Green Card kumbe ni kweli aisee tucheze hii kitu

Kama hawajabadilisha, unapewa 6 months ya kwenda US (LAZIMA)!! Sasa kama ni miezi 6, manake unaweza kufanya booking ya ticket miezi 6 kabla ili kubana matumizi ya fare. Ukifanya booking mapema zaidi, unaweza kupata tickets za chini ya $1000! Ukifika US, unaenda zako sehemu kama Texas ambako jimbo ni tajiri, michongo mingi, lakini apartments ni cheap ukilinganisha na majimbo kama New York. Huko unapata hata kwa $500. Kwahiyo, Kibaharia Sh 10M inatosha kabisa kwenda kuanza mapambano! Usisahau, watu kibao tu wanaingia US wakiwa hata $100 hawana, na hawaajiriki kwa sababu hata kama umeenda kihalali, lazima uwe na work permit, na hilo ndilo linalowakwamisha wengi! Wewe tayari unayo GC, kwahiyo siku ya pili tu, unaweza kuingia mtaani with confidence. Kwa kuanzia sio lazima upate kazi ya ofisini. As long as unayo GC, kupata vibarua itakuwa rahisi kwa sababu sio radioactive material!
 
Sasa kama uko na family basi inabidi uwe na kama dollar 10,000 kwa ajili ya kuku sort
 
Mkuu hivi hakuna uwezo wa mtu kuomba mara nyingi kwa wakati mmoja kwa kubadilisha badilisha majina kweli.
Huwezi kufanya uo upumbavu maana inatakiwa uwe na hati ya kusafiri zaidi ya moja. Picha za passport zaidi ya moja. Nchi unayotoka iwe ni zaidi ya moja. Elimu yako iwe tofauti Mara diploma, Mara degree, Mara form six na majina yawe tofauti tofauti kwenye vyeti. ..ukifaulu hapo wewe ni zaidi ya mchawi
 
Safi sana mkuu. Umetoa details za kutosha. Nimejifunza mengi.

Ila hata baadhi ya nafasi za usalama wanachukua hasa za jeshi. Kigezo uwe na green card au uraia na uwe chini ya miaka 35. Kama umri umezidi 35 na si zaidi ya 37 ni hadi uombewe kibali maalum. Wao jeshi linaajiri kila siku.
 
Figo, Moyo, etc viungo etc.
Hii nilishuhudia nilipokuwa majuu, raia wa kichina wanaandamana kupata support kupinga vitendo vya watu kutolewa viungo vyao.......nafikiri ni wale wanaokuwa wamefungwa magerezani ndo waathirika zaidi wa kugemwa viungo. Sijasikia kama kwa mabeberu hili nalo lipo....
 
Wakuu mi najaza sehemu ya zipcode ndio sielewi.. msaada
Unajaza vipi wakati bado?! Au unazungumzia siku za nyuma?! Anyway, Google "Tanzania Zip Codes" na utakuta document ya TCRA ambayo imetaja zip code ya kila eneo. Ukiona hiyo doc, anza kutafuta mkoa wako, kisha wilaya yako, halafu kata yako, na hatimae utaona zip code ya eneo lako!
 
Kama hujapata nauli na miezi sita imepita hapo inakuwa vipi....huu uraia wa green card unakoma baada ya muda gani?
 
Sina uhakika kama wamebadili utaratibu lakini kwa zamani ilikuwa ukimaliza ile miezi 6, wanaku-cancel out!
Hapo ndo utaona namna beberu anavyotaka kuwafanya binadamu kutoka ulimwengu wa tatu kuwa watumwa wa kifikra.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…