Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mungu wako katengenezwa kwa a priori fallacy kwamba yupo.Anhaa, umepata taabu kwa sababu moja tu ya kuweka kama Mungu ako anachukia uovu yaani angeweza angeufuta tu usiwepo kwa waja wake. Wrong.
Kwa kuanzia tujue kwamba mpaka sasa concept/taswira/picha ya Mungu tuliyofikia ni upendo na uwezo usio na kikomo, na ujuzi usio na kikomo. Ukicontrast na sie, mimi na wewe tuna ukomo katika hayo mambo yote.
Unapokaa wewe na Kiranga halafu mkajiona kuwa mna akili sana naujuzi wote kiasi kwamba mnajua kuwa uovu ni mbaya for all intents and purpose mkaona mko sahihi kuliko Mungu mnajidanganya. Yeye anajua zaidi.
Mimi na nyie wote ni watoto, katika utoto wetu tunaweza kukubaliana kabisa kwamba viboko havifai, na baba anapaswa kutupatia kila kitu, na atupe sasa hivi [no delay] tukaona ni sahihi tunajidanganya. Ndiyo naweza nikaungana na nyie kwamba uovu ni kitu kibaya kwa mwisho wa utashi wetukwa sasa. Lakini nikifikiri hata hili suala la muda, kutuwekea kwamba tunaexperience mambo fulani kulingana na muda kadri tunavyokua naamini yu sahihi. I trust HIM
Maswali yenu yanaonesha hampendi kukua, hampendi hata kuishi sasa as a result. Maana yake maisha yanajumuisha kila siku kukua na kupata experience mpya na kupambana na vichangamoto vidogovidogo vinavyotaka kutusambaratisha. Sasa imagine unatokea na kila kitu then unaishi ili iweje. Kwa kweli kuweka muda ni akili kuu ya Mwenyewe. Mungu fundi😊💪, asante sana.
Ukiiondoa hiyo a priori fallacy kwamba yupo, useme hujui kwamba yupo au hayupo, halafu ukataka ku prove yupo, logically, huwezi ku prove kwamba yupo.
Kwa sababu hayupo.