Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,528
- 3,352
Alama za uwepo wa Mungu zipo kila sehemu ila kwa viziwi, vipofu na mabubu hawawezi kuzisikia,kuona wala kuzisema. Pole sana.!!Haya ni mahubiri.
Hujathibitisha Mungu yupo.
Sasa hivi usiku umeingia kabla hapo ulikuwepo mchana...ni ishara gani zaidi ya hiyo unaitaka kujua kuwa aliyeviumba hivi yupo?
Hii ardhi unayoikanyaga na kutembea kwa jeuri, unadhani imetokea tu spontaneously pasi na kuumbwa?
Hiyo pumzi unayojivunia nayo na kwa kiburi unajitamba kuwa hakuna Mungu , je umeitengeneza wewe!!??
Huoni usiku unapoingia unalala na asubuhi unaamka. Je ni nani anaekutoa katika mauti ya usingizi usiku na kukuhuisha tena asubuhi??
Huzioni ishara za uwepo wa Mungu ndani ya nafsi yako au ni jeuri na kibri ndio vimekujaa kijana??
Quran 15:3
ALLAH anasema
"Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua."
Siku utakapokuja kujua utakuwa umeshachelewa sana na kwa hakika utakuja kuyakumbuka haya maneno yangu.
ALLAH anasema tena
Quran 6:158
"Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja"