Going Bongo: Filamu ya kwanza ya Tanzania kukubalika Kimataifa

Going Bongo: Filamu ya kwanza ya Tanzania kukubalika Kimataifa

Mie nikitaka kuangalia comedy zipo zenye akili, sio vichekesho vya kipuuzi visivyo stimulate ufahamu. Kina wayn brothers, kevin hart, sinbad, desiree murch, tyler perry na wengineo. Wenzetu kenya wana eric omondi, walau he makes political jokes and football that i can relate to.

Hebu wacheki hao jamaa uone vichekesho vyenye akili. Kuna mnaijeria simkumbuki, nae niliona akiongelea how africans get killed in a movie nikacheka sana.

mkuu umemsahau Kijana wetu KINYAMBE
 
I bet iwe kali kama asemavyo promoter maana movie zetu zinaboa mpaka basi. Nahisi ningekuwa director wa movie wasanii wabongo wangenichukia na nasikitika Siwezi ingia kwenye hiyo industry coz aina ya kazi nazofanya. Sababu kwa nini zinaboa
1. Movie masaa matatu/manne story ni moja tu
2. You can easily predict the end no surprises
3. Mtu unaweza ukatoka dk 5 ukarudi na ukawa hujapitwa na kitu (wanatongozana baharini more than 20minutes)
4. They are very slow unasinzia unaamka still you can connect the dots (halafu naona kwenye YouTube Watu wanasifia uwongo mtupu)
5. Zinakosa uhalisia hasa katika maongezi (watu hawatumii Sauti zao wanabana pua wanajivuuuuta kuongea. These people are imitating and not acting. Tunahitaji actors not imitators kama unakunywa juisi ipige kama vile unavyoipigaga ukiwa off camera sio unaitemeatemea mate

Huwa najiuliza hivi huwa hawaangalii movie za nje (not nigeria maana najua huko ndo wanapokopi)? Hawana role model ambao wanawish wangefikia kam yeye? Misichana iliyojazana kwenye movie haiujui kazi yenyewe ni kushindana kuvaa tu na kukaa kaa uchi, tunataka kazi hatutaki mipaja nje.

Jaribuni kuchanganya stories, kama mtu anatongozwa baharini basi isiwe kitendo ni cha kutongozana tu onesheni na jambo lingine linatokea unexpectedly mfano x wake anapita, au anakuwa poisoned si hatujui ni nani later mnatulink na aliyempoison yaani unanifanya nisubirie kujua ni nini kilitokea hata kama anagongwa na gari si lazima mtuonyeshe mtu alimgonga ni nani at instant badae unatupa background kama wewe unataka bring changes nadhani unanielewa. Wafanye watazamaji waumize kichwa kujua.

Oooh pia umesema tussaport nakubali ila unatakiwa uelewe mtu hanunui movie kwa sababu aliyecheza ni mtanzania Bali ni quality ya movie. Unatakiwa utengeneze movies Watu mtaani wanaziongelea midomoni mwao soko utaona hiloooo linapanda of coz plus promotion.

Daaaah mtu anaangalia movie unaonyeshwa nyumbani na ofisini tu masaa matatu kweli jamani!!!!! Na nyumbani ni story ya kumdate house girl throught inaishia kufumwa na mkewe. Ofisini no story iliyoandaliwa so ni Kusign file na kumuwaza house girl full stop kweli jamani halafu unataka tussaport. Sasa hapo unaniconvice vipi nitoe $9 kwa mfano.
 
Bawawi umemaliza, wakifuata haya maneno nadhani watapiga hatua kubwa sana. IQ yako safi sana Tz inahitaji watu kama wewe ili itoke kwenye umasikini wa kujitakia.
 
MTOTO WA KUKU nategemea input zako hapa maana kweli yanahitajika mapinduzi ya kweli......hii tabia ya kubeba mamiss wawe waigizaji bila kupata mafunzo ya kutosha na muongozo wa karibu imefanya wengine tuzisusie kazi zenu....hii going to Bongo inaanza kushawishi improvement ya ubora wa kazi zenu.......pongeza wenzako kidogo bana.......
 
Last edited by a moderator:
Mngejitahidi kuboresha waigizaji kwanza. Tatizo la waigizaji wetu halina tofauti sana na la wanahabari wetu. Hizo zimekuwa fields za failures. Ukiangalia waigizaji wa marekani, na hata wakenya pia; wenzenu wameenda shule. Hata kama umesoma shule isiyo ya uigizaji inakuweka akili sawa. Nyie uigizaji ni factor ya weupe na hips. Scripts pia haziko original kivile.

kila la kheri, mie nilishagoma kuangalia both nigerian and bongo movies, naona zinanidumaza tu akili

Muvi za kibongo na nigeria zote zero, sio muvi ni maigizo. Wakiamua kuonesha mtu sna mawazo basi hiyo scene itachukua dakika zaidi ya tano mtu anatikisa kichwa sijui ndo tone ana uchungu sana!
 
hey Tyta. I saw your comment today. I think unaniongelea mimi. Nilifanya kazi ya utangazaji Channel5 ambayo sasa ni EATV chini ya marehemu Mutie Mengi miaka zaidi ya kumi iliyopita. Halafu nikafanya muziki kidogo chini ya jina la MC Napo. Mimi pia ni mmoja ya waandishi wa hii filamu. Asante kwa comment yako, PA1!
Hongera Sana...inaonesha Ni movie nzuri



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tunatumaini kuzindua Dar mwishoni wa mwezi wa nane. Tulikuwa tayari kufanya hivyo hata mwanzoni wa mwaka huu. Lakini Corporate Tanzania na media za Bongo kama wenyewe mnavyoelewa ni matatizo matupu. Media zinataka kushikilia "status quo", Corporate Tanzania ni cheap huwezi amini. Mtu unamletea proposal ya maana, unapitch vizuri, yuko interested halafu humpati kwenye simu. Siku ukimpata baada ya wiki tatu, anakwambia, ooh hatuna hela, lakini tunaweza kuwapa kreti za bia :A S-eek: So right now, we are organizing private equity to do so...
 
Hamna part 2. Tukipata support from you, tutashot nyingine mwanzoni wa mwaka ujao. Sasa hivi tunaandika script. Inatuchukua zaidi ya miezi 6 kuandika script ya maana. We are planning to take Tanzanian movies to another level. Level ya South Africa and maybe beyond, Inshallah!
 
Back
Top Bottom