God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Hujaeleza ulimwengu uliopo unathibitisha vipi Mungu yupo.

Unaeleza imani yako tu, ambayo si lazima iwe kwenye ukweli.

Na hata hiyo imani yako, kwamba ulimwengu upo kwa kusudi fiulani, huwezi kuithibitisha.

Na hata hilo neno "kusudi" hujalinyambulisha kutueleza ukiongelea "kusudi" unamaanisha nini.
 
Sasa tofauti ya huyo na wewe kudai una freewill wakati hauwezi kurudi nyuma katika muda ni nini?
Sasa tofauti ya huyo anayedai mpaka kuwepo gari ya rangi ya udhurungi ndiyo aseme amechagua rangi. Na wewe unayetaka mpaka urudi nyuma ya mda kwamba ndio ukohuru kutumia will yako na muda wako ni ipi?

Machaguo uliyonayo katika kuutumia muda wako ni huru kabisa kadiri ya mambo unayohitajika kuyachagua katika muda duniani. Uko huru
 
Ninaamini katika kila nilichofanikiwa kujua, nimeliona kusudi jema lake.

Kusudi kiingereza wanasema purpose, kitu mithili ya lengo la kufanyika jambo fulani.

Hapana sijui kila jambo

Not relevant

Nitajua kwa sababu kwa nilivyofanikiwa kuvijua, imeonesha ndiyo asili ya uhalisia uliopo. Mda mwingine nilikuwa na picha mbaya ya kitu lakini baada ya muda niligundua kusudi lake. Hivyo naamini katika vile ambavyo sitafanikiwa kuvijua katika maisha haya basi nitavielewa muda fulani katika safari yangu duniani au mbinguni.

Ulimwengu huu na yaliyomo ni mzuri unaeuhusu maisha yaendelee, na maisha ni basically kutatua changamoto mbalimbali huku ukijifunza na kuwa bora zaidi.

Tungekuwa na ulimwengu huo, watu wa kulaumu mngekuja na kusema kwa nini hakutuumba tumeshiba hadi tupate taabu ya kutafuta chakula. Kwa nini hakutuumba tuna watoto na vijukuu tayari? Yaani mambo yote yanayohusisha kuishi unanuwezo wa kuyalaumu kuwa ni 'evil' ukiamua. Bottomline kukataa mabadiliko chanya ni unataka kuwa kinyume na maisha/life as we know it.
 
Yote yamejibiwa #670
 
Ona sasa Kiranga hapo demand unayoiweka ni kwamba kwa nini Mungu hakuniumba na mimi Mungu kama yeye? Utokee unajua tu kila kitu.? Halafu baada ya hapo uishi ili iweje? Hujui kama maisha yetu yote ni kumjua/kumjifunza Mungu, kumtumikia Yeye na uumbaji wake.......Sasa kila kitu kitokee hatua za mwisho halafu utakitumikiaje ili ugundue nini?

Good news ni kwamba Mungu amekuumba wewe mungu, tena wewe ni potential Mungu baada ya muda milele. Unaweza kuwa mkamilifu kama yeye alivyo mkamilifu baada ya muda milele. Ni kama umbali kutoka pointi A kwenda B [infinity distance] ambao utautembea katika njia fulani [WAY] kwa muda wote na kiukweli hautafika maana utahitaji umilele/eternity kufika. Na hicho ndiyo kinapelekea phenomenon ya maisha [LIFE] ya milele. Huo ndio ukweli wenyewe[TRUTH] ulivyo. Ukiukataa simply unakufa. DEATH means no further change and without change there is no time, and without time no existance as materialist know it.

Takwa lako la kuumbwa ukiwa tayari upo hatua ya mwisho ni ombi la kuyakataa maisha, hutaki changamoto yoyote ya kufanyia kazi. Mungu mwenyewe aliamua asikae tu ajipe kazi ya kulea uumbaji wake. Hiyo inaonesha hata kama ungeumbwa mojakwamoja level ya Mungu, maisha ndiyo the best way of existing, I mean seriously what could be the alternative?. Muige uyafurahie maisha sasa tayari umepewa. Maana Yeye anajua zaidi.

Ametupenda sisi haswaa na ametupa kile ambacho akili yake kuu ilishan'gamua kitambo na yeye mwenyewe akakipenda. Nacho ni MAISHA.
 
Nimeanza kukujibu zamani sana kwa kukupa ilmu, mpaka ikuingie. Narudia, Je, unafahamu kuwa salat kwa mujibu wa Qur'an haijaanza kwa Mtume Muhammad?
Nikikuuliza nabii Ibrahim alikua anasali vipi, sijui utanijibu nini au nabii Musa alikuwa ana sali vipi utanijibu nini ? Yaani nakuona mjinga wa kutupwa.

Kwa ufupi hujui kitu, yaani hapa mpaka unakufa hutaweza kujibu swali hili, hata kujaribu.
 
Nimekueleza na nnarudia, je, unajuwa kwa mujibu wa Qur'a sala haijaanzia kwa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam?
Unauliza swali la kijinga sana, mitume wote walikuwa wanaabudu. Swali litazidi kuwa zito kwako nikikuuliza utuelezee kwa kutumia Qur'aan walikuwa wana sali vipi, hutaweza sasa usibishane na mimi katika jambo hilo utazidi kuumia.

Baada ya hapa sitakujibu tena mpaka pale utakapo leta aya inayo tufundisha namna ya kusali.
 
Wewe kutoweza kuchagua kupaa juu bila msaada wa vifaa, na wewe kutoweza kuchagua kurudi nyuma katika muda, ni sawasawa na mtu aliyeambiwa anaweza kuchagua gari la rangi yoyote, as long as rangi hiyo ni nyeusi.

Wote mmewekewa mipaka katika mnayoweza kuchagua, na hivyo, hamuwezi kusema mko huru kuchagua mnachotaka.
 
Imani yangu ipi?

Hujajibu swali

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao utakuwa na mazuri yote ambayo yatampendeza kila mtu kwa namna yake bila uwezekano wa watu hao kukosoa chochote?
 
Unachoamini hujui, na unachojua huamini.

Unaelewa hilo.

Kama hujui kila jambo, unajuaje kila jambo lina kusudi?

Unajuaje wewe uelewa wako unatosha kukupa picha yote ya ulimwengu, hususan kama ushakubali hujui yote?

Ulimwengu huu ni mzuri kwa sababu unaruhusu maisha yaendelee? Unajua kwamba ulimwengu huu hauruhusu maisha yaendelee bila tabu sana na kwa kuangalia the second law of thermodynamics maisha yote yatakufa na kutoweka? Ulimwengu huu unaruhusu maisha au unakatisha maisha?

Mungu wako muweza yote alishindwa kuumba ulimwengu mzui, ambao watu hawana lawama ujinga, njaa wala lawama?
 
Kwanza kabisa, unaelewa kwamba mimi siweki demand yangu yoyote, naangalia tu logical consistency ya dhana ya kuwapo kwa mungu wako?

Unaelewa kwamba dhana ya kuwapo kwa Mungu wako haina logical consistency?
 
Shida imeanzia hapo kwenye kuamini vitu vyenye utata bado.

Shida ikakomaa zaidi pale unapojaribu KUPERSONALIZE kile kiitwacho Mungu, kwa hoja kwamba ana Hiki ama Kile, yupo hivi ama vile.

Futa hiyo dhana kwanza kichwani mwako, aanza upya. Jitazame upya ukijihusianisha na kila kinachokuzunguka, Utakachokiona ndio Ukweli unaopaswa kuuishi.

Mengi ni Viini Macho hakika.
 
Nikikuuliza nabii Ibrahim alikua anasali vipi, sijui utanijibu nini au nabii Musa alikuwa ana sali vipi utanijibu nini ? Yaani nakuona mjinga wa kutupwa.

Kwa ufupi hujui kitu, yaani hapa mpaka unakufa hutaweza kujibu swali hili, hata kujaribu.
Kwanza umekubali au umekataa kuwa kwa mujibu wa Qur'an Salaa imeanza kwa Nabii Ibrahim?

Jibu la swali langu hilo ndilo linakufanya uendelee kuogopa, leo ndio utajulikana u Muislam au Mnafiki.

Yesu, alayhi salaam, ni Muislam.
 
Kwanini ukifa unaliliwa na watu kuhuzunika?
Kwanini ukitenda mema unafurahi na wengi wanafurahi?

Nini chanzo cha mauti.
Kwanini Mungu alituumba tujue mema pekee.

Leo ukiambiwa kuchagua uzima na mauti, mema na mabaya, baraka na laana utachagua nini?

Kwanini Mungu alituumba tuishi tukijua upande mmoja wa shilingi na si upande wa pili?
 
Kwanza umekubali au umekataa kuwa kwa mujibu wa Qur'an Salaa imeanza kwa Nabii Ibrahim?
Hili mpaka utupe ushahidi toka kwenye Qur'aan kwamba Sala imeanza kwa nabii Ibrahiim.
Jibu la swali langu hilo ndilo linakufanya uendelee kuogopa, leo ndio utajulikana u Muislam au Mnafiki.

Yesu, alayhi salaam, ni Muislam.
Swali nililo kuuliza mpaka unakufa huwezi kulijibu.
 
Imani yangu ipi?

Hujajibu swali

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao utakuwa na mazuri yote ambayo yatampendeza kila mtu kwa namna yake bila uwezekano wa watu hao kukosoa chochote?
Imani kwa ilivyotumika ni muunganiko wa uhalisia kuhusu ukweli wa jambo/mambo ulivyo kama mtu binafsi anavyoona mwenyewe. Imani ni binafsi unaijua mwenyewe imani yako.

Kama ndicho unachokitaka basi amini kwamba ulimwengu huu uliopo ndio huo unaoutamani, ni suala la muda tu.

Ulimwengu tulionao unayo mazuri yote yanayompendeza kila mtu kwa namna yake katika dunia/[uhalisia] wake, hakuna uwezekano wa watu kukosoa chochote katika uhalisia wao. Bali watakosoa vitu vingine tu katika uhalisia wa wenzao walio katika dunia nyingine.

Natumai sasa nimejibu tena, najua nishajibu zaidi ya mara moja.
 
Tupo huru kwa yale tunayopaswa kuwa huru nayo, na ipo mipaka kwa yale tusiyohitajika kuyafanya kadiri ya maisha yetu duniani yanavyotupasa. Kama ambavyo mtu wako yupo huru kuchagua rangi za magari kadri ya rangi zilizopo za magari. Asijitungie tu nataka gari la rangi 'transparent. au urujuani au udhurungi rangi ambazo hata haziwekwagi kwenye magari!! ni fujo tu za huyo mtu anataka kuonesha umemfungia machaguo.

Nakubali kuna mipaka, na hilo halinifanyi kujihisi siko huru - nipo huru ndani ya mipaka hiyo. Ninautumia uhuru wangu kuchagua[kwa mambo yanayopaswa kuchaguliwa], kumtii na kuitii na kuiheshimu mipaka yake.

Ninamuamini aliyeweka mipaka ya kuwa ana lengo zuri na sisi hivyo ninaifurahia hadi hiyo mipaka yenyewe naipenda.
 
Hapana: Labda kusaidiana tutumie kiingereza. In English we have, belief, faith,and trust. Those are arranged in order of knowingness involved. There is almost no knowledge in belief, there is balanced known and unknown in faith[but you have full trust anyway], and almost full knowledge in things you trust. Kwa kiswahili tuna neno moja tu imani basi. Hence unaweza kukijua unachokiamini kwa kizungu wanaita trust.

Ujuzi na imani[faith] vinahusika kujua kila jambo lina kusudi.

Uelewa wangu hautoshi, mimi na wengine wote hata wewe tunategemea pia ufunuo ili kuipata picha kamili zaidi ya ulimwengu na sio uelewa kama uelewa pekee.

Second law of ther........ brother hii material universe unayoiona ni hatua tu ni kama mageuko ya kipepeo. Purely materialist kuelewa hilo labda chukulia metamofosisi za kipepeo. Kutoka lifunza [caterpillar] kula majani, na kutembelea tumbo ardhini na mtini tu[kuelekea kushoto au kulia tu] kufa kuwekwa kwenye jeneza[buu] hadi kuwa kakipepeo kufyonza nekta tamu na kupaa angani[kuelekea kushoto, kulia, juu, chini, kujongea kushoto-chini, kushoto-juu, kulia-chini na kulia juu au ku hover palepale maybe!] kuvuka mito na kuishi popote na kuvinjari almost msitu wote. Watu wanaoamini uwepo zaidi ya material wala hawatishwi na mabadiliko madogomadogo ya kiumbo ikijumuisha kifo cha maada wanafahamu kuwa yajayo yanafurahisha zaidi, na yana uhuru zaidi.

Aliweza na ndio huu ulimwengu niliopo wenye maisha, mzuri na hauna lawama. Ila ujinga unao ili tuendelee kujifunza, na njaa unayo ili tuendelee kujishibisha. Kiufupi unaruhusu MAISHA. Karibu pia huku, ukipenda
 
Kwanza kabisa, unaelewa kwamba mimi siweki demand yangu yoyote, naangalia tu logical consistency ya dhana ya kuwapo kwa mungu wako?

Unaelewa kwamba dhana ya kuwapo kwa Mungu wako haina logical consistency?
Okay sawa

Dhana ya kuwapo Mungu ni logical na ni consistent kwa premise ya/za upande huu. Sio logical wala sio consinstent katika premise yako/zako. Mfano wa premise zinazotrendi huku ni To every thing there is a season, and a time to every purpose under the heaven - Ecclesiastes. Everything have a purpose broh, a very good one just trust the process.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…