Nimekupata vizuri sana, na nimeielewa hiyo paradox uliyoitengeneza. Inavunjika tukija kwenye tafsiri ya Mungu. Kwenye definition yake. Anayeweza kutengeneza paradox ya hivyo ni tu aliyekana Mungu pekee. Kwa hiyo hilo ni tatizo la huko kwenu tu sio kwetu. Kwetu first cause nndiyo Mungu.
Nikijaribu kuingia huko kwenye logic za kwenu japo sidhani kama itakuwa ya kujitosheleza. Naomba niseme kuwa kila jambo material lina sababu. Kuna vingine ambavyo tunasema ni being hivyo ni vipo sema kuna muda unaweza kukuta unachanganyikiwa kimawazo kwamba uanzie chini au uanzie juu, mwanzo au mwisho? Labda ni duara who knows?
God is at the centre and circumference thereof and everything in between, up above down below and everywhere!.
Nahisi unaruhusiwa kuwa na wazo la namna inayokupeleka kuunda set/au maduara ya Mungu kama wakristu/walokole walio wengi walivyofanya.
Tuseme kwamba ulimwengu wote huu upo ndani ya Kristu naye Kristu yu ndani yake. Na sisi ndani ya Kristu na Kristu ndani yetu - Mwana wa Mungu na Mungu with respect to us/kwa mtazamo wa sisi viumbe wadooooogo. Mungu ni muumba na kwa kuwa ulimwengu huu tunaoujua [upo na tusioweza kuujua kwa sasa] sisi wote umeumbwa na Kristu/Neno basi Yesu ni Mungu kabisa kwetu. Hata kama tutasema hivyo haimpunguzii utukufu Mungu Baba aliyemtuma. In fact tunamtukuza Baba katika Mwana. Tunaamini Mungu ni mmoja tu Ndiye chanzo cha wote, na ndiye wote pia. Mkuu
draga ana concept kali zaidi kwa hii phenomenon mcheki.
Lakini ukipanda juu unakuta huyo Mwana wa Mungu yumo ndani ya Mungu tena na Mungu yumo ndani yake. Kwa hiyo Kristu anavyomuona Mungu inakuwa tena ni hivyohivyo ambavyo sisiwanadamu/walokole tunamuona Kristu.
Kwa hiyo sababu ya kuwepo Kristu ni Mungu Baba na inatosha kwa sasa maana ili tuje kuielewa sababu ya Mungu Baba itatubidi labda tungekuwa Kristu sisi wenyewe. Itoshe kusema tunahitaji umilele kuelewa jinsi kikamilifu mambo yalivyo. Elewa tu kwamba kama ambavyo sisi ni sehemu ya Kristu na kiotomati ni sehemu ya Mungu naye Mungu ni ndani ya Kristu kiotomati ndani ya sisi basi unaweza kuta hili ni duara lisilo na mwisho hakuna cha cause wala effect hapa na hapohapo tena kuna cause na effect!!. Unakumbuka nilikuambiaga quantum physics ni sehemu ya msahafu tu kwa anayeongozwa na Roho?
Kama wewe Kiranga huwezi kuishi bila sababu au unaweza kuishi na sababu [either way] basi tumia hiyo kwa kuanzia, muamini Yesu aliyetumwa na Baba yake halafu kadri unavyokua utazidi kuelewa zaidi sababu na kusudi. Ila stay assured tu kwamba kimsingi wao ni Mmoja hadi sisi huku tu sehemu yake. Taz. picha
Naona post imekuwa ndefu kama uzi, basi kama ilivyo ada isindikizwe na kapicha:
KEY: Maelfu ya seli ndio kama sisi hapa.
View attachment 2252445