Goli la mama, Yanga yaingiza milioni 50 kwa kodi za wananchi

Goli la mama, Yanga yaingiza milioni 50 kwa kodi za wananchi

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Rais Samia alitoa ahadi yake ya kutoa hamasa kwa timu zinazo shiriki michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu vya YangaSC, Simba SC, Coastal Union na Azam FC kila Goli moja Rais anatoa shilingi milioni 5.

Na hadi sasa Yanga SC amenufaika zaidi ya kuvuna milioni 50 katika michezo yake miwili dhidi ya Vital'O katika ushindi wa Goli 4 kwa 0 na goli 6 0 jumla Yanga amefunga magoli 10.

Ugenini Yanga ilishinda goli 4 - 20,000,000

1724522520049.png

Nyumbani Yanga imeshinda goli 6 - 30,000,000

1724543477011.png

JUMLA 50,000,000 (MILIONI 50)


PIA SOMA

- News Alert: - FT: CAFCL - Yanga SC 6-0 Vital'O | (Agg: 10-0)Preliminary Stage 2nd Leg | Azam Complex | 24.08.2024
 
Hapa ndio walipotuweza na wanagonga hapa hapa kwenye mshono.

Unahisi kinachofanyika ni kizuri tuache usimba na uyanga?
Kiukweli mkuu, mpira una mashabiki wengi sana na ushawishi ni mkubwa, mwanasiasa popote anapoona kuna ushawishi mfano muziki, filamu, mpira wa miguu na wao hupitia humo humo.

Hii maana yake ni kuongeza mvuto na ushawishi kwa waTanzania wapenda mpira, unafikiri pesa zinazotolewa shabiki kindakindaki akifika kwenye daftari la kudumu la kura atafanya nini?

No free lunch in Africa, hapa kinachonunuliwa ni nguvu ya ushawishi na kukubalika.

Lakini huko hospitali kuna raia ugonjwa unamuua kakosa milioni moja.

Tutafanya nini!!
 
Back
Top Bottom