Huwa inaanza October
Kwa kifupi kabisa, Green Card Lottery, formally DV Lottery ni bahati nasibu inayoendeshwa na serikali ya Marekani ambapo kila mwaka, inachagua applicants 50K randomly kutoka sehemu mbalimbali duniani, na hawa applicants hupewa Green Card. Ukipata Green Card unakuwa ni kama Mmarekani tu, kwa sababu unakuwa na haki
karibu zote wanazopata raia wa Marekani. Linapokuja suala la ajira, unakuwa na haki ya kufanya kazi hadi serikalini EXCEPT, kwenye nafasi nyeti hususani za usalama!
Hulipii hata sent 5, lakini ukishinda, ni wajibu wako kulipia makaratasi ya hapa na pale lakini sio ghali sana! Aidha suala la utafikaje US, na utaenda kuishi wapi na vipi ni wajibu wako mwenyewe! Mwaka jana waliingiza utaratibu mpya kwamba kama unataka kuomba basi ni lazima uwe na passport. Kama tayari una passport, basi subiri October 07, kisha ingia
hapa kwa ajili ya kujiandikisha! Condition nyingine (kama haitabadilik) unatakiwa kuwa na angalau diploma!