Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Sasa tofauti ya huyo na wewe kudai una freewill wakati hauwezi kurudi nyuma katika muda ni nini?Hapo hajapewa uchaguzi katika rangi. Katika rangi hajapewa freewill.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa tofauti ya huyo na wewe kudai una freewill wakati hauwezi kurudi nyuma katika muda ni nini?Hapo hajapewa uchaguzi katika rangi. Katika rangi hajapewa freewill.
Hujaeleza ulimwengu uliopo unathibitisha vipi Mungu yupo.Upo na kusudi fulani. Hivyo ukijumlisha ukagawanya vyoote unakuta ni vyema vina kusudi jema.
Hata hivyo unavyowaza vingeondolewa kwamba viovu, kwamba vibaya havifai - Jua katika akili kubwa ni vyema. Hata mimi sijidai kwamba naelewa hivyo ila nina imani[trust] kwa Mungu ambaye ni Mwema kila wakati.
Sasa tofauti ya huyo anayedai mpaka kuwepo gari ya rangi ya udhurungi ndiyo aseme amechagua rangi. Na wewe unayetaka mpaka urudi nyuma ya mda kwamba ndio ukohuru kutumia will yako na muda wako ni ipi?Sasa tofauti ya huyo na wewe kudai una freewill wakati hauwezi kurudi nyuma katika muda ni nini?
Ninaamini katika kila nilichofanikiwa kujua, nimeliona kusudi jema lake.Unajuaje kwamba kuna kusudi kwa kila jambo?
Kusudi maana yake ni nini?
Wewe unajua kila jambo?
Kama unajua kila jambo, unajuaje?
Kama hujui, utajuaje kwamba kuna kusudi kwa kila jambo?
Kwa nini freewill ni muhimu kuliko kuumba ulimwengu ambao watoto hawawezi kufa kwa kukosa lishe?
Kwani Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu wana freewill lakini pia watoto hawafi kwa kukosa lishe?
Yote yamejibiwa #670Hujaeleza ulimwengu uliopo unathibitisha vipi Mungu yupo.
Unaeleza imani yako tu, ambayo si lazima iwe kwenye ukweli.
Na hata hiyo imani yako, kwamba ulimwengu upo kwa kusudi fiulani, huwezi kuithibitisha.
Na hata hilo neno "kusudi" hujalinyambulisha kutueleza ukiongelea "kusudi" unamaanisha nini.
Ona sasa Kiranga hapo demand unayoiweka ni kwamba kwa nini Mungu hakuniumba na mimi Mungu kama yeye? Utokee unajua tu kila kitu.? Halafu baada ya hapo uishi ili iweje? Hujui kama maisha yetu yote ni kumjua/kumjifunza Mungu, kumtumikia Yeye na uumbaji wake.......Sasa kila kitu kitokee hatua za mwisho halafu utakitumikiaje ili ugundue nini?Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna ujinga, watu wote wana uelew mzuri kuhusu uwepo wake, na kila kitu, bila mapungufu?
Kama aliweza, na ana uwezo wote ujuzi wote na upendo wote, kwa nini hakuumba hivyo?
Yeye ni mchoyo wa kuwapa watu elimu na raha?
Kama hakuweza, je, yeye ni Mungu muweza yote kweli?
Nikikuuliza nabii Ibrahim alikua anasali vipi, sijui utanijibu nini au nabii Musa alikuwa ana sali vipi utanijibu nini ? Yaani nakuona mjinga wa kutupwa.Nimeanza kukujibu zamani sana kwa kukupa ilmu, mpaka ikuingie. Narudia, Je, unafahamu kuwa salat kwa mujibu wa Qur'an haijaanza kwa Mtume Muhammad?
Unauliza swali la kijinga sana, mitume wote walikuwa wanaabudu. Swali litazidi kuwa zito kwako nikikuuliza utuelezee kwa kutumia Qur'aan walikuwa wana sali vipi, hutaweza sasa usibishane na mimi katika jambo hilo utazidi kuumia.Nimekueleza na nnarudia, je, unajuwa kwa mujibu wa Qur'a sala haijaanzia kwa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam?
Wewe kutoweza kuchagua kupaa juu bila msaada wa vifaa, na wewe kutoweza kuchagua kurudi nyuma katika muda, ni sawasawa na mtu aliyeambiwa anaweza kuchagua gari la rangi yoyote, as long as rangi hiyo ni nyeusi.Sasa tofauti ya huyo anayedai mpaka kuwepo gari ya rangi ya udhurungi ndiyo aseme amechagua rangi. Na wewe unayetaka mpaka urudi nyuma ya mda kwamba ndio ukohuru kutumia will yako na muda wako ni ipi?
Machaguo uliyonayo katika kuutumia muda wako ni huru kabisa kadiri ya mambo unayohitajika kuyachagua katika muda duniani. Uko huru
Imani yangu ipi?Unaona? hapa ni wewe mwenyewe unataka kutokuwepo na unaona ni sahihi kabisa! sasa ni kwa nini usipokee sambamba na imani yako? Unataka dunia ambayo haina critic na hapo upo, the critic mwenyewe!! serious. Anza wewe mwenyewe kwa kuamua kutokuwa critic na hapohapo dunia nzima itachange na utaishi critic-free-earth papo kwa hapo. Amua kuyaona mema ya dunia na kufumba na kufumbua dunia yako nzima itakuwa njema!!
Mungu anatupenda na anatupatia sambamba na tunachokitaka huo ndio upendo. Dfn ya mdogo angu alisema kuna power na kuna will. Power ni uwezo wa kuifanya will yako itendeke yaani iwe. Power ndo kila kitu -Mdogo angu.
Nikamwambia kuna power, kuna will na kuna love. Power ni kama alivyoidefine yeye. Na love ni pale unapotumia power yako willingly kutekeleza will ya huyo unayempenda. It is your will that his/her will be done. Mara nyingi unam-love mtu/entity kwa kuwa unam-trust/unaitrust. Kama hakuna trust na ukatekeleza will ya mtu mwingine itabidi utumie uoga/fear. Mungu anatupenda sisi ndio maana ameamua kwa matakwa yake kuyasikiliza na kuyafanyia kazi matakwa yetu kwa nguvu zake alizonazo. Tukimpenda na sie tutaamua kwa will zetu kutekeleza will yake kwetu. Ndo maana kuna kauli MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.- Mimi
Dunia iliyopo haikufanyi kuwa critic automatically, bali unaamua wewe kuwa critic au vipi ni wewe kama wewe. Na Mungu kwa upendo anakuacha uishi kikamilifu mlolongo mzima wa matukio katika huo mnyororo wa fikara - FreeWILL
Mbona imewezekana katika dunia hii hii nikawepo mimi [trusting people] na ukawepo wewe [sceptic,critic people]. Naamini ni matokeo ya tulivyoamua kuitazama dunia hiihii na kujiumbia uhalisia tofauti. Kila mmoja atauishi ulimwengu anaouona ni sahihi. Aliyechagua maisha ataishi, na aliyechagua kifo atakufa. Ni mapenzi yake, ni will yake mtu binafsi na Mungu Baba kwa upendo wake anatupatia sambamba na chaguzi zetu. LOVE & FREE-WILL
Unachoamini hujui, na unachojua huamini.Ninaamini katika kila nilichofanikiwa kujua, nimeliona kusudi jema lake.
Kusudi kiingereza wanasema purpose, kitu mithili ya lengo la kufanyika jambo fulani.
Hapana sijui kila jambo
Not relevant
Nitajua kwa sababu kwa nilivyofanikiwa kuvijua, imeonesha ndiyo asili ya uhalisia uliopo. Mda mwingine nilikuwa na picha mbaya ya kitu lakini baada ya muda niligundua kusudi lake. Hivyo naamini katika vile ambavyo sitafanikiwa kuvijua katika maisha haya basi nitavielewa muda fulani katika safari yangu duniani au mbinguni.
Ulimwengu huu na yaliyomo ni mzuri unaeuhusu maisha yaendelee, na maisha ni basically kutatua changamoto mbalimbali huku ukijifunza na kuwa bora zaidi.
Tungekuwa na ulimwengu huo, watu wa kulaumu mngekuja na kusema kwa nini hakutuumba tumeshiba hadi tupate taabu ya kutafuta chakula. Kwa nini hakutuumba tuna watoto na vijukuu tayari? Yaani mambo yote yanayohusisha kuishi unanuwezo wa kuyalaumu kuwa ni 'evil' ukiamua. Bottomline kukataa mabadiliko chanya ni unataka kuwa kinyume na maisha/life as we know it.
Kwanza kabisa, unaelewa kwamba mimi siweki demand yangu yoyote, naangalia tu logical consistency ya dhana ya kuwapo kwa mungu wako?Ona sasa Kiranga hapo demand unayoiweka ni kwamba kwa nini Mungu hakuniumba na mimi Mungu kama yeye? Utokee unajua tu kila kitu.? Halafu baada ya hapo uishi ili iweje? Hujui kama maisha yetu yote ni kumjua/kumjifunza Mungu, kumtumikia Yeye na uumbaji wake.......Sasa kila kitu kitokee hatua za mwisho halafu utakitumikiaje ili ugundue nini?
Good news ni kwamba Mungu amekuumba wewe mungu, tena wewe ni potential Mungu baada ya muda milele. Unaweza kuwa mkamilifu kama yeye alivyo mkamilifu baada ya muda milele. Ni kama umbali kutoka pointi A kwenda B [infinity distance] ambao utautembea katika njia fulani [WAY] kwa muda wote na kiukweli hautafika maana utahitaji umilele/eternity kufika. Na hicho ndiyo kinapelekea phenomenon ya maisha [LIFE] ya milele. Huo ndio ukweli wenyewe[TRUTH] ulivyo. Ukiukataa simply unakufa. DEATH means no further change and without change there is no time, and without time no existance as materialist know it.
Takwa lako la kuumbwa ukiwa tayari upo hatua ya mwisho ni ombi la kuyakataa maisha, hutaki changamoto yoyote ya kufanyia kazi. Mungu mwenyewe aliamua asikae tu ajipe kazi ya kulea uumbaji wake. Hiyo inaonesha hata kama ungeumbwa mojakwamoja level ya Mungu, maisha ndiyo the best way of existing, I mean seriously what could be the alternative?. Muige uyafurahie maisha sasa tayari umepewa. Maana Yeye anajua zaidi.
Ametupenda sisi haswaa na ametupa kile ambacho akili yake kuu ilishan'gamua kitambo na yeye mwenyewe akakipenda. Nacho ni MAISHA.
Shida imeanzia hapo kwenye kuamini vitu vyenye utata bado.Hello y’all..
NB: Naomba moderator mada hii msiihamishie jukwaa la dini maana huko itakosa wachangiaji na lengo langu la kutaka kujuzwa jambo hili halitatimia and that will leave me frustrated and bums me out, Natuamaini mtatii takwa langu hili. Ahsanteni.
Binafsi kiimani ni muumini wa kanisa Katoliki kwa kuzaliwa na kubatizwa, pia ninaamini na kuisadiki kanuni ya imani yangu katoliki isemayo “Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu Bwana wetuu….” Self-schemas: katika sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Self-Concept ni i hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future self (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo). Toka nilipoanza kutambua Self Concept yangu Nimekua na swali ambalo kwakweli pamoja na kuisadiki imani yangu hii na kupokea ya Sakrament takatifu ya Communion swali hilo limekua mwiba mchungu na kikwazo kikubwa katika imani yangu hii na Mungu kwa ujumla.
Toka nilipoanza kujitambua nimejaribu kuwashirikisha watu wenye uelewa jambo hili ila bado sijapewa majibu thabiti….natumaini hapa JF nitapewa maelekezo vyema , mnivumilie kama maelezo yatakua marefu maana hua siwezi kuelezea kwa ufupi but it worth your time.
The One above all, In-Betweener and The One bellow all.
Monotheism ni imani ya kua kuna Mungu mmoja pekee ambae aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Watu wanao amini katika imani hii ni wafuasi wa dini zilizotokana na Ibrahim ambae anachukuliwa kama baba wa imani ambazo ni Judaism, Ukristo,uislam, mandaeism ,Rastafarian na Bahai. Mungu wa imani hii ndio huyu tunayemfahamu mimi na wewe ambae ana sifa kuu tatu ambazo ni yupo kila mahali, anajua kila kitu, na anaweza kila kitu. Omni ni neno la kilatini lenye maana ya yote au kila kitu na Sciens ni neno la kilatini likimaanisha kujua(conscious)……. Moja kati ya sifa kuu tatu za Mungu nilizotaja hapo juu ni Omniscience ikimaanisha kwamba Mungu anajua yote yaliyopita,yaliyopo na yajayo.
The Great Chain of Being ni mchoro au nadharia ambayo inaonyesha kwamba maisha ya mwanadamu yapo kwenye ngazi /mtiririko Fulani ambapo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,mimea halafu chini kabisa yupo shetani. Mungu ni the one above all, mwanadamu ni aliyekati /in-betweener na shetani ni the one below all. Unajua mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote walioumbwa na mungu kuzidi hata malaika ndio maana kuna malaika wanafanya kazi kwa wanadamu ya kutulind, Moja kati ya utajiri na kitu kikubwa alichonacho mwanadamu hakuna kiumbe kingine anacho ni uwezo wa kuchagua na kuamua Kuishi vile atakavyo yeye yaani Free Will….Katika Great chain of being mwanadamu amewekwa katikati (In-Betweener) maana yeye ameumbwa na roho isiyokufa (immortal) na mwili ambao unaokufa (mortal) hivyo inamuwezesha yeye kuishi duniani au mbinguni . Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi Uungu kwa kutenda mema maishani mwake au ushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Kwakua mwanadamu ana free will uamuzi ni wake ni kuchagua kwenda kwa The One above all au kwa the one bellow all.
Free Will is illusion (?)
Kuna mada Fulani niliwahi kusema kwamba tukio la kuumbwa Adam na eva hadi kufukuzwa eden linapinga uwepo wa Mungu kwa kupinga sifa tatu alizonazo Mungu kwamba anaweza yote,anajua kila kitu na yupo kila mahali… ndio maana mimi hua nalichukulia kama lugha ya picha tu na sio tukio halisi na kama kweli ni kweli lilitokea kama lilivyoelezewa kwenye kitabu cha mwanzo basi linaonyesha Mungu hafai kupokea sifa tunazompa. Kama anajua kila kitu je wakati anamuumba adamu bila Eva hakujua kwamba adamu hatapata uhitaji wa kua na mwenza? Yupo kila mahali jewakati adam na eva wamekula tunda hakuwepo pale walipojificha hadi aanze kuuliza wako wapi? Alikua hajajua juu ya tukio la adam kula tunda maana lilimuudhi kwelikweli like he didn’t know a thing from a first place.
Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?
Kuna phrase protestant wanapenda kusema kwamba sisi wakatoliki hatujui kusoma na kuielewa biblia, naamini name ni mmoja wapo nisiojua kusoma biblia. Hivyo basi napenda kuwaalika wale wote wenye uelewa juu ya jambo hili. Naombeni mnijuze kama Mungu anajua hatima yangu na hukumu yangu siki ya mwisho na kama anajua je naweza kubadirisha? Kama mchezo kautengeneza yeye na sharia za mchezo kazitengeneza yeye je wachezaji wanawezaje kua huru?
Vinjii…
Kwanza umekubali au umekataa kuwa kwa mujibu wa Qur'an Salaa imeanza kwa Nabii Ibrahim?Nikikuuliza nabii Ibrahim alikua anasali vipi, sijui utanijibu nini au nabii Musa alikuwa ana sali vipi utanijibu nini ? Yaani nakuona mjinga wa kutupwa.
Kwa ufupi hujui kitu, yaani hapa mpaka unakufa hutaweza kujibu swali hili, hata kujaribu.
Kwanini ukifa unaliliwa na watu kuhuzunika?Freewill ni uhuru wa kuchagua mema na mabaya
Na wanasema kwamba bila freewill watu watakuwa kama marobot
At least mushukuru shetani basi
Yes naswma shetani kwakua yeye ndio aliowapa hiyo knowledge ambayo Mungu hakutaka watu wawe nayo
Katika bustani ya eden kina adam na eve walikuwa hawana utambuzi wa kujua lipi jema lipi baya, mpaka pale shetani alipowashawishi walw tunda la utambuzi wa mema na mabaya
Tunda ambalo Mungu hakutaka watu hao wale, kwa tafsiri fupi ni kuwa Mungu hakutaka watu wawe na utashi huru alitaka kuwatenganisha na ukweli.
Na ndio maana kwa miaka mingi walikuwa uchi ila hawakuwahi kustuka ila walipopata maarifa kupitia lile tunda ndio wakagundua kuwa wako uchi.
Lakini pamoja na hayo yote bado watu wanamchukia shetani, lakini ukianza ku count mabaya ya shetani au ukatiri wa shetani sidhani kama utaishia kumuona shetani kafanya ukatiri kumzidi Mungu.
Hili mpaka utupe ushahidi toka kwenye Qur'aan kwamba Sala imeanza kwa nabii Ibrahiim.Kwanza umekubali au umekataa kuwa kwa mujibu wa Qur'an Salaa imeanza kwa Nabii Ibrahim?
Swali nililo kuuliza mpaka unakufa huwezi kulijibu.Jibu la swali langu hilo ndilo linakufanya uendelee kuogopa, leo ndio utajulikana u Muislam au Mnafiki.
Yesu, alayhi salaam, ni Muislam.
Imani kwa ilivyotumika ni muunganiko wa uhalisia kuhusu ukweli wa jambo/mambo ulivyo kama mtu binafsi anavyoona mwenyewe. Imani ni binafsi unaijua mwenyewe imani yako.Imani yangu ipi?
Hujajibu swali
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao utakuwa na mazuri yote ambayo yatampendeza kila mtu kwa namna yake bila uwezekano wa watu hao kukosoa chochote?
Tupo huru kwa yale tunayopaswa kuwa huru nayo, na ipo mipaka kwa yale tusiyohitajika kuyafanya kadiri ya maisha yetu duniani yanavyotupasa. Kama ambavyo mtu wako yupo huru kuchagua rangi za magari kadri ya rangi zilizopo za magari. Asijitungie tu nataka gari la rangi 'transparent. au urujuani au udhurungi rangi ambazo hata haziwekwagi kwenye magari!! ni fujo tu za huyo mtu anataka kuonesha umemfungia machaguo.Wewe kutoweza kuchagua kupaa juu bila msaada wa vifaa, na wewe kutoweza kuchagua kurudi nyuma katika muda, ni sawasawa na mtu aliyeambiwa anaweza kuchagua gari la rangi yoyote, as long as rangi hiyo ni nyeusi.
Wote mmewekewa mipaka katika mnayoweza kuchagua, na hivyo, hamuwezi kusema mko huru kuchagua mnachotaka.
Hapana: Labda kusaidiana tutumie kiingereza. In English we have, belief, faith,and trust. Those are arranged in order of knowingness involved. There is almost no knowledge in belief, there is balanced known and unknown in faith[but you have full trust anyway], and almost full knowledge in things you trust. Kwa kiswahili tuna neno moja tu imani basi. Hence unaweza kukijua unachokiamini kwa kizungu wanaita trust.Unachoamini hujui, na unachojua huamini.
Unaelewa hilo.
Kama hujui kila jambo, unajuaje kila jambo lina kusudi?
Unajuaje wewe uelewa wako unatosha kukupa picha yote ya ulimwengu, hususan kama ushakubali hujui yote?
Ulimwengu huu ni mzuri kwa sababu unaruhusu maisha yaendelee? Unajua kwamba ulimwengu huu hauruhusu maisha yaendelee bila tabu sana na kwa kuangalia the second law of thermodynamics maisha yote yatakufa na kutoweka? Ulimwengu huu unaruhusu maisha au unakatisha maisha?
Mungu wako muweza yote alishindwa kuumba ulimwengu mzui, ambao watu hawana lawama ujinga, njaa wala lawama?
Okay sawaKwanza kabisa, unaelewa kwamba mimi siweki demand yangu yoyote, naangalia tu logical consistency ya dhana ya kuwapo kwa mungu wako?
Unaelewa kwamba dhana ya kuwapo kwa Mungu wako haina logical consistency?