Mahakama nchini Urusi imeiamuru Google kulipa faini ya $2.5 undecillion, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko utajiri wote wa Dunia kwa kukataa kurejesha akaunti za vyombo vya habari vinavyounga mkono Kremlin.
Kiasi hiki kimehesabiwa baada ya Google kuondoa channel ya urusi ya Tsargrad kwenye YouTube, kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya mmiliki wake.
Mwanasheria Ivan Morozov alisema Google ilitakiwa kuwajibika kisheria kwa kuondoa channels hizo. Ikiwa faini haitalipwa ndani ya miezi tisa, itazidishwa kila siku bila kikomo. Kampuni mama ya Google, Alphabet, iliripoti mapato ya zaidi ya $307 bilioni mwaka 2023, hali inayoonyesha kuwa ni vigumu kwa kampuni hiyo kulipa kiasi hicho.
Faini hii inakuja wakati Google ikikabiliwa na mashtaka matatu dhidi ya vyombo vya habari vya Urusi, huku ikituhumiwa kutokutekeleza amri za mahakama. Google pia ilisitisha ufadhili wa vyombo vya habari vya Urusi mara tu baada ya uvamizi wa Ukraine mwaka 2022.