Wakati Mungu anataka kuwatoa Wana wa Israel kutoka utumwani (Misri) alilazimika kuandaa kiongozi aitwae Musa.
Musa alipoishia njiani, Joshua alichukua kijiti na kuwafikisha watu wale nchi ya ahadi.
Tanzania ilibahatika kupata kiongozi wa kwanza JKN ambae sio tu alipigania uhuru wa nchi hii, bali alituunganisha kuwa taifa z nchi yanye makabila zaidi ya 120.
Akaja na JKT kuwaunganisha Watanzania.
Shule za sekondari zilichukua watu across the country.
Ili tupate mustakabali bora wa kesho yetu Watanzania, lazima tuwe na kiongozi madhibuti, mwenye maono anaeweza kujenga taasisi ambazo zitasimamiwa na watu (viongozi) ili kufikia matarajio yetu.
Hivyo, lazima tumguse Mkulu wa sasa kuona kama anachokifanya, kina akisi matarajio yetu kuifikia Tanzania tunayoitaka.
Leo tunalia kukosa uhakika wa mafuta ya kula na kupanda kwa bei za bidhaa kama ngano.
Moja ya nchi inayouza ngano na robo ya mafuta ya alizeti duniani ni Ukraine.
Ukraine ni theluthi mbili ya size ya Tanganyika.
Wamekuwa na aina gani ya uongozi wa nchi na kisekta kwenye kilimo-biashara, ili kukumata soko la mauzo ya mafuta ya alizeti duniani.
Kuna msemo unasema 'Proper leadership and management are key factors for a country to take off'
Je tuna aina ya uongozi na viongozi kwenye taifa na sekta chungu mzima ambao wakionesha uongozi na management sahihi, kuwafanya Watanzania wajione wana mchango kwenye kukuza uchumi wao binafsi na kutokuendelea kutembeza 'bakuli' duniani?
Happy Easter Monday!
Sent from my M2006C3LG using
JamiiForums mobile app