Kwanza kabisa napenda niwatakie Sabbatical njema, pili leo ni Nyerere day, nitamuenzi baba wa Taifa kwa njia hii.
Kwanza naomba nikiri huyu Zari mimi namsikia jina tu sijawahi kujuwa hasa kwa hakika shughuri zake ni nini zaidi ya kujuwa ni hawara wa msanii Diamond that's it. Huwa sina muda wa kudiscuss drama za watu wa aina hii lakini kwakuwa hili la zari lipo in economics grounds naomba nitowe maoni yangu.
Kwa maoni yangu ni dharau kwa Watanzania GSM kumleta Zari kuzinduwa hilo duka lao la Danube nadhani kwa maoni yangu mtu sahihi walipaswa wamuite Diamonds kufanya uzinduzi huo
Kwakuwa Watanzania sasa hivi ni mashabiki ushuzi wa Team ushuzi hawawezi kunielewa wala kukubali kitendo hiki ni dharau kubwa imefanywa na GSM dhidi ya models wetu, kumleta mganda halafu utegemee wateja Watanzania huu ni ufala uliopitiliza.
Binafsi yangu natangaza rasmi boycott bidhaa za duka hilo la Danube kwa kitendo hiki cha kutowapa support models wetu kufanya jukumu hilo.
Tunao kina Mbwana Samatta, Flavian Matata, yupo Joti yupo Masanja, yupo mzee Majuto why Zari? Zari ni Celeb wa nini jameni naomba kujuzwa.