni ni ya kina nani mbona hatujawahi kusikia ndugu zao wakiitafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.... SHUKRANI YUPO SALAMA UKITOKEA AMEPATWA NA LOLOTE NI HAOHAO TUTAWAHISI.
SWALI KWANI WANAMAMLAKA YA KUKAMATA?
 
Hakuna wa kuwachukulia hatua Mrs Van maana hivi ni vikaragosi vya dikteta na dhalimu anavyovitumia ili kuwaweka raia kwenye hofu kubwa na huku akivuruga amani na mshikamano vilivyojengwa kwa muda mrefu na Baba wa Taifa.

Na kina musiba mbona kila siku wanawakashifu wapinzani na hawajawahi chukuliwa hatua yoyote
 
Unaishi Tanzania ipi taahira wewe?

Nimeuliza hiyo miili kuna ndugu walishawahi kujitokeza kuulizia ndugu zao? Sijakuambia uniwekee video ya sheikh ponda. Kwasababu nayeye anaongea kama unachoongea wewe hapa. Miili inayookotwaga baharini inaweza kutokea popote pale kwenye ukanda ambao nchi inapakana nao kama Somalia, Kenya n.k siyo lazima iwe imetoka Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu zwazwa wa lumumba kaongea hivi wiki chache zilizopita lakini hakuna kiongozi yeyote yule ccm au Serikalini aliyekemea kauli yake, ina maana wanaunga mkono maneno yake. Maneno haya haya angeyasema mtu wa Chadema dhidi ya kiongozi wa Serikali au ccm masaa machache tu angeshawekwa lupango na kwa kipigo kikali sana.



Na kina musiba mbona kila siku wanawakashifu wapinzani na hawajawahi chukuliwa hatua yoyote
 
Onyo Mabalozi ni marufuku kuandika mitandaoni nendeni direct kwa waziri
 
Miili iokotwe Tanzania Serikali ikae kimya kabisa bila uchunguzi wowote ule bila kuulizia nchi za jirani kama kuna watu wamepotea huko, lakini wawe na assumption kwamba hawa si Watanzania bila ushahidi wowote ule!

Una ufinyu mkubwa sana wa akili.

Nimeuliza hiyo miili kuna ndugu walishawahi kujitokeza kuulizia ndugu zao? Sijakuambia uniwekee video ya sheikh ponda. Kwasababu nayeye anaongea kama unachoongea wewe hapa. Miili inayookotwaga baharini inaweza kutokea popote pale kwenye ukanda ambao nchi inapakana nao kama Somalia, Kenya n.k siyo lazima iwe imetoka Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona polisi wetu wana weledi tatizo linakuja kwa watu wasiojulikana pamoja na kiongozi wao. Wanaonekana ni watu wenye nguvu polisi wanaufyata!
 
JARIBIO LA KUTEKWA MALISA GJ NA WATU WASIOJULIKANA LINATUKUMBUSHA HALI YA USALAMA WETU.

Malisa GJ was almost to be kidnapped na maafisa wa usalama (watu wasiojulikana). Tukio hili, kama lingefanikiwa, sijui ningelikuwa kwenye huzuni kiasi gani, sijui ningekuwa kwenye uchungu kiasi gani? haswa ninapomkumbuka Ben rabiu saanane.

Mungu ni mwema kwamba, mipango hii ya uovu imeshindikana na kufeli dakika za mwisho kabisa na ambapo watekaji na wauwaji hao kwa jina la usalama wa Taifa wakashindwa kutekeleza mipango yao na habari zao zimetufikia mapema. Mipango ambayo muda kama huu tungelikuwa kwenye hali ya kumpoteza kijana mahiri anaetumia weledi, uzalendo na haki zake za kikatiba kuijenga nchi hii.

Tukio hili lisipite kwa bahati mbaya, lisipite kimyakimya. Tujue kwamba kuna taarifa kwamba kuna watu wamechuliwa kwenye nyumba hiyo, kama mbadala baada ya jaribio la Malisa Gj kushindikana, je ni wakina nani hao waliochukuliwa? Na kwanini wao wachukuliwe usiku, nani amewapa mamlaka hao mashushu kuchukua watu tena usiku kinyume kabisa na sheria za usalama wa Taifa?

Tukio hili litukumbushe kwamba, watu wasiojulikana walijificha ndani ya mfumo wetu wa usalama wa Taifa, kwamba bado wapo na kazi yao ipo palepale. Wale ambao ni sehemu ya juu za mamlaka za nchi ambao ndio wanaowatuma kuteka na kuua watu ambao ni wakosoaji wa serikali nao bado dhamira zao ziko palepale na mipango yao iko palepale, sema tu Mungu amewaumbua mapema.

Tusijisahau kwamba sisi ambao mara kadhaa tumenusurika kutekwa na watu hawa, kwamba bado tunatafutwa kwa udi na uvumba. Bado watu hawa ambao wanashiriki kwenye misiba ya watu ambao wamehusika kuwaua tena wakilia kwa machozi ya unafki Wanaendelea kupanga na kuchukua hatua za kutokomeza kabisa kizazi cha ukosoaji dhidi ya serikali.

Watu hawa (kamati ya roho mbaya) ndio waliomteka Ben saanane, ndio waliojaribu kumuua Tundu Lisu na ndio hawahawa ambao leo walijaribu kumteka Malisa Gj bila mafanikio, Asnte Mungu.

Usalama wetu uko mikononi mwa Mungu mwenyewe. Watu hawa wanaoratibu utekaji huu wa wakosoaji wa serikali, wamefanikiwa kuwateka viongozi wa dini kadhaa, wamefanikiwa kuwateka wanasiasa kadhaa na wamefanikiwa kuwateka wajinga kadhaa, ambao wameendelea kutumika kama kinga yao dhidi ya unyama wao wanaoutenda kwenye nchi hii, unyama wa kuwateka, kuwapiga risasi, na kuwafungia kwenye viroba watu ambao wamekataa kusifiasifia upumbavu.

Ujenzi wa miundombinu umegeuka kuwa kinga ya watu wasiojulikana, watu ambao wameendelea kukikingiwa kifua na serikali ya Magufuli, kwa kukataa uchunguzi huru na kimataifa dhidi ya kundi hili la kigaidi, jambo ambalo linatufanya kuwahusisha watu hawa na mamlaka za serikali ya Tanzania.

Leo tena, Mungu ametukumbusha kwa upendo kabisa, kupitia kijana wake mahiri, Malisa Gj kwamba bado hatupo salama. Bado maadui wa haki, demokrasia na utawala wa sheria wanaendelea kuwatafuta na kuwatokomeza wale wote wanao ukosoa utawala huu wa kiimla (udikteta). Bado wale watekaji hawajamaliza mission yao, bado dhamira za mamlaka za serikali za siri ni kuhakikisha watanzania wote wanamsifia tu mkuu, si umnakumbuka maneno ya Kabudi!!

Ndugu zangu, tuendelee kuwa makini sana, maana wauwaji na watekaji wetu, sisi ambao tumechagua upande wa haki, upande wa kuikosoa serikali, ndio kwanza tuko nao kwenye misiba na tunalia nao, ndio kila kukicha wanakesha na viongozi wa dini, sasa wanafikili tumesahau....

Pole sana kamanda Malisa Gj
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom