Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Huu ni ushauri wangu kwa wana JF wote ambao wamekuwa wakijadili zaidi watu (viongozi wa kisiasa) zaidi kuliko mambo yanayohusu taifa.
Ukweli ni kwamba, kwa sasa taifa letu limegawanyika kiitikadi/ufuasi pengine kuliko wakati mwingine wowote.
Hii inatokana na kuwepo makundi ya wanaojadili utawala wa kiongozi aliyepo madaraka kwa sasa na yule aliyefariki akiwa bado madarakani.
Hii ndio hasa tofauti kati ya siasa za hapo kabla na hizi za sasa. Kwani, kwa sasa ni vigumu kupata mrejesho toka kwa mmojawao ambaye hayuko tena duniani.
Awamu zilizopita ilikuwa ni rahisi kupata mrejesho hata kwa kuwahoji wahusika. Na ndio maana wengine wametumia fursa ya kuwa kwao hai kwa kuandika vitabu vya historia zao.
Wanajf, hebu tujikite zaidi katika kujadili maendeleo ya taifa letu kisiasa, kiuchumi na hata kijamii.
Madhaifu ya viongozi waliopita yatusaidie kujifunza na kutafuta mbinu za kukabiliana nayo.
Aidha, tusione shaka kuwashauri viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Badala ya kuwakosoa au kuwalinganisha na waliopita, tujitahidi kutoa maoni ya namna bora ya kuboresha maslahi ya taifa.
Kuendelea kulumbana kwa kuwapambanisha viongozi waliopo na wasiokuwepo madarakani, haitasaidia kustawisha taifa; na badala yake kutazidi kuligawa taifa!
Mwenyezi Mungu aibariki na kuistawisha Tanzania!