GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo


ongezea TAMESA hapo! hawa jamaa ni tabu nyingine gharama ya services au matrngenezo ya magari hapo ni mara tatu zaidi ya bei ya mtaani. Sababu wao wenyewe hawana vifaa na mafundi so wanaisub contract kazi kwenda kwa garage za mtaani ambazo taasisi za serikali zinazuiwa kwenda moja kwa moja.
Naunakuta taasisi za serikali wanakarakana zao na hao TAMESA hawataki motokaa za taasisi hizo zitengenezwe na magereji mengini isippkuwa wao tu.
 
hivi gawio alitoa kwa mkuluuu?!
gpsa hata majengo yao hawapaki rangi kuonyesha uhai au ubunifu ofisi zimechooka sana na watumishi wamekata taamaa kwa mionekano yao.
wahusika wafanyie kazi hiki kwa kweli.
Duh..!!
Kumbe ishu hii ni serious?
 
hivi gawio alitoa kwa mkuluuu?!
gpsa hata majengo yao hawapaki rangi kuonyesha uhai au ubunifu ofisi zimechooka sana na watumishi wamekata taamaa kwa mionekano yao.
wahusika wafanyie kazi hiki kwa kweli.
Gawio lilitolewa kaka..
Kama mwanzo nilivoeleza, GPSA ni taasisi yenye vyanzo vingi vya mapato, mojawapo ni kumiliki visima vya mafuta Tanzania nzima na wateja wake sio wa kutafuta.

Huwezi kuwa na management yenye maslahi binafsi kwenye taasisi halafu utegemee taasisi ipate maendeleo. Hiki ndicho kilichopo GPSA,Kinachotokea ni kuwagawa wafanyakazi ili viongozi wawe wanapelekewa umbeya unaohusu madhambi yao ...matokeo taasisi imegeuka kuwa ya kimbeya, unafiki, majungu na morali na Ari ya kazi kwa watumishi ndani ya taasisi haipo kabisa. Yaani mtumishi ukiwepo GPSA unajiona kama umelaaniwa vile

Angalia namna Kitengo cha rasimali watu kinavyofanya kazi..kazi yao imegeuka kutafta habari za umbeya badala ya utawala...Hiki Kitengo kingevunjwa chote waletwe watu wenye kujua majukumu ya utawala.

Viongozi wanatumia Pesa nyingi kufanya uhamisho ambao sio wa maboresho na hauna tija kwa taasisi ila kwa sababu tu wamepata majungu kuhusu mtumishi....Special Audit ikifanyika hapa kuona gharama za uhamisho taasisi inayotumia na sababu zake wanaweza wasiamini watakachokiona..mtu mmoja anaweza kuhamishwa sehemu mbili ndani ya miezi4 na huko kote akalipwa mamilioni ya pesa...Sasa angalia hali ya ofisi zao zina hali gani halafu linganisha na gharama wanazotumia kuhamishahamisha watu.

Tungepata management kama ya MSD, GPSA tungekuwa mbali...yule CEO na DBSS hawana uwezo wa kuivusha GPSA zaidi wataididimiza kwa uroho na Ufisadi wao
 
Aisee! Hii ni hatari kubwa sana wanayoifanya. Bado nakuna kichwa ujasiri huo wanautolea wapi!?
 

Tatizo kubwa na huu ndio ukweli ni kwamba GPSA ilikuwa shamba la bibi huko zamani sasa hivi taasisi hii inafanya vizuri mno.

Tatizo watumishi wamekaa sehemu moja miaka na miaka kwa kuwa hakukuwa na uwezo kutoa stahiki za uhamisho, kwa sasa Wakala huu unavyopiga hatua kuongeza mapato inahamisha watumishi kwenda maeneo ya kukusanya mapato ya serikali ili kuchangia uchumi wetu, mbona wengine tumehamishwa na tumekubaliana kuwa ni kwa maslahi na hitaji la utumishi wa umma na hatulalamiki?

Wapo tuliohamishwa kwenda kwenye mikoa na sio kijijini ni makao makuu ya mikoa ya Tanzania bara kuongeza nguvu au kuongoza utamaduni huu haujakuwepo tangu GPSA imeanza na wapo waliohamishwa na idara kuu ya utumishi yani Wizara ya utumishi kwa kuwa ni kwa maslahi mapana ya umma nikiwepo mimi, watu waliokulia hapo hapo na ikaonekana tuhamishww kuleta maboresho kwa Wakala uliofikia hatua ya kufutwa kabisa kwa kuwa ulikuwa haujawahi kufikia lengo la kuanzishwa kwake, tumehama tulipewa stahiki zote kwa mujibu wa kanuni za utumishi!

Kwa mara ya kwanza bila kushurutishwa GPSA imetoa gawio serikalini ile awamu ya kwanza kabisa . Ni maendeleo makubwa mno na brand yake imekuwa kuliko miaka yote ya huo uongozi unaoonekana ulikuwa na afadhali! Na kama ni suala la watumishi posho, haijawahi kutokea hata siku moja miaka yote huko nyuma kuwa na posho hizo? Sasa hivi waliopo pale wanapewa! Sasa kwa nini tusione sasa hii ni mwanzo mzuri kwa uongozi uliopo? Mimi ambaye nimehamishwa ninaona maendeleo na haya hapa ni majungu ya baadhi yetu tuliohamishwa kwa maslahi mapana ya umma.

Pia uongozi wa serikali umeendelea kuboresha taasisi zake na baada ya muundo mpya wa GPSA wapo ambao ni viongozi nafasi zao hazikuwepo kwenye muundo huo mpya kwa sasa ndio wanataka kuongoza majungu haya. Ikumbukwe GPSA ina maslahi makubwa ya nchi.

Hiyo clearing inayotajwa tajwa inafanywa kwa kiwango kikubwa na hapa wengi wanaotaka kuhujumu serikali wana hasira kwa kuwa walikuwa na makampuni au wako nyuma ya makapuni ya watu binafsi tangu tukiwepo hapo. Sasa wanaumia kwa sababu biashara hiyo sasa inasimamiwa na GPSA yenyewe ujanja ujanja hakuna.

Ninashauri pia tuangalie zamani GPSA ilikuwa inatoa kiasi gani serikalini na sasa wanatoa nini? Na ni kwanini serikali ilifikia hatua ya kuifuta Wakala huo na kwanini leo hii serikali imewapa dhamana ya kugomboa mizigo yote ya serikali! Sio kwamba wameaminika?

Mimi niliekuwepo hapo GPSA ninaona kabisa baadhi yetu tumeanza kuhujumu umma na juhudi za serikali katika kuongeza mapato yake huu ndio ukweli. Tuache maslahi binafsi na taamaa zetu na badala yake tujikite kujenga nchi! Na tukumbuke kuwa sio lazima wote kuwa viongozi na tukiendelea hivi huku tulipo tutaonekana hatufai.
 
Mzee jakatugu wewe inawezekana kabisa ni mmojawapo mnaofisadi hii taasisi unajificha kwenye hoja dhaifu unazozitoa kwa mdada CuteJancs hebu pitia maandiko yangu humu halafu unisaidie kutoa majibu yanayoeleweka kabla hatujaendelea kufunua mafile mengine ukiangalia maandiko yangu nimeanza kuelezea Ufisadi tangu enzi za mwambega acha blah blah na uwe umejipanga kwelikweli hapa Mimi nataja majina kwenye reference usidhani naweka code.

Nakusubiri
 

Mkuu mimi niko hapa tangu 2017 wee upo tangu tarehe 2/4 siwezi kukimbia . Tukubali kwamba hii ni network yenu ya clearing iliyofutwa nyie ndio mliibia sana serikali na hamtaki kukubali kwamba nyakati zimebadilika serikali ina macho na inaona ukweli. Kubalini kwamba serikali imeamua kusimamia taasisi yake na si janja janja


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vipi kuhusu hoja za FRAME-19
Ndio maana namsubiri aje kabla sijapost andiko lingine hapa..

Aje akiwa amejiandaa hapa hamna umbeya Mimi nataja majina kabisa na nini wamefanya siweki code ili ajue tunafahamu.

Na ukipitia maandiko yangu nimezungumzia ufisadi tangu enzi za mwambega na kinachofanyika Sasa huyu mzee aache blah blah kama ametumwa huku akiwa na hoja dhaifu.

Nipo hapa namsubiri
 
Acha blah blah jibu hoja zangu kwa evidence sio swala la kuwepo JamiiForums...sema ni kampuni gani niliyokuwa nayo na inamilikiwa na nani?
 
Vipi kuhusu hoja za FRAME-19

Huwezi ukamjibu Frame- kwakuwa wote mna maslahi wote mlikuwa mnamiliki na mnatumiwa na wafanya bishara zamani kuhujumu serikali acheni tamaa msijifiche kwa uhuni wa kuharibu taasisi .


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huwezi ukamjibu Frame- kwakuwa wote mna maslahi wote mlikuwa mnamiliki na mnatumiwa na wafanya bishara zamani kuhujumu serikali acheni tamaa msijifiche kwa uhuni wa kuharibu taasisi .


Sent from my iPhone using JamiiForums
Wataje majina hao watu...huo ndio uzalendo tunaoutaka hatutaki umbeya...wewe taja utakuwa umeisaidia serikali kuwafahamu ili hatua zichukuliwe
 
Wataje majina hao watu...huo ndio uzalendo tunaoutaka hatutaki umbeya...wewe taja utakuwa umeisaidia serikali kuwafahamu ili hatua zichukuliwe

Wanajulikana mwingine hata jina lake linasadifu na nimemtaja hapo juu. Yeye na wenzake wanawake hao wawili. Wamebaki kudistabilize taasisi hata baada ya kuhama na mwingine kubaki hapo. Tujifunze kuwa watumishi na si wambea


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mzee jakatugu nijibu hili, unajua kwa nini CEO alimuondoa Aliyekuwa Mhasibu ( nadhani anaitwa amani) kama mwenyekiti kwenye kamati ya mapokezi ya Vifaa pamoja na kwamba alipendekezwa na PMU lakini jina lilipofika kwa CEO likakatwa na wote aliokuwa nao kwenye kamati iliyopita wakabakishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Afisa utawala (Ally) na mda mfupi akahamishiwa mkoani?
 
Mkuu itabidi nikupuuze naona kama unaleta umbeya kwa mambo yaliyo serious nimeshakuruhusu utaje majina kuvisaidia vyombo vya kiusalama kufanya kazi yao, humu ndani TAKUKURU, TISS na vyombo vya serikali vinasoma huu uzi wataje acha porojo za umbeya na hoja za kitoto

Ngoja nivute file lingine niweke hapa
 

Kwa bahati mbaya sana nimegundua haujui maana ya mhasibu, mhasibu ni Mtu mwenye CPA, nakumbuka wakati ninatoka amani alikuwa ni karani wa mahesabu. Lakini pia kiutendaji kazi ya CEO ni kupokea mapendekezo kijiridhisha na kisha kuamua,kama aliamua kumuweka au kutomuweka ni maamuzi yake kiutendaji


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilichogundua wewe utakuwa ni mfisadi unaweweseka...Nalog off ingia hapa saa2:30 usiku utakuta bandiko lililojaa ushahidi na watu watatajwa majina humo na Ufisadi waliofanya nikishindwa leo naliweka kesho mapema sana..

Hapa tunaisaidia serikali kupata taarifa za Ufisadi hatutoi umbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…