GSM inawadharau models wa Kitanzania? Why Zari?

GSM inawadharau models wa Kitanzania? Why Zari?

Matola!! Acha ubaguzi wa kijinga kabisa!! Vipi ingekuwa ni celeb wa kibongo kaalikwa kufungua duka nje ya Tz, ungeandika nn? Hii ni Africa mashariki na tunajaribu kuunganika we unakuja na mawazo yako mgando. Sijawahi kumtukana mtu hapa JF na pia nachelea kukutusi pia ila naomba ubadili msimamo wako.
 
Sidhan kama ananyonyesha yule kila siku kiguu na njia nahisi mtoto keshaanzishiwa maziwa ya kopo ndo maana akadai pesa ndefu za matunzo. Huko nairobi kaalikwa na yule shosti ake aliyemtumia kuvujisha picha akiwa na dai kitandani
ha ha ha aseee
 
Pia usisahau Zari kazaa na Dai na watoto ni watz so acha wivu wa kipumbavu
 
Kwanza kabisa napenda niwatakie Sabbatical njema, pili leo ni Nyerere day, nitamuenzi baba wa Taifa kwa njia hii.

Kwanza naomba nikiri huyu Zari mimi namsikia jina tu sijawahi kujuwa hasa kwa hakika shughuri zake ni nini zaidi ya kujuwa ni hawara wa msanii Diamond that's it. Huwa sina muda wa kudiscuss drama za watu wa aina hii lakini kwakuwa hili la zari lipo in economics grounds naomba nitowe maoni yangu.

Kwa maoni yangu ni dharau kwa Watanzania GSM kumleta Zari kuzinduwa hilo duka lao la Danube nadhani kwa maoni yangu mtu sahihi walipaswa wamuite Diamonds kufanya uzinduzi huo

Kwakuwa Watanzania sasa hivi ni mashabiki ushuzi wa Team ushuzi hawawezi kunielewa wala kukubali kitendo hiki ni dharau kubwa imefanywa na GSM dhidi ya models wetu, kumleta mganda halafu utegemee wateja Watanzania huu ni ufala uliopitiliza.

Binafsi yangu natangaza rasmi boycott bidhaa za duka hilo la Danube kwa kitendo hiki cha kutowapa support models wetu kufanya jukumu hilo.
Tunao kina Mbwana Samatta, Flavian Matata, yupo Joti yupo Masanja, yupo mzee Majuto why Zari? Zari ni Celeb wa nini jameni naomba kujuzwa.
Binafsi sio mdau kabisa hata wa hao celeb wa kibongo ila mkuu kwa hili la zari lipo sawa kwa sababu ni mtu maarufu na mwenye mvuto kwa watanzania kuliko ma celeb wengi wa hapa nyumbani
 
Kutangaza biashara lazma uangalie mtu anaeuzika, kwa hapa bongo wema sepetu anafaa sana, yani alitakiwa atangaze hadi matangazo ya chips snacks tatizo lake unalijua kabisa hajielewi
Sasa mnataka makampuni yafanyeje
Huyu Wema watanzania tulimpa ushauri hadi tukachoka .....
 
Zari ni Mtanzania pia,
Mwanamume mtanzania akimuoa msichana wa nchi nyingine basi msichana huyo huwa Automatikali Raia wa Tanzania.
Ila Raia mwanamue wa nchi nyingine akimuoa msichana mtanzania, hawi raia wa Tanzania, inaogopwa kuwa watu ambao sio raia wasijetumia njia ya kuoa kupata uraia.
Zari Hassan ni Raia wa Tanzania wa kuolewa.
Kuna uraia wa Kuomba, Kuzaliwa, Kurithi, Kupewa, Kuwa Tanzania kabla ya Uhuru wa Tanganyika, na Kuolewa.

Zari ni Mtanzania wa Kuolewa.
Msimbague ni Mtanzania mwenzenu.

Zari Ze Boss Lady.
 
Huyu Wema watanzania tulimpa ushauri hadi tukachoka .....
Wema angekua anajielewa ni bonge moja ya Brand, yani nadhani ndo angetakiwa kuwa boss lady wa East Africa, alikua na diamond akaanza kupanda nae stejini anakata mauno na kina iyobo, basi tena hakujijua na muda ndo huoooo
 
Wema angekua anajielewa ni bonge moja ya Brand, yani nadhani ndo angetakiwa kuwa boss lady wa East Africa, alikua na diamond akaanza kupanda nae stejini anakata mauno na kina iyobo, basi tena hakujijua na muda ndo huoooo
Nakumbuka haya anayo yafanya Zari tulimshauri sana tena sana kwenye hili jukwaa Wema kama angelisikia hakika angekuwa anapiga hela ndefu sana.....ni lazima watu wakubali kuwa Zari kwa sasa ana heshimika kibiashara kuliko Wema....
Wafanya biashara wote hawaangalii undugu wala uzalendo bali ni fursa ya kutengeneza hela.....
 
Uliyeleta Uzi acha dharau, si Kila mtu ana akili kama zako.
 
TAZAMA Mwenyewe Zari The Boss Lady Ilivyokuwa Shangwe katika uzinduzi wa Mall | Dar Es Salaam
 
Back
Top Bottom