Unataka kinanda kilekile kinachozalisha bongoflava kisitoe gospel...anyway kinachofanya muziki uitwe gospel ni ujumbe dhahiri wa mungu coz hata huyo bahati bukuku ananyimbo nyingi alizotembea kama reggae
Sent using Jamii Forums mobile app
Troublemaker,😀😀
Akutane na hip hop halafu anaambiwa hiyo nayo ni injili😜
Tufumbue macho sasa. Gospel inapimwa kwa nini?
Lazima iwepo tofauti kati ya wana wa Nuru na wana wa giza.
Lazima iwepo tofauti kati ya mziki wa injili na muziki wa dunia.
Tofauti hii ionekane kuazia dhamira ya ndani, uvaaji wa wahusika, uchezaji wao n.k
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Chachasteven, Gozbert mimi mwenyewe nilikuwa namtilia mashaka sana mara niliposikia nyimbo zake kwa mara ya kwanza, lakini wimbo huu alioutoa ndio ulithibitisha kwamba huyo hakiki sio Mtumishi, yaani sio muimbaji wa Nyimbo za Injili bali huyo ni wale wanaoitwa wasanii wa nyimbo za injili, itoshe tu kutambua na hakuna haja ya kubishana hapa, naamini hata yeye mwenyewe analijua hilo, na anashangaa anapoona kuna watu wanamtetea, Kuimba Injili inataka Mtu uwe na Wito na pia Ushuhuda, sio kujiimbia tu kwa sababu unaweza kuimba, sijajua wewe msimamo wako kiimani ni upi, yawezekana unaweza kuwa unamtetea ukifurahi kuona jinsi anavyowapoteza watu wengi watakaochagua kumfuata, lakini kama wewe unatamani kuona watu wanapewa iliyo kweli kwenye Injili nadhani tusaidiane kuwakosoa watu kama Gozbert waache mara moja kusaidia wanaoutukana Ukristo kwa sababu ya style zao za Uimbaji, nakuhakikishia asipokemewa atakuja kufanya vituko sana kwenye aina hiyo ya uenezaji wa Injili.
Aisee. Rose Muhando aliimba ameonja utamu wa yesu, mbona hatujalalamika kuona vitendo akiwa anauonja utamu kwenye video??Hatutambambua mtu kwa maneno yake bali kwa matendo...naona wengi wanampima Goodluck Gozbert kwa maneno yake!!,,,Very wrong hata Kanye West ametoa album inayomtaja Yesu ila ndani ya album kuna matendo mengi sana ambayo ni ya kufuru...Mnakumbuka mfano watoto wawili waliotumwa na baba yao kwenye biblia?,,,Mmoja alisema anaenda ila hakwenda na mwingine alisema haendi ila akaenda. Aliyetii amri ya baba yake ni yule aliyeenda alikotumwa. HATUPIMWI KWA MANENO BALI MATENDO na ndio maana nimezungumzia matendo yaliyopo kwenye video na sio maneno. Hata manabii wa uongo siku hizi wanasema maneno ambayo kama haupo makini huwezi kuwatofautisha na wanaohubiri injili ya kweli..Ila wachunguze matendo yao ndio utajua ukweli "Mtawatambua kwa matendo yao"...Na sio kila aniitaye Bwana Bwana atauona ufalme wa Mungu....Matendo ya kwenye wimbo nilioutaja hapo juu hayana tofauti na matendo ya kidunia ambayo biblia imesema yasifuatwe. Fanya jaribio: Mute sauti kwenye hiyo nyimbo kisha iangalie na ujaribu kumute nyimbo ya Harmonise na kuaiangalia...Kisha tofautisha kama utaweza kufahamu gospel ni ipi...Hata uvaaji wa wadada kwenye nyimbo hiyo sio unaokubalika....Bado kuna mtu atakuambia huyo ni nyimbo ya kuabudu!!!
Tuanze kwanza kwa kutofautisha waimbaji wa Injili na waimbaji wa nyimbo za dini.
Tuanze kwanza kwa kutofautisha waimbaji wa Injili na waimbaji wa nyimbo za dini. Nitajie wimbo mmoja wa Injili(Gospel) ambao msanii tajwa kauimba.Habari wana JF,
Moja kwa moja kwenye mada, kama tujuavyo neno Gospel maana yake ni Habari njema kwa watu wote (kutokana na imani ya kikristo). Na kuna waimbaji wengi (hatuwaiti wasanii maana hamna usanii kwenye dini) wanaimba kama njia ya kumtumikia Mungu.Wapo wengi kama kina Bahati Bukuku, Rose Muhando,Christina Shusho n.k
Mwanzo nilikuwa nasita kupinga kuwa Goodluck gozbert sio muimbaji wa Injili ila ni mziki wake ni wa Bongo flavour tu. Hili linajidhirisha vyema kupitia nyimbo yake ya 'Nibadilishe' ambayo ndani yake mahadhi ya nyimbo na style za kucheza hazitofautiani na zile za kina Harmonise, Diamond, Burna Boy n.k. Hii inaniaminisha kuwa huyu si muimbaji wa gospel bali anafanya Bongo flavour kwa kivuli cha dini. Kama hujaona wimbo huo...Angalia kwenye link hapa chini....
Sent using Jamii Forums mobile app