Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

Graduates sikilizeni kutoka kwa malegend wa kitaa...

Unakosa hata jero ya vocha, unapoteza mpaka confidence halafu mademu ndio wanazidi kuwa wakali mamaaaee.

Zile illusion ulikuwa nazo kuwa ukimaliza chuo unapata kazi unamiliki ghetto kali na chuma chakutembelea zinayeyuka kama barafu mbele ya jua.

Ukimpigia mtu simu anakata hapo hapo hata kama unataka kumpa salamu anadhani unataka kupiga ukware.
Kwa zama hiz bado kuna mtoto wa maskini akiwa chuo anawaza hiv?
 
Hahahahah kuna ndugu hawawezi kumsaidia mtu yani yupo radhi akupige bata ila sio akupe mchongo! Ndugu wa aina hio huwa nawakwepa kama ukoma yani!

Mademu ni kweli kuna wanaochezea free kende bila mpango wa kazi kukamilika yani!
witnessj i remember that case
Kweli kabisa mzee

Kuna mtu wangu wa karibu aliwahi pata interview taasisi fulani ya serikali

Sasa kwa bahati nzuri kuna mzee mmoja ni senior memba pale taasisini anafahamiana sana

Akamwomba ampige tafu kwenye michongo ya interview ndani na nje atusue

Alikuja kosa na sio hakuwa na uwezo maana yuko competent sana Ila alipigwa chini hii yote ni kumtegemea mtu akushike shavu

Ikapita mwaka mmoja ile ile taasisi itangaza Tena ajira mwana akaomba this time akaenda fanys interview kimya kimya hakumpa mtu taarifa

Akapita na Sasa Ana kazi

Funzo :usimtegemee mwanadamu ,kuna watu hawawezi kukusaidia coz hawaoni umuhimu wowote kwako

Komaa mwenyewe kimya kimya kelele huwa zinaleta negative energy
 
Baada ya kuchakaa sana na mtaa,heshima home inashuka kwa kasi, madogo hawakuheshim tena,unaifikiria miaka yako mingi uliyoipoteza shule.
Unaiangalia gpa yako kali uliyoidotea chuo na kwauchungu sana unachukua tecno yako iliyopasuka kioo na kutype JF “natafuta kazi yeyote halali”.
Kutokana na kwamba uko broke unaandika vitu visivyoeleweka na detail chache kukuhusu.
Basi wanabodi walivyo na roho mbaya wanacomment ‘ngoja niwahi siti ‘ au ‘ngoja waje wakupe mwongozo’.


Aisee maisha haya omba yadikukute asee[emoji23]
Hahahaha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Smart911
 
Huwa namshukulu sana Mungu!! Asee

Japo Ndo Naingia kuisaka bachelor!!!
Sijachelewa sana!! Now 20's...

Nilipata mchongo nikiwa na 20 years!!! ...nazama kwa Government!!!!

Zaman sikuona thaman yake! Nadhan umri pia ulichangia!! Lakin Leo hii ndo naiona thaman yake:

Imagine namaliza form four tu!! Hata sikukaa sana kitaa!!.... Na wale!! Walioenda six!! Mpka degree!!!
Now day wengi nawapa company [emoji849]

Cha msingi mola ndo anaepanga!! Sis kama vijana kukata tamaa Ni mwiko:
MUNGU Ana maajabu sana
 
Brother wangu ni Advocate mkubwa tu hapa Tanzania ni class mate zake kina Lissu,Ngeleja, Feleshi huyu AG na wengine wengi!

Baada ya Chuo,nilijikomba sana kwake,Osha sana gari zake akiwa kazipaki pale kwake,peleka sana watoto wake shule,ukienda nae town, anakutambulisha huyu flani,yupo sehemu flani,huyu flani yupo sehemu flani! Kuna siku nimepiga interview PPF, enzi zile DG alikua William Erio,nikamwambia brother afanye mchakato huyu jamaa si hua tunakutana nae pale Leger Plaza Bahari Beach?? Jamaa akasema poa,nikaja kutana na Erio,nikamuuliza akasema hapana kaka yako hakuniambia lolote,Erio akavuta sharubu kwa brother,dogo anasema ulikua na ujumbe wangu,ni upi huo, brother akasema,nilipitiwa,nitakutafuta tuongee!

Niliporudi home,niliwashiwa moto hatari,namzaririsha kwa marafiki zake,naomba omba utadhani yeye hajui kama sina ajira,basi nikatulia zangu,nikawa naomba kudra za mwenyezi Mungu tu, jamaa mkienda bar mnakunywa beer hata za laki 3,na demu anakutafutia,anamlipa hata 50,000 ukachakate mbususu,lakini eti akupe pesa thubutu!

Pia nina brother wangu mwingine aliwahi kua DED enzi za Mkapa,Kikwete hadi kwa Magu mwanzoni ndiyo akasitaafu,nae alikuaga magumashi tu,sasa hivi ukimwona hata huwezi amini kama huyu ni Ex DED choka mbaya hama mbele wala nyuma,pesa zimeisha,karudi kijijini kwetu,ana stress ile mbaya,watoto wake wote hawana kazi,walisha jiunga na Mama yao,so dingi hana thamani tena!

Nilikuja saidiwa na mwana Jumuiya wenzangu, ndiyo alinipa connection,nikapata kazi,namshukuru sana yule Mzee,alishafariki lakini,Mungu amuweke mahala pema, Mwanga wa milele umwangazie, apumuzike kwa Amani!

Wanawake pia wanapata shida sana,anajikomba Weee,mwisho wa siku anachakatwa mbususu na kazi hapati,mwisho wa siku anakua na stress hadi unamuonea huruma!
Dogo kumbe una kinyongo! Alafu unajiona maisha umeyapatiiia kweli au sio?
Ngoja, shida haziishagi.
 
Mnawajambisha sana waachane maana nasikia sasa namba ya wanafunzi wanaoacha chuo ni kubwa sana
 
Mkuu ushauri muhimu
Nilivyokuwa chuo nilikuwa nawaza mambo ya kitaa , mambo ya kujakupata kazi baadae .but kwa wakati huo haikusaidia zaidi ya kujiongezea mzigo wa stress

Ila kuna jamaa aliniambia kitu maliza chuo kwanza .kila mtu na njia yake aliondikiwa kupata ridhiki so hivyo viwaze ukimaliza .so we waza shule kwanza maliza then waza kinachofuata . unataka kuruka stage au [emoji2]


Halafu usiogope kuhangaika huko kupo tu we ninani kwenye dunia hii usihangaike mathalani umeumbwa wa kiume msoto upo

Jibu langu ni lile lile maliza chuo kwanza

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nilivyokuwa chuo nilikuwa nawaza mambo ya kitaa , mambo ya kujakupata kazi baadae .but kwa wakati huo haikusaidia zaidi ya kujiongezea mzigo wa stress

Ila kuna jamaa aliniambia kitu maliza chuo kwanza .kila mtu na njia yake aliondikiwa kupata ridhiki so hivyo viwaze ukimaliza .so we waza shule kwanza maliza then waza kinachofuata . unataka kuruka stage au [emoji2]


Halafu usiogope kuhangaika huko kupo tu we ninani kwenye dunia hii usihangaike mathalani umeumbwa wa kiume msoto upo

Jibu langu ni lile lile maliza chuo kwanza

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
sawa mkuu kweli bahati tumetofautiana kikubwa ni dua tu
 
Me baada ya kugraduate nilipata kazi kwenye NGO flani, miezi miwili badae kazi ikaisha. Nikasugua bench hadi akiba ikaisha. Nikawa beach boy, daily bahari beach kuogelea. Nikapata marafiki wavuvi, nikajifunza uongo maana hakuna watu waongo kama wavuvi.

Anakudanganya wazi eti aliwahi kuona jini limesimama juu ya maji

Nilichakaa vibaya sana. Nikabaki na pens moja, suruali moja na tshirt mbili. Nguo nyingine ziliisha.
Pole mkuu
 
Mtaani ni kubad asikwambie mtu. Mimi nimeacha chuo baada ya masuala ya ada kunipiga chenga na familia haina pesa. Nikaamua kurudi zangu nyumbani tu, huu ni mwezi wa sita sasa kila unakoomba kibarua hakuna yaani hadi zile zisizohitaji elimu kubwa hata darasa la saba anafanya hakuna kudadeki[emoji21].
Kibaya zaidi nikikutana na washkaji wananiambia mwanetu unanenepa tuu maisha safi ila hali yangu ya mkunga nikijikuna natoka unga. Bado tunasaka chochote cha kufanya ili mradi tusiwe mzigo kwa familia. Nachukia sana utegemezi especially nikijiangalia najiona umri unazidi kwenda.
Ila hopefully mambo yatakaa vyedi tu.
 
Kuna mwanangu alimaliza dip alichapika mpaka akabaki na suruali moja ili watu wasimuone kauka nikuvae akaanza kutembea usiku kama bundi.Alichapika haswa akanikopa cash akaenda kusoma driving.Shukrani Kwa sakata la vyeti feki akapata kazi Tanesco mambo safi.Tatizo lake moja tu kasahau alipotoka.
 
Back
Top Bottom