Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

Kwa zama hiz bado kuna mtoto wa maskini akiwa chuo anawaza hiv?
 
Kweli kabisa mzee

Kuna mtu wangu wa karibu aliwahi pata interview taasisi fulani ya serikali

Sasa kwa bahati nzuri kuna mzee mmoja ni senior memba pale taasisini anafahamiana sana

Akamwomba ampige tafu kwenye michongo ya interview ndani na nje atusue

Alikuja kosa na sio hakuwa na uwezo maana yuko competent sana Ila alipigwa chini hii yote ni kumtegemea mtu akushike shavu

Ikapita mwaka mmoja ile ile taasisi itangaza Tena ajira mwana akaomba this time akaenda fanys interview kimya kimya hakumpa mtu taarifa

Akapita na Sasa Ana kazi

Funzo :usimtegemee mwanadamu ,kuna watu hawawezi kukusaidia coz hawaoni umuhimu wowote kwako

Komaa mwenyewe kimya kimya kelele huwa zinaleta negative energy
 
Hahahaha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Smart911
 
MUNGU Ana maajabu sana
 
Dogo kumbe una kinyongo! Alafu unajiona maisha umeyapatiiia kweli au sio?
Ngoja, shida haziishagi.
 
Vijana waliopo chuo now second and third year ushauri wenu wadau wafanyaje hili kitaa wa ki mudu
 
Mnawajambisha sana waachane maana nasikia sasa namba ya wanafunzi wanaoacha chuo ni kubwa sana
 
Mkuu ushauri muhimu
Nilivyokuwa chuo nilikuwa nawaza mambo ya kitaa , mambo ya kujakupata kazi baadae .but kwa wakati huo haikusaidia zaidi ya kujiongezea mzigo wa stress

Ila kuna jamaa aliniambia kitu maliza chuo kwanza .kila mtu na njia yake aliondikiwa kupata ridhiki so hivyo viwaze ukimaliza .so we waza shule kwanza maliza then waza kinachofuata . unataka kuruka stage au [emoji2]


Halafu usiogope kuhangaika huko kupo tu we ninani kwenye dunia hii usihangaike mathalani umeumbwa wa kiume msoto upo

Jibu langu ni lile lile maliza chuo kwanza

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
sawa mkuu kweli bahati tumetofautiana kikubwa ni dua tu
 
Pole mkuu
 
Mtaani ni kubad asikwambie mtu. Mimi nimeacha chuo baada ya masuala ya ada kunipiga chenga na familia haina pesa. Nikaamua kurudi zangu nyumbani tu, huu ni mwezi wa sita sasa kila unakoomba kibarua hakuna yaani hadi zile zisizohitaji elimu kubwa hata darasa la saba anafanya hakuna kudadeki[emoji21].
Kibaya zaidi nikikutana na washkaji wananiambia mwanetu unanenepa tuu maisha safi ila hali yangu ya mkunga nikijikuna natoka unga. Bado tunasaka chochote cha kufanya ili mradi tusiwe mzigo kwa familia. Nachukia sana utegemezi especially nikijiangalia najiona umri unazidi kwenda.
Ila hopefully mambo yatakaa vyedi tu.
 
Kuna mwanangu alimaliza dip alichapika mpaka akabaki na suruali moja ili watu wasimuone kauka nikuvae akaanza kutembea usiku kama bundi.Alichapika haswa akanikopa cash akaenda kusoma driving.Shukrani Kwa sakata la vyeti feki akapata kazi Tanesco mambo safi.Tatizo lake moja tu kasahau alipotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…