Granit Xhaka ndio kuigharimu Arsenal mchezo wa leo, na ubingwa wa ligi

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Kwa wale ambao ni watazamaji wa mchezo wa mpira wa miguu wanajua kuna vitu vidogo sana ambavyo vinaweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo na kubadili na matokeo moja kwa moja

Kitu ambacho kimebadili mchezo wa leo wakati Arsenal ikiongoza 2-0 ni kitendo cha mchezaji wao Granit Xhaka kutaka kupigana na mchezaji wa Liverpool na wachezaji wenzake ikabidi waje kutenganisha na yeye kupewa kadi

Yaani tukio lile liliondoa concentration au focus ya wachezaji wa Arsenal mchezoni na kusababisha Liverpool kurudisha goli moja sekunde chache zilizofuata

Baada ya Liverpool Kurudisha goli moja , basi motivation/morali yao ikapanda maradufu na matokeo yake ndio yaliyotokea
 
Xhaka ni mkorofi sana na ile game ingekuwa ugomvi mtupu..
 
Kocha ndie aliye igharimu timu, kwanini uzuie wakati uwezo wa kucheza unao? Unawezaje kuzuia karibu dk 50 wakati sio fani Yako.
Alitakiwa aendelee ku push kwakua Liverpool walikua wanafanya makosa mengi. Ata Liverpool ikiwa mbovu ni ngumu kuwazuia pale kwao Kwa dk nyingi.
 
Ningeshangaa eti hiyo arisenali mbov ibebe ubingwa! Asante liva kwakututolea ka uzibe leo.
 
Kwa wale ambao ni watazamaji wa mchezo wa mpira wa miguu wanajua kuna vitu vidogo sana ambavyo vinaweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo na kubadili na matokeo moja kwa moja

Kitu ambacho kimebadili mchezo wa leo wakati Arsenal ikiongoza 2-0 ni kitendo cha mchezaji wao Granit Xhaka kutaka kupigana na mchezaji wa Liverpool na wachezaji wenzake ikabidi waje kutenganisha na yeye kupewa kadi

Yaani tukio lile liliondoa concentration au focus ya wachezaji wa Arsenal mchezoni na kusababisha Liverpool kurudisha goli moja sekunde chache zilizofuata

Baada ya Liverpool Kurudisha goli moja , basi motivation/morali yao ikapanda maradufu na matokeo yake ndio yaliyotokea
Sio mara ya kwanza Arsenal kuongoza Liver wakarudisha magoli, nakumbuka kuna mechi kama sikosei ilikuwa ni FA Arsenal walikuwa wanaongoza goli tatu bila, mwisho wa siku Arsenal alilala kwa bao tano kwa tatu, hivyo usimsomange Xhaka wa watu.
 
Hii mechi ndo ilikuwa ya kutengeneza mazingira ya ubingwa.,basi ndo hivyo hatuwezi kumzuia city kubeba ubingwa
 
Washukuru Klopp alifanya silly sub akamtoa Jones badala ya captain. Jones jana alikuwa na game nzuri sana. Angebaki na Thiago akaingia arsenal wangekuwa kwenye wakati mgumu sana.
 
Kwa wale ambao ni watazamaji wa mchezo wa mpira wa miguu wanajua kuna vitu vidogo sana ambavyo vinaweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo na kubadili na matokeo moja kwa moja

Kitu ambacho kimebadili mchezo wa leo wakati Arsenal ikiongoza 2-0 ni kitendo cha mchezaji wao Granit Xhaka kutaka kupigana na mchezaji wa Liverpool na wachezaji wenzake ikabidi waje kutenganisha na yeye kupewa kadi

Yaani tukio lile liliondoa concentration au focus ya wachezaji wa Arsenal mchezoni na kusababisha Liverpool kurudisha goli moja sekunde chache zilizofuata

Baada ya Liverpool Kurudisha goli moja , basi motivation/morali yao ikapanda maradufu na matokeo yake ndio yaliyotokea
Kitendo alichafanya ni cha kijinga kweli kweli. Huyu mchezaji ana tatizo la hasira. Kwake hakuna jambo dogo. Nakubaliana na wewe kuwa wanaosema yeye ndiye alibadilisha mchezo wanaweza kuwa sahihi. Arsenal wangeenda mapumziko wakiwa mbele 2-0, pengine ingekuwa game tofauti kabisa. Kwenye mpira wa miguu hakuna kitu kibaya kama unapokuwa mbele 2-0 uruhusu mpinzani wako apate bao moja wakati muda bado upo.
 
come back kwenye mpira si jambo jipya
Ni kawaida hata Liverpool alimtangulia Madrid baadae wakapoteza nnacho maanisha huwezi kuwa unataka kuwa bingwa unacheza kizembe hivyo bora ushinde goli 1 ulilinde kuliko goli mbili unachomolewa
 
Arsenal hana mentality ya ubingwa, huwezi ukawa uko kwenye final stages za race halafu unadrop points kijinga hivyo.

Angalia race za city vs liva zinavyokuwa, hakuna aliyekuwa anafanya ujinga wa namna hiyo.
 
Back
Top Bottom