Wadau nimeona mada nyingi zilianzishwa kwenye jukwaa hili zikihusisha google adsense ila wadau walioanzisha mada hizo hawakuongelea kwa upana kuhusu google adsense pamoja na dependencies zake:
kwenye uzi huu naomba mdau kama una shauku ya kuijua vizuri google adsense basi kaa mkao wa kula, nitaongelea vitu hivi:
Google adsense:-
- Google adsense ni nini
- Maudhui yapi yanaweza kuwekewa google ads
- Maudhui yapi ambayo hayana sifa kuwekewa google ad
- Website ili ipate google ads inapaswa kuwa na sifa zipi
- Google adsense estimate metric
- Invalid click and invalid traffic
- Jinsi ya kufungua blog
- Jinsi ya kufungua adsense account
- Jinsi unavyoweza kupokea malipo
Search engine optimization for blogger blog:-
- On-page SEO
- Off-page SEO
- Structured data (schema)
- Sitemap
- Jinsi gani ya kufanya website yako iaminike
- Search Engine Crawler | SE BOT
Analytical tools
- Google Analytics
- Session
- Bounce rate
- Userflow
- Search console
- Search perfomance
- Coverage
- Schema Markup Testing Tool | Google Search Central
Additional tool za kujichotea traffic
- Google news
- Google Discover
- facebook group
- telegram channel
- Facebook page
- verified insta account(optional)
- linkedin account
- Researchgate account
- pinterest account
- youtube channel
- more social media account if any
1. GOOGLE ADSENSE
1.0 Google Adsense ni nini?
Google Adsense ni programu inayoendeshwa na Google ambapo wawekaji wa maudhui kama makala, news article, machapisho ya blog, picha, video, au matangazo ya midia kwenye kurasa za wavuti wanaweza kujisajili kwenye programu hii na kuwa kama partner hivyo basi wakaweka ads space kwenye kurasa za wavuti na kuruhusu google kutangaza kwenye tovuti zao. Matangazo haya yanasimamiwa na Google.
wachapishaji (content publisher | content creator) wanaweza kujivunia mapato kwa kila mbofyo au kwa kila onyesho la tangazo (impression).
Note ni sehemu ya mafunzo:
Mfano wa website/blog yenye google adsense [
Kilimanjaroyetu]
1.1 Maudhui yapi yanaweza kuwekewa google ads
Ili tovuti yako iwe na sifa za kupata Google AdS, inapaswa kuwa na maudhui ya kipekee (unique content) ambayo yanavutia watembeleaji. Kabla ya kujisajili kwa Adsense, inapendekezwa ukague kurasa zako ili kuhakikisha kuwa ziko katika hali nzuri.
Note nilipochapa unique content haimanishi kwamba tovuti au blog yako iwe na content tu ambazo hazijawahi kuonekana kwenye Search engine hapa namaanisha add value kwenye content zilizopo angalau kuwe na uniqueness ukilinganisha na content za mwanzo utaelewa zaidi nitakapoelezea kuhusu schema (structured data)
1.2 Maudhui yapi ambayo hayana sifa kuwekewa google ads
Content zenye utupu
Sexually gratifying, maudhui yanayochochea ngono na/au yanayokusudiwa kusababisha msisimko wa kingono.
Mifano: content zinazoonesha matiti, matako, mavazi yanayoonesha utupu, sehemu za mwili za siri ambazo zimetiwa ukungu.
Discusses sexual fetishes
Mifano: Voyeurism, sadomasochism.
Maudhui yanayohusu burudani za ngono.
Mifano: Sherehe za filamu za ponografia, adult webcam services,
Maudhui yanyopromote biashara za ngono.
Mifano: Vichezeo vya ngono, genital enhancement tools
Hutoa ushauri kuhusu utendaji wa ngono.
Mifano: Vidokezo vya ngono
Maudhui ya kutisha
Picha za kuchukiza
Mifano: Damu, utumbo, majimaji ya ngono, uchafu wa binadamu au wanyama, picha za matukio ya uhalifu au ajali
Maudhui yanayoonyesha vitendo vya ukatili
Mifano: Akaunti au picha za risasi, milipuko, au milipuko ya mabomu
Maudhui yenye lugha chafu
Mifano: Maneno ya matusi au laana, tofauti na tahajia zisizo sahihi za lugha chafu
Maudhui kuhusu vilipuzi Vilipuzi
yanakuza uuzaji wa bidhaa ambazo zimeundwa kulipuka na zinaweza kusababisha uharibifu kwa watu au mali iliyo karibu.
Mifano: mabomu ya kemikali, mabomu au fataki .
Maudhui kuhusu uunganishaji, uboreshaji au upatikanaji wa vitu vinavyolipuka
Mifano: Miongozo ya kutengeneza mabomu; programu au vifaa vinavyokusudiwa uchapishaji wa 3D part za mabomu au vifaa vingine vya kulipuka.
Content zinazobariki biashara za madawa ya kulevya
References soma hapa: [
Google Publisher Restrictions - Google AdSense Help]
1.3. website ili ipate google ads inapaswa kuwa na sifa zipi
Kuna baadhi ya sheria na sifa ambazo Google inatarajia kutoka kwa tovuti yako
- Angalau machapisho 10 hadi 20 ya blogu yaliyofanyiwa SEO na yawe yameandikwa kwa google ads surppotive language
- Sera ya faragha (privacy policy)
- Kanusho (disclamer)
- Sheria na masharti (terms of service and condition) (ikiwa una chochote kinachohusiana na pesa)
- Contact us information
- Kikoa lazima kiwe cha top level domain .com, .in, .net, .info, E.t.c
- Chapisha Machapisho Yako Kwa Kuendelea
- hakikisha hakuna maudhui ya hakimiliki yaliyochapishwa kwenye tovuti yako.
- Tovuti lazima iwe na SSL certificate so user watumie https.
- Tumia responsive themes.
- Tovuti au blogu yako inapaswa kuwa na umri wa miezi 6. (Sawa, najua kwamba Google hawajatilia mkazo sana Timu ya Google Adsense endapo imereview tovuti yako na kuona ni nzuri vya kutosha basi wanaidhinisha hata ikiwa ina umri wa miezi 1-2.)
1.4. google adsense estimate metric
Page views
Ni mara ambazo ukurasa wa wavuti (webpage) umekuwa loaded kwenye browser single user anaweza akawatengeneza page view nyingi
Clicks (mibofyo)
Kwa matangazo ya kawaida ya Google, huhesabu mbofyo mtumiaji anapobofya tangazo.
Cost per Click (CPC )
Zabuni ya Gharama kwa mbofyo inamaanisha kuwa hiyo ndio gharama ambayo advertiser analipia kila mbofyo kwenye matangazo yake. Kwa kampeni za zabuni za CPC, advertiser anaweka bei kwa kila mbofyo - au "max. CPC" - hicho ndicho kiasi ambacho yuko tayari kulipa kwa kubofya tangazo lake.
kwa upande wa google adsense kwakuwa google ndio wanahandle matangazo ya advertiser so wanamodify CPC
matangazo huweza kuwa hata na cpc hadi $6 ila kibongo bongo cpc ikiwa juu sana ni $1, $2 au $3
kiwango cha ingizo lako la cku hukokotolewa kwa kuzidisha cpc
Estimate earn=CPC*Clicks
cpc=$0.05
clicks=300
Estimate Earn=$0.05*300
estimate Earn=$15
Note: nitaongelea mbeleni ni jinsi gani ya kuhusisha higher paid keyword, kutengeneza niche ya site pamoja na kufanya traffic segimentation yote haya ni kwa ajili ya kuongeza cpc
The page clickthrough rate (CTR)
uwiano (ratio) ya kubofya tangazo (CTR) ni idadi ya mibofyo ya tangazo gawanya kwa page views. CTR = Mibofyo / page views. Kwa mfano, ukipokea mibofyo 300 kwa page views 1000, ukurasa wako wa CTR utakuwa 0.3%. CTR ni kipimo cha ubora kama matangazo ya advertiser yanahusiana na machapisho yako endapo ads ni relevant na content zako bac CTR itakuwa kubwa
Impression
huhesabiwa kwa kila tangazo linapooneshwa kwenye kifaa cha mtembeleaji. Ni idadi ya matangazo yanayooneka user wanapofungua tovuti yako
mfano impression ni 10000 per day it means tovuti yako imeonesha matangazo elfu kumi kwa siku hiyo
Page RPM
(Page revenue per thousand impressions )Mapato ya ukurasa kwa kila maonyesho ya matangazo elfu moja (RPM) hukokotolewa kwa kugawa mapato yako yaliyokadiriwa (Estimate Earn) kwa idadi ya mara ambazo ukurasa umetazamwa, kisha kuzidishwa na 1000. page RPM = (Estimate Earn / page view) * 1000
mfano Estimate Earn =$15
Page view =10000
Page rpm=(15/10000)*1000
Page RPM=$1.5
1.5 Invalid click and invalid traffic
Invalid click(Mibofyo isiyo sahihi)
Mibofyo kwenye matangazo ambayo Google inachukulia kuwa si halali, kama vile kubofya bila kukusudia au kubofya kwa kutumia software (kama burpsuite, paros, httrack na spidering tools nyingine pia hata kama umeandika script yako ya kufanya spidering ya link).
Kila mbofyo kwenye tangazo huchunguzwa, Google ina mifumo ya kisasa ya kutambua mibofyo isiyo sahihi na kuiondoa kwenye click count. Google inapobaini kuwa mibofyo si sahihi, huichuja kiotomatiki na haitawekwa kwenye estimate earn pia ndio maana wakati mwingine unaweza ona ulikuwa labda umeingiza $15 ghafla zinashuka zinakuwa $10.
Hapa kuna mifano michache ya kile Google inaweza kuzingatia kuwa mibofyo isiyo sahihi:
- Wamiliki wa tovuti kubofya matangazo yao wenyewe ili kuongeza faida.
- Mibofyo kwa zana za kubofya kiotomatiki, roboti au kutumia spidering tool
- mtembeleaji wa tovuti anapobofya tangazo moja mara mbili, mbofyo wa pili ni invalid
invalid traffic (specific kwa ads si traffic za web)
Trafiki batili ni mfumuko wa mibofyo na impression kwenye tovuti ambayo haitoki kwa watumiaji halisi waliovutiwa na maudhui. Trafiki batili hutokea kwa bahati mbaya na kwa nia ya ulaghai.
Note: hichi ni chanzo cha watu wengi kufungiwa account zao, mimi pia sijafungiwa akaunti yangu ila ukweli ni kwamba nina trick ambayo kwa kiasi fulani inanitengenezea invalid traffic mfano unaweza angalia hapa uniambie wapi nimetric user [
President Samia Suluhu Announces New Teacher Positions in Tanzania in 2022]
Trafiki batili inajumuisha mibofyo au maonyesho yoyote ambayo yanaweza kuongeza mapato ya mchapishaji.
Trafiki batili inajumuisha
- Mibofyo itokanayo na wachapishaji wanapobofya matangazo yao ya moja kwa moja
- Mibofyo ya tangazo mara kwa mara kutoka kwa user mmoja
- mibofyo itokanayo na Wachapishaji kuwaomba/kuwataka user wabofye matangazo yao (mifano inaweza kujumuisha: lugha yoyote inayowahimiza watumiaji kubofya matangazo)
- Zana za kubofya kiotomatiki au vyanzo vya trafiki, roboti au programu nyingine potofu.
- mibofyo itokanayo na popup ads
- mibofyo itokanayo na popunder ads
Mibofyo kwenye matangazo ya Google lazima itokane na mambo yanayovutia users(visitor), na mbinu yoyote ambayo inazalisha mibofyo kwa njia isiyo halali imepigwa marufuku. google wakiona viwango vya juu vya trafiki batili kwenye akaunti yako, wanaweza kusimamisha au kuzima akaunti ili kulinda watangazaji na watembeleaji. Zaidi ya hayo, ikiwa hawawezi kuthibitisha ubora wa trafiki yako, wanaweza kuzuia au kuzima uonyeshaji wa matangazo kwenye tovuti yako. Kwa sababu ya mibofyo isiyo sahihi, unaweza pia kuona tofauti kati ya mapato yako yaliyokadiriwa (estimate earn) na actual earn.
google wanaelewa kuwa watembeleaji wengine wanaweza kuzalisha trafiki batili kwenye matangazo yako bila ujuzi au ruhusa yako. Hata hivyo, hatimaye ni wajibu wako kama mchapishaji kuhakikisha kwamba trafiki kwenye matangazo yako ni halali. Kwa sababu hii, google wanapendekeza sana ukague site yako ili kuzuia trafiki isiyo sahihi.
NITAENDELEA NA VIPENGELE NILIVYOBAKIZA KAMA UNA SWALI UNAWEZA ULIZA NA KAMA UNANYONGEZA KWA NILIYOKWISHA ELEZEA JAZILISHIA