Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Aseeee,

Umejibu kwa hekima,kufunza, na kutamanisha.
 
mkuu una hatari kubwa sana, nitakutembelea hapo nione how you are leading your life kiasi cha kuona kuishi tanzania ni upuuzi mtupu kwakuwa hakuna umeme, maji wala hewa ya oxygen. Yaani unaona maisha bila kuishi Marekani hayawezekani kabisa. Ninawasihi vijana tena na tena na tena kuwa ni wahamiaji wachache sana wanaofanikiwa kule Marekani, majority wanaishia pabaya sana na kufanya donkey jobs ambazo hata huku zinakutoa na zina heshima. Mwenye afadhali ni yule mwenye ujuzi unaohitajika kule baasi, unemployment rate is very high na viwango vya uhalifu viko juu sana, wenye rangi nyeusi wengi wako magrezani believe me. Huyu jamaa hayuko Marekani amehadithiwa tu habari za Marekani, is a layer. Tatizo kubwa la Marekani ni ukosefu wa ajira baada ya viwanda vingi kuhamishiwa Asia kupunguza cost of production (gharana za uzalishaji kuwa kubwa) baada ya watumwa kudai haki zao na malipo makubwa ya kazi na masaa. Hii tabia ya ushoga kule haikuja hivihivi tu kijingajinga bali maisha magumu yaliwalazimisha kuhalalisha tabia hiyo. Asikudanyange mtu, ukiona deal is so good think twice. Kama huna elimu inayohitajika kule usiende kuishi kule badala yake tembea tu kisha urudi, nenda kasome kisha urudi.
 
I doubt about your cleanness and integrity, sisi tupo huku na Mungu anatupa mkate wetu wa kila siku, tuna amani ya moyo. Naweza kujiuliza ni kwa namna gani nijute eti kwasababu siishi Marekani, utahitaji akili fulani kufanya hivyo, yaani ndoto yako ni kuona vijana wote wanahamia Marekani na kuikimbia nchi yao.
 
Hivi Kuvulata unasoma notes nini? Maana ni kama mtu aliyeko Marekani anaposoma notes za poverty ya Africa, nimesoma development economics, najua kutumia data ziseme nachotaka kusema!
Anyway kwa kukutarifu niliingia Marekani kwa Greencard, na nimechukua uraia wa Marekani kwa hiari yangu! Sikulazimishwa!
Siku ya kuapishwa kuwa raia, ofisi zilifunguliwa asubuhi na kufungwa jioni,kulikukuwa na makundi makubwa mno ya watu! Cha ajabu waafrika tulikuwa sana! Maybe 2% Mchanganyiko toka nchi mbali mbali,Brazil, China,Korea, India, Mexico...Ulaya nk! Nchi ambazo hawajawahi hata kuchukuliwa manamba! Hivi hao wote ni wapuuzi!
Na kwa taarifa tu,ukisikia illegal immigrants,Waafrika ni aslimia ndogo kabisa! Na hata number ya legal immigrants toka Africa, number yetu ni ndogo mno!
Watu wanatoka sehemu mbali mbali za dunia kuingia US! Wenye pesa kuja kuweka investments zao, na wengine kutafuta wanachokitafuta!
Kijana wangu marafiki zake chuoni walikua toka Italy, Korea na India, wako IBM,Google! Wote ni wahamiaji!
Walimaliza University hata hawakusubiri ajira!
Kama huo ndio umanamba,watched wawe manamba!
 
Huo ndio umanamba mamboleo, brainwashed, Sio vibaya kuishi Marekani kama mkimbizi lakini ni vizuri zaidi kuishi kwenye taifa lako mkitafuta majibu ya matatizo ya jamii yenu. Yaani wewe unatamani usikie Elon Musk ameinunua Tanzania kwa bei ya kutupwa.
 
Hayo ni mawazo yako...lakini kuna mahali ulisema unajenga nchi! I hope unajenga kweli, maana tunawajua mno wanaotafuna nchi! Huwa tunawaona wanapokuja kufanya shopping huku!
 
Sijaja Marekani kama mkimbizi! Nimekuja kufuata ndoto zangu ambazo siwezi kuzipta Tanzania!
 
Hata mimi mbona ninazo kadi za membership wa Walmart na TCF Bank? hii haimaanishi kitu kikubwa sana.
 
Chief huwez kujifunza lolote ukiwa mazingira yale yale na watu wale wale. Ndio maana nikasema ingekuwa ni uwezo wangu ningewatoa watanzania waende huko nje hawatarud watupu kuna kitu kitabadilika. We umesemea watu waliochoka tu lakin kuna wengine wameenda na wamekuja na mawazo mapya. Kuhusu utumwa upo popote hata bongo upo ila huwez kuuona coz sio eneo lako. Hiv unajua uchumi wetu hapa bongo unamilikiwa na wahind na Waarabu? Wenyeji wamebaki kuongea tu hawana habar na ulimwengu unavyokwenda. Leo hii wasomali na ukorofi wao cku wakirud kwao wakikaa kwa aman wanatupita. Kisa ninini wengi sana wanajua how things work coz tayar wana exposure ya kutosha.
 
Hayo ni mawazo yako...lakini kuna mahali ulisema unajenga nchi! I hope unajenga kweli, maana tunawajua mno wanaotafuna nchi! Huwa tunawaona wanapokuja kufanya shopping huku!
hahaha! sio mimi! lakini nitakuwa wa mwisho kuikimbia nchi yangu, I can not let my country go to the dogs just because of greener pastures.

Vijana take my words, success rate for immigrants in the US is only 30%. Na kati ya hao 90% ni wale wenye elimu na ujuzi unaohitajika marekani, vinginevyo utakwenda kuchuma matofaa, kuchunga ng;ombe, kuosha magari, kushikishwa ukuta
 
Hakuna umanamba kama kuwa chawa wa ccm!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…