Goodluck Gozbert sio mwimbaji wa Gospel

Goodluck Gozbert sio mwimbaji wa Gospel

Coaster2015,
Mhh! Inatafakarisha sana, ndugu Coaster.

Naomba nisichangie chochote kwa sasa hadi nitakapokuwa tayari ila labda nitoe dokezo tu kabla sijarudi: Kiwango cha mtu kuwa amekosea au amepatia kinategemeana na upande wa senyenge aliosimamia na sio namna watu wengine wanavymtafsiri. Na pengine ndiyo maana mjadala unakuwa mrefu sana kwa sababu mtu anayeweza kulijibu hili swali kwa ufasaha ni Goodluck mwenyewe - yeye ndiye anajua ukweli na Mungu wake huyo anayemuimba. Sisi tunapiga porojo tu. Sina haja ya kuelezea hapa kwa sababu wewe ni mtu na unayo akili ya kutafakari.
 
Chachasteven, Wakati akijipanga kukujibu na mimi naweka maswali
1. Hivi mtu akija naaimba maneno Ysu ni mwokozi halafu yuko uchi vuuu lile na pipe kama sio papuchi unaiona ileee. Je anaimba gospel?
2. Je nikaimba na demu halafu nasikitika jinsi nilivyokuwa nawapiga vidole halafu naonyesha namoiga kidole demu sitejini au namuinamisha kuonyesha maisha yangu ya dhambi nilivyokuwa nawafanya, je nitakuwa naimba Gospel?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Omulasil,
Unaniuliza swali ambalo majibu yake unayo... Sijajua lengo lako ni nini, lakini nitakujibu. Jibu la swali la kwanza ni "hapana" na swali la pili jibu ni "hapana" na majibu ya maswali yako yote yanaweza kuwa "ndiyo." Inategemeana na Mungu unayemuabudu anafurahishwa na nini tu. Kama anapendelea uimbe uchi, basi upo sahihi kabisa - Ni gospel hiyo kwa mujibu wa Mungu wako.
 
😀😀
Akutane na hip hop halafu anaambiwa hiyo nayo ni injili😜
Troublemaker,
Lengo la mimi kumuomba jamaa akasikilize hiyo albamu ni kumrahisishia kuelewa muziki wa injili ni mpana kuliko anavyofikiria yeye. Wataalamu wa muziki wamekaa chini kuitafsiti hio albamu ni nyimbo za gospel licha ya midundo na rap system.

Staili ya uimbaji haijalishi. Kinachojalisha ni ujumbe unaoimba. Je unaakisi injili au unapinga. Kwa kipimo hicho cha ujumbe ndiyo maana halisi ya kuchuja ipi ni injili na ipi siyo injili.

Na wewe kasikilize hiyo albam halafu uje. Na kwa nyongeza kipindi Kanye anatoa hiyo albamu alisema haimbi tena nyimbo za kidunia, na hajabadilisha aina ya flow. Tofauti ni kwambwa anamsiu na kumuabudu Mungu (wake) kwa ku rap.
 

Attachments

  • Screenshot_20200120_222107.jpg
    Screenshot_20200120_222107.jpg
    62.6 KB · Views: 4
Lazima iwepo tofauti kati ya wana wa Nuru na wana wa giza.

Lazima iwepo tofauti kati ya mziki wa injili na muziki wa dunia.

Tofauti hii ionekane kuazia dhamira ya ndani, uvaaji wa wahusika, uchezaji wao n.k




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatutamtambua mtu kwa maneno yake bali kwa matendo...naona wengi wanampima Goodluck Gozbert kwa maneno yake!!,,,Very wrong hata Kanye West ametoa album inayomtaja Yesu ila ndani ya album kuna matendo mengi sana ambayo ni ya kufuru...Mnakumbuka mfano watoto wawili waliotumwa na baba yao kwenye biblia?,,,Mmoja alisema anaenda ila hakwenda na mwingine alisema haendi ila akaenda. Aliyetii amri ya baba yake ni yule aliyeenda alikotumwa. HATUPIMWI KWA MANENO BALI MATENDO na ndio maana nimezungumzia matendo yaliyopo kwenye video na sio maneno. Hata manabii wa uongo siku hizi wanasema maneno ambayo kama haupo makini huwezi kuwatofautisha na wanaohubiri injili ya kweli..Ila wachunguze matendo yao ndio utajua ukweli "Mtawatambua kwa matendo yao"...Na sio kila aniitaye Bwana Bwana atauona ufalme wa Mungu....Matendo ya kwenye wimbo nilioutaja hapo juu hayana tofauti na matendo ya kidunia ambayo biblia imesema yasifuatwe. Fanya jaribio: Mute sauti kwenye hiyo nyimbo kisha iangalie na ujaribu kumute nyimbo ya Harmonise na kuaiangalia...Kisha tofautisha kama utaweza kufahamu gospel ni ipi...Hata uvaaji wa wadada kwenye nyimbo hiyo sio unaokubalika....Bado kuna mtu atakuambia huyo ni nyimbo ya kuabudu!!!
 
Unamkataaje Gozbert unamkubali Rose Muhando?

Maajabu
Mkuu Chachasteven, Gozbert mimi mwenyewe nilikuwa namtilia mashaka sana mara niliposikia nyimbo zake kwa mara ya kwanza, lakini wimbo huu alioutoa ndio ulithibitisha kwamba huyo hakiki sio Mtumishi, yaani sio muimbaji wa Nyimbo za Injili bali huyo ni wale wanaoitwa wasanii wa nyimbo za injili, itoshe tu kutambua na hakuna haja ya kubishana hapa, naamini hata yeye mwenyewe analijua hilo, na anashangaa anapoona kuna watu wanamtetea, Kuimba Injili inataka Mtu uwe na Wito na pia Ushuhuda, sio kujiimbia tu kwa sababu unaweza kuimba, sijajua wewe msimamo wako kiimani ni upi, yawezekana unaweza kuwa unamtetea ukifurahi kuona jinsi anavyowapoteza watu wengi watakaochagua kumfuata, lakini kama wewe unatamani kuona watu wanapewa iliyo kweli kwenye Injili nadhani tusaidiane kuwakosoa watu kama Gozbert waache mara moja kusaidia wanaoutukana Ukristo kwa sababu ya style zao za Uimbaji, nakuhakikishia asipokemewa atakuja kufanya vituko sana kwenye aina hiyo ya uenezaji wa Injili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatutambambua mtu kwa maneno yake bali kwa matendo...naona wengi wanampima Goodluck Gozbert kwa maneno yake!!,,,Very wrong hata Kanye West ametoa album inayomtaja Yesu ila ndani ya album kuna matendo mengi sana ambayo ni ya kufuru...Mnakumbuka mfano watoto wawili waliotumwa na baba yao kwenye biblia?,,,Mmoja alisema anaenda ila hakwenda na mwingine alisema haendi ila akaenda. Aliyetii amri ya baba yake ni yule aliyeenda alikotumwa. HATUPIMWI KWA MANENO BALI MATENDO na ndio maana nimezungumzia matendo yaliyopo kwenye video na sio maneno. Hata manabii wa uongo siku hizi wanasema maneno ambayo kama haupo makini huwezi kuwatofautisha na wanaohubiri injili ya kweli..Ila wachunguze matendo yao ndio utajua ukweli "Mtawatambua kwa matendo yao"...Na sio kila aniitaye Bwana Bwana atauona ufalme wa Mungu....Matendo ya kwenye wimbo nilioutaja hapo juu hayana tofauti na matendo ya kidunia ambayo biblia imesema yasifuatwe. Fanya jaribio: Mute sauti kwenye hiyo nyimbo kisha iangalie na ujaribu kumute nyimbo ya Harmonise na kuaiangalia...Kisha tofautisha kama utaweza kufahamu gospel ni ipi...Hata uvaaji wa wadada kwenye nyimbo hiyo sio unaokubalika....Bado kuna mtu atakuambia huyo ni nyimbo ya kuabudu!!!
Aisee. Rose Muhando aliimba ameonja utamu wa yesu, mbona hatujalalamika kuona vitendo akiwa anauonja utamu kwenye video??
 
Tuanze kwanza kwa kutofautisha waimbaji wa Injili na waimbaji wa nyimbo za dini.
 
Saizi wapo wengi tu wanatumia dini kufanya business,hana tofauti nahawa wahubiri hewa wanauza mafuta,maji na ujinga jinga mwingine
 
Habari wana JF,
Moja kwa moja kwenye mada, kama tujuavyo neno Gospel maana yake ni Habari njema kwa watu wote (kutokana na imani ya kikristo). Na kuna waimbaji wengi (hatuwaiti wasanii maana hamna usanii kwenye dini) wanaimba kama njia ya kumtumikia Mungu.Wapo wengi kama kina Bahati Bukuku, Rose Muhando,Christina Shusho n.k

Mwanzo nilikuwa nasita kupinga kuwa Goodluck gozbert sio muimbaji wa Injili ila ni mziki wake ni wa Bongo flavour tu. Hili linajidhirisha vyema kupitia nyimbo yake ya 'Nibadilishe' ambayo ndani yake mahadhi ya nyimbo na style za kucheza hazitofautiani na zile za kina Harmonise, Diamond, Burna Boy n.k. Hii inaniaminisha kuwa huyu si muimbaji wa gospel bali anafanya Bongo flavour kwa kivuli cha dini. Kama hujaona wimbo huo...Angalia kwenye link hapa chini....



Sent using Jamii Forums mobile app

Tuanze kwanza kwa kutofautisha waimbaji wa Injili na waimbaji wa nyimbo za dini. Nitajie wimbo mmoja wa Injili(Gospel) ambao msanii tajwa kauimba.
 
Back
Top Bottom